F. A. Hayek’s , “Competition as a Discovery Procedure”

USHINDANI KAMA UTARATIBU WA UGUNDUZI

F.A. HAYEK

IMETAFSIRIWA NA MARCELLUS S. SNOW

I.

Haingekuwa rahisi kutetea wachumi wakubwa dhidi ya shtaka kwamba kwa miaka 40 au 50 wameuchunguza ushindani kwanza kwa dhana ambazo, kama zingekuwa kweli hasa, zingefanya ushindani kutokufaa na kutokuvutia kabisa.  Iwapo mtu yeyote kweli angejua kila kitu kuhusu nadharia ya uchumi inayotajwa kama “data”, ushindani hakika ungekuwa ni mbinu isiyofaa ya kupata marekebisho ya  maelezo haya.  Kwa hiyo, haishangazi kuwa baadhi ya waandishi wamehitimisha kwamba tunaweza ama kuacha soko, au kwamba matokeo yake yanapaswa kuzingatiwa sanasana kuwa hatua ya kwanza kuelekea katika uanzishaji bidhaa ya jamii ambayo tunaweza kutengeneza, kurekebisha, au kuisambaza upya kwa namna yoyote tunayotaka.  Wengine, ambao inavyoonekana wamechukua dhana yao ya ushindani mbali na vitabu vya kiada vya kisasa, wamehitimisha kuwa ushindani huo haupo kabisa.

 

Kinyume chake, ni muhimu kukumbuka kuwa kila tunapofanya ushindani, hili linaweza kuthibitishwa tu kwa sisi kutokufahamu mazingira ya lazima ambayo yanaukilia tabia ya washindani.  Katika

 

____________________

Marcellus S. Snow ni Profesa mstaafu wa Chuo Kikuu cha Hawaii huko Manoa; Snow@hawaii.edu.  Hii ni tafsiri kutoka Kijerumani ya F.A. Hayek’s “Der Wettbewerb als Entdeckungsverfahren,” mhadhara wa 1968 uliodhaminiwa na Institut für Weltwirtschaft katika Chuo Kikuu cha Kiel.  Ilichapishwa kama Na. 56 katika mfululizo wa Kieler Vortäge.

 

michezo, mitihani, utoaji wa mikataba ya serikali, au utoaji wa tuzo kwa ajili ya mashairi, bila ya kutaja sayansi, itakuwa upuuzi mtupu kudhamini shindano kama tunafahamu mapema mshindi atakuwa nani.  Kwa hiyo, kama mada ya mhadhara inavyopendekeza, napenda sasa kuuchukulia ushindani kimfano kama utaratibu wa kugundua ukweli ambao, kama utaratibu usingekuwepo, usingefahamika au angalau usingetumika.

 

Mwanzoni inaweza kuonekana dhahiri kabisa kuwa wakati wote ushindani unahusisha utaratibu wa ugunduzi ambao huenda ukafaa kusisitizwa.  Huu unaposisitizwa kwa uwazi, hata hivyo, mahitimisho hupatikana mara moja ambayo hayako dhahiri sana.  La kwanza ni kwamba ushindani ni muhimu tu kwa sababu na kwa kiasi ambacho matokeo yake hayatabiriki na kwa ujumla ni tofauti na yale ambayo mtu yeyote angeweza kujitahidi kuyapata; na kwamba matokeo yake mazuri lazima yajidhihirishe kwa kupinga baadhi ya makusudio na kubatilisha baadhi ya matarajio.

 

Hitimisho la pili, linalohusiana kwa karibu na la kwanza, ni la kimethodolojia.  Lina mvuto wa pekee kiasi kwamba linahusisha sababu kuu kwa nini, katika miaka 20 au 30 ya uchumbuzi wa maelezo mazuri ya mfumo wa uchumi ambao pekee unaweza kutufundisha kuelewa dhima ya ushindani – umepoteza kwa kiasi kikubwa sifa yake, na hakika kama matokeo ya naelekea kutokueleweka kabisa na wale wanaojiita wanadharia wachumi.  Kwa sababu hii ningependa kuanza hapa kwa maneno machache kuhusu ukamilifu wa kimethodolojia wa kila nadharia ya ushindani ambayo inafanya mahitimisho yaliyotokana nayo kutiliwa shaka kwa wale wote ambao kwa kawaida huamua, kuhusu misingi ya kigezo kilichorahisishwa, ambacho wanajiandaa kukitambua kama cha kisayansi.

 

JARIDA LA KILA ROBO LA UCHUMI LA AUSTRALIA JUZUU LA 5, NA. 3 (SUMMER 2002)

Sababu pekee inayotufanya tutumie basi ushindani ina matokeo yake ya lazima kwa ukweli kwamba uhalali wa nadharia ya ushindani kamwe haiwezi kuthibitishwa kwa kutegemea nadharia kwa masuala yale ambayo ina raghba nayo.  Bila shaka inawezekana kuthibitisha nadharia kuhusu mifano ya kinadharia iliyowazwa kwanza; na kimsingi labda tungeweza labda kuthibitisha nadhari katika mazingira yaliyotengenezwa kibandia ambayo ukweli wote kwamba ushindani ni kugundua yangefahamika kwa mchunguzi mapema.  Katika hali hiyo, hata hivyo, matokeo ya jaribio yasingevutia sana, na yasingekuwa na thamani ya gharama ya kulifanya.  Hata hivyo, kama hatufahamu mapema kile tunachotaka kugundua kwa msaada wa ushindani, hatuwezi vilevile kuukilia namna ambavyo ushindani ungepelekea kwenye ugunduzi wa mazingira yote muhimu ambayo yangeweza kugunduliwa.  Yote haya yanayoweza kuthibitishwa bila kutegemea nadharia ni kwamba jamii zinazotumia ushindani kwa madhumuni haya zinatambua matokeo haya kwa kiasi kikubwa sana kuliko wengine – swala ambalo, ninaliona kama, historia ya ustaarabu inajibu waziwazi kwa kukubali.

 

Ukweli wa udadisi kuwa ustahilifu na ushindani hauwezi kuthibitishwa kwa kutegemea nadharia, hasa kwa masuala yenye maslahi yanayochangiwa pia na utaratibu wa ugunduzi wa sayansi kwa ujumla.  Faida ya taratibu za kisayansi zilizoanzishwa zenyewe haziwezi kuonyeshwa; zinatambuliwa tu kwa sababu kwa kweli zimetoa matokeo mazuri sana kuliko taratibu mbadala.¹

 

Tofauti baina ya ushindani wa kiuchumi na utaratibu unaofuatia wa kisayansi ni kwamba wa kwanza unaonyesha mbinu ya ugunduzi wa

____________________

¹  Tazama majadiliano ya kuvutia kuhusu matatizo haya kwenye M. Poyani, The Logic of Liberty (London, 1951), ambamo mwandishi anaelekezwa kutoka kwenye uchunguzi wa mbinu za utafiti wa kisayansi kwenda ushindani wa kiuchumi.  Tazama pia K.R. Popper, Logik der Forschung, zd. Ed. (Tübingen, 1966), uk 16.

 

mazingira mahsusi ya muda, wakati sayansi inatafuta kugundua kitu kinachojulikana mara nyingi kama “ukweli wa jumla”, yaani ukawaida katika matukio, unashughulika na upekee, hususan ukweli kwa kiasi kwamba unaelekea kukanusha au kuthibitisha nadharia zake.  Kwa kuwa hili ni suala la ugunduzi wa kisayansi una muda wa kutosha kuonyesha thamani yao, wakati umuhimu wa mazingira maalumu yaliyotolewa na ushindani na kiuchumi kwa kiasi kikubwa ni wa kupita.  Ingekuwa rahisi kupuuza sifa ya nadharia ya mbinu ya kisayansi katika kuzingatia kuwa haipelekei kwenye utabiri wa kuthibitika wa soko kwa kubaini kwamba haipelekei kutabiri kuhusu matokeo maalumu ya mchakato wa soko.  Hata hivyo, kulingana na hali ya mambo, nadharia ya soko haiwezi kutimiza haya katika mambo yote ambayo yanafaa kufanya ushindani.  Kama tutakavyoona, nguvu ya utabiri wa nadharia hii imezuiwa kwenye utabiri wa aina ya muundo au utaratibu wa kidhahania ambao utatokea; hata hivyo, haiendelezwi hadi kwenye utabiri wa tukio mahsusi².

 

II

Ingawa hii itanipeleka zaidi mbali na mada yangu kuu, napenda kuongeza maneno machache kuhusu matokeo ya kutoridhishwa na nadharia ya uchumi mkubwa kulikosababishwa na kutumia vigezo vya kimethodolojia vya uongo vya usayansi. Kwanza kabisa, kutokuridhishwa huku yawezekana ilikuwa ndiyo sababu kubwa ya idadi kubwa ya wachumi kukataa kupendelea kile kinachoitwa nadharia ya uchumi

 

 

___________________

2 Tazama insha yangu “The Theory of Complex Phenomena” kwenye The Critical Approach in Science and Philosophy, M. Bunge, ed. (London na New York, 1964).  Imechapwa upya katika My Studies in Philosophy, Politics, and Economics (Chicago na Uingereza, 1967).

 

mkubwa, ambao kwa kuwa inalenga kutabiri matukio thabiti, inaelekea kuhusiana vizuri zaidi na vigezo vya usayansi.  Hata hivyo, ukweli ni kwamba, kwangu inaelekea zaidi kidogo ya kisayansi – hakika, kwa maana halisi sana, haiwezi kufanya madai kwa jina la sayansi ya nadharia.

 

Msingi wa mtazamo huu ni kusadikisha kuwa mfumo wa uduni wa uchumi hauwezi kuonyesha taratibu ambao sio matokeo za mfumo mzuri, na kwamba mkusanyo huo au thamani ya wastani pekee vinavyoweza kuchukuliwa kitakwimu, havitupi taarifa yoyote kuhusu kinachoendelea katika miundo yetu mizuri.  Dhana kwamba lazima tuunde nadhari zetu ili ziweze  kutumika mara moja kwa idadi zinazochunguzika kitakwimu au idadi nyingine zinazopimika, ambalo ninaziona kama ni kosa la kimethodolojia ambalo, kama sayansi asilia, ingelilifuata, lingezuia maendeleo yake kwa kiasi kikubwa.  Tunachoweza kuhitaji kutokana na nadharia ni kwamba, baada ya kuingizwa kwa data muhimu, kutoka kwake yanaweza kupatikana mahitimisho ambayo yanaweza kukaguliwa dhidi ya uhalisia.  Ukweli kwamba data ni anuwai hizi na tata sana katika eneo letu la uchunguzi kwamba kamwe hatuwezi kuzizingatia zote ni ukweli usiobadilika, lakini sio kushindwa kwa nadharia.  Matokeo ya ukweli huu ni kwamba kutokana na nadharia zetu tunaweza kupata taarifa tu za jumla, au “utabiri wa ruwaza,” kama nilivyoziita mahali pengine³; hata hivyo, hatuwezi kuchukua utabiri wowote mahsusi wa matukio binafsi kutoka kwake.  Hakika, hata hivyo, hili halithibitishi kwa kusisitiza kuwa tunachukua uhusiano tata kati ya ubadilikaji unaoonekana mara moja, au kwamba hii ndiyo njia pekee ya kupata maarifa ya kisayansi – hususan sio kama tunafahamu hivyo, katika taswira hiyo isiyoeleweka vizuri ya ukweli tunaouita takwimu, katika mkusanyiko na wastani ambavyo hatutakwepa kutoa muhtasari wa vitu

_________________________

3  Tazama insha yangu iliyotajwa hapo juu, “The Theory of Complex Phenomena.”

 

vingi ambavyo maana yake isiyo rasmi ni anuwai.  Ni kanuni ya kiepistemolojia ya uongo kubadili nadharia kwa taarifa iliyopo, ili kwamba alama zinazowakilisha thamani zinazochunguzwa zionyeshwe moja kwa moja kwenye nadharia.

 

Alama zinazowakilisha thamani za kitakwimu kama vile pato la taifa, kitegauchumi, viwango vya bei, na uzalishaji ni alama zinazowakilisha thamani ambazo hazina dhima yoyote katika mchakato wa uamuzi wake.  Tunapaswa kuweza kubaini mabadiliko (“Sheria zisizotegemea nadharia katika maana maalumu ambayo Carl Menger alitofautisha na sheria za kinadharia) katika tabia iliyochunguzwa ya alama hizi zinazowakilisha thamani.  Mara nyingi mabadiliko haya yanatumika, lakini wakati mwingine hayatumiki.  Na bado kutumia njia za nadharia kubwa, hatutakaa tuweze kuweka masharti yanayotumika.

 

Hii isimaanishe kwamba nachukulia hiyo inayoitwa nadharia kubwa kuwa haina manufaa kabisa.  Kuhusu masharti mengi muhimu tuna taarifa tu za kitakwimu badala ya data zinazohusu mabadiliko katika mfumo mzuri.  Nadharia kubwa basi mara nyingi inamudu thamani zinazokaribia au, labda, utabiri ambao hatuwezi kuupata kwa njia nyingine yoyote.  Mara nyingine inaweza kufaa, kwa mfano, kutegemeza fikra zetu kwenye dhana kwamba kuongezeka kwa mahitaji ya mkusanyiko kutapelekea kwa ujumla ongezeko kubwa katika uwekezaji, ingawa tunafahamu kuwa katika mazingira fulani ni kinyume chake.  Uhakiki huu wa kimantiki wa nadharia kubwa una thamani kubwa kama kanuni zitokanazo na mazoea kwa ajili ya kuongeza utabiri kama hakuna taarifa za kutosha.  Bali sio tu kwamba sio za kisayansi zaidi kuliko nasharia ndogo; kwa maana halisi hawana kabisa sifa yoyote ya nadharia za kisayansi.

 

Kwa ajili hiyo lazima nikiri kwamba bado ninaisikitikia zaidi mitazamo ya Schumpeter mdogo kuliko ile ya mkubwa, ambao huu wa karibuni umehusika kwa kiasi kikubwa na kutokeza kwa nadharia kubwa.  Miaka 60 kamili iliyopita, kwenye chapisho lake adhimu la kwanza4, kurasa chache baada ya kutambulisha dhana ya nadharia ya “ubinafsi ya kimethodolojia” katika kuonyesha mbinu za nadharia ya kiuchumi, aliandika:

Kama mtu anasimamisha jengo la nadharia yetu ambalo halijaathiriwa na maoni na mahitaji ya nje, haiwezekani kukuta dhana hizi [zinazojulikana kama “pato la taifa”, “uajiri wa taifa”, “mtaji wa jamii”]  hivyo hatutahusika zaidi navyo.  Kama tungependa kufanya hivyo, hata hivyo, tungeona ni kwa ukubwa gani wamehuzunishwa na kutokueleweka na ugumu, na ni kwa ukaribu gani wanahusishwa na dhana nyingi potofu, bila ya kufanya nadharia maji ya ukweli yenye thamani.

 

III.

Sasa nikirejea kwenye mada yangu halisi baada ya kukuwasilishia shaka yangu kuhusu jambo hili, ningependa kuanza na maoni kwamba mara nyingi nadharia ya soko inazuia kupata uelewa halisi wa ushindani kwa kutoka kwenye dhana ya “idadi iliyotolewa” ya bidhaa adimu.  Bidhaa gani ni adimu, hata hivyo, ama vitu gani ni bidhaa, au ni duni au za thamani kiasi gani, hasa ni moja ya masharti kwamba ushindani unapaswa kugundua: katika kila suala ni matokeo ya awali ya mchakato wa soko ambao unataarifu watu mahali panapostahii utafiti.  Utumiaji wa maarifa yaliyosambazwa duniani kote katika jamii kwa mgawanyo wa

 

 

4 J. Schumpeter, Das Wesen und der Hauptinhalt der theoretischen Nationalökonomie Leipzig, 1908), uk. 97.

 

kazi uliotolewa hauwezi kuzingatia sharti kwamba watu wanafahamu matumizi yote halisi ambayo yanaweza kufanywa kwa vitu vilivyoko kwenye mazingira yao.  Mkazo wao utaelekezwa na bei zinazotolewa na soko kwa ajili ya bidhaa na huduma mbalimbali.  Maana yake ni kwamba, miongoni mwa mambo mengine, kwamba kila mchanganyiko maalumu binafsi wa stadi na  uwezo ambavyo kwa ajili hii wakati wote ni vya pekee – (na hata sio vya awali) havitakuwa tu ujuzi ambao mtu anayehusika ataeleza kwa kina au ripoti kwa wakala wa serikali.  Kisha, maarifa ninayozungumzia yanayojumuisha kwa kiasi kikubwa uwezo wa kubainisha masharti – uwezo ambao watu hao wanaweza kuutumia tu ipasavyo wakati soko linawaambia ni aina gani ya bidhaa na huduma zinazotakiwa, na kwa haraka kiasi gani.

 

Haya, pendekezo hili lazima litosheleze kufafanua aina ya maarifa ninayozungumzia ninapouita ushindani utaratibu wa ugunduzi.  Zaidi sana lingeongezwa kama ningependa kutengeneza muhtasari huu kwa uthabiti ili kwamba maana ya mchakato huu itokeze dhahiri.  Nilichosema, hata hivyo, kingetosha kuelezea upuuzi wa mkabala wa kawaida unaotokana na hali ambayo masharti yote ya lazima yanadhaniwa kufahamika – hali ambayo kiuchunguzi nadharia inaonyesha ushindani kamili, ingawa fursa kwa ajili ya shughuli tunazoziita ushindani haipo tena.  Hakika, inadhaniwa kuwa shughuli hiyo tayari imetekeleza jukumu lake, hata hivyo, lazima sasa nigeukie swala lingine ambalo bado lina mkanganyiko, ambalo ni maana ya dai kwamba soko hurekebisha lenyewe mipango ya watu kwa mambo yaliyogunduliwa; kwa maneno mengine, suala la madhumuni ya namna taarifa zilizogunduliwa zinavyotumika.

 

Mkanganyiko uliopo hapa unaweza kudhaniwa juu ya yote kuwa ni wazo la uongo kwamba utaratibu ambao soko linaleta unaweza kuonekana kama uchumi kwa maana halisi ya neno, kwamba matokeo kwa hiyo lazima yaamuliwe kulingana na vigezo ambavyo kwa ukweli vinafaa tu kwa uchumi huo binafsi.  Lakini hivi, vigezo ambavyo vinaandaa uchumi halisi ambamo juhudi zinaelekezwa katika kuwa na utaratibu unaolingana wa malengo, kwa kiasi fulani hauhusiki kabisa na mfumo changamani unaojumuisha aina nyingi za uchumi binafsi ambazo kwa bahati mbaya tulizitaja kwa neno hilohilo “uchumi”.  Uchumi katika maana thabiti ya neno ni mpango au mpangilio ambao mtu kwa ufahamu wake anautumia katika kuhudumia madhumuni ya mfumo wa mamlaka.  Mfumo wenyewe ulioletwa na soko ni kitu ambacho ni tofauti kabisa.  Lakini ukweli wa kwamba utaratibu huu wa soko kwa namna nyingine hauna tabia kama ya uchumi kwa maana halisi ya neno hususan, ukweli kwamba kwa ujumla hauhakikishi kuwa kila watu wengi wanachokiona kuwa ni muhimu zaidi wakati wote kinaridhishwa kabla ya yale yenye umuhimu mdogo – ni mojawapo ya sababu kubwa ambazo watu wanazikataa.  Inaweza kusemwa hakika, kuwa ujamaa wote hauna madhumuni mengine zaidi ya kugeuza halaksi (kama ninavyopenda kuuita utaratibu wa soko, kuepuka kutumia neno “uchumi”) katika uchumi halisi ambamo kipimo kinacholingana cha thamani kinaamua ni mahitaji gani yanakidhi na ni yapi hayakidhi.

 

Matakwa haya yanayochangiwa duniani kote yanaibua matatizo mawili.  Kwanza, kadri maamuzi ya uongozi ya uchumi wa kweli au utaratibu mwingine unavyohusika, ni maarifa tu ya waandaaji au mameneja peke yao yanayoweza kuwa na matokeo.  Pili, wanachama wote wa uchumi huo wa kweli – unaofikiriwa kuwa utaratibu unaosimamiwa kwa ufahamu – lazima utumikie mfumo wa mamlaka unaolingana wa malengo katika hatua zake zote.  Linganisha huu na faida mbili za utaratibu wenyewe wa soko au katalaksi:  Unaweza kutumia maarifa ya washiriki wote, na malengo unaoyatumikia ni malengo mahsusi kwa washiriki wake wote katika uanuwai na pande zake zote.

 

Ukweli kwamba katalaksi haitumikii mfumo unaolingana wa malengo ya kuibuka kwa matatizo yote ya kawaida yanayowasumbua sio tu wajamaa, lakini pia wachumi wote wanaojitahidi kutathmini utendaji wa mfumo wa soko.  Kwa kuwa kama mfumo wa soko hauhudumii utaratibu wa ngazi maalumu wa malengo, na kweli kama, utaratibu mwingine ulioanzishwa, hauwezi kusemwa kihalali kuwa una malengo dhahiri, wala kuweza kuwakilisha thamani ya matokeo yake kama kiasi cha nguvu binafsi.  Tuna maana gani, basi, tunapodai kuwa mfumo wa soko kwa namna fulani unazalisha kiasi kikubwa sana au cha juu sana?

 

Pa kuanzia swali lazima kuwe na utambuzi kuwa, ingawa utaratibu wenyewe haukuanzishwa kwa ajili ya lengo binafsi maalumu, na kwa ajili hiyo hauwezi kusemwa kuwa unahudumia lengo thabiti maalumu, hata hivyo unaweza kuchangio kutambua idadi ya malengo binafsi ambayo hakuna anayeyafahamu kwa ujumla wake.  Utekelezaji wa uwiano wenye mafanikio unaofanywa na mtu unawezekana tu katika dunia ambayo kwa kiasi fulani ina mpangili mzuri, ambayo mtu yeyote aliyechaguliwa kwa kubahatisha ana matarajio ya kutekeleza malengo yake kwa ufanisi iwezekanavyo, hata kama hatuwezi kutabiri ni watu gani mahsusi watakaonufaika na ambao hawatanufaika.  Kama tulivyoona, matokeo ya utaratibu wa ugunduzi hayatabiriki, na tunachoweza tu kutarajia kwa kutumia utaratibu unaofaa wa ugunduzi ni kwamba utaongeza matazamio ya watu wasioanishwa, lakini sio matazamio ya matokeo yoyote maalumu kwa ajili ya watu maalumu.  Lengo pekee la pamoja tunaloweza kufuatilia katika kuchagua mbinu hii kwa ajili ya kufuata uhalisia wa jamii ni mfumo au utaratibu wa kidhahania ambao utaundwa kama matokeo.

 

 

 

IV.

Tumezoea kuuita utaratibu ulioletwa na ushindani, ulinganifu – neno lisilo la ufasaha sana, kwa kuwa ulinganifu wa kweli unamaanisha kwamba maelezo husika yamekwisha kugunduliwa na kwamba mchakato wa ushindani umekwisha.  Dhana ya utaratibu, ambayo ndiyo ninayopendelea zaidi ya ulinganifu, angalau katika majadiliano kuhusu ukweli kwamba utaratibu unaoweza kutekelezwa kwa kiwango kikubwa au kidogo sana, na kwamba utaratibu unaweza vilevile kuhifadhiwa kulingana na vitu vinavyobadilika.  Wakati ulinganifu haujawahi kuwapo kamwe, hata hivyo mtu anaweza kudai kwa kuthibitisha kuwa aina ya utaratibu ambao “ulinganifu” wa nadharia unawakilisha aina ya mawazo unatekelezwa kwa kiasi kikubwa.

 

Utaratibu huu unajidhihirisha wenyewe kwanza kabisa kwa ukweli kwamba matazamio ya miamala maalumu na watu wengine, ambayo yanazingatiwa na mipango ya washiriki wote wa uchumi, kwa kiasi fulani yanatekelezwa.  Marekebisho haya ya pamoja ya mipango binafsi yanaletwa na mchakato tuliojifunza kuuita mwitiko hasi tangu sayansi asilia – zilipoanza kujishughulisha na taratibu za papo kwa hapo au mifumo inayojiongoza yenyewe.”  Kwa hakika, hata wanabiolojia wanaojua sana sasa wanafahamu,

 

Zamani kabla ya Claude Bernard, Clark Maxwell, Walter B. Cannon au Norbert Wiener kuanzisha Saibenetiki, Adam Smith alielewa wazo hilo kama lilivyo kwenye kitabu chake Wealth of Nations.  “Mkono usioonekana” ambao unarekebisha bei ulielekea kuelezea wazo hilo.  Smith anasema kimsingi kwamba katika soko huria, bei zinaamuliwa na mwitiko hasi5.

 

_________________________

5  G. Hardin, Nature and Man’s Fate (New York na Uingereza), Mentor Edition, 1961, uk. 54.

 

 

Ni wazi kupitia kutokuridhishwa na matarajio kwamba kiwango cha juu cha makubaliano ya matarajio kinaletwa.  Ukweli huu, kama tutakavyoona baadaye, una umuhimu mkubwa katika kuelewa utendaji wa mfumo wa soko.  Lakini mafanikio ya soko hayatumiwi katika kuleta marekebisho ya pamoja ya mipango binafsi.  Unaonyesha pia kwamba kila bidhaa inazalishwa na wale ambao wanaweza kuizalisha zaidi kwa gharama ndogo (au angalau rahisi) kuliko yeyote ambaye kwa ukweli haizalishi, na kwamba bidhaa zinauzwa kwa bei ambayo ni ya chini sana kuliko zile ambazo mtu yeyote angeweza kumpa bidhaa yule ambaye hazitoi.  Bila shaka hii haiwazuii watu wengine kupata faida kubwa zaidi ya gharama zao, mradi gharama hizi zinaonekana za chini sana kuliko zile za mzalishaji mwingine bora wa bidhaa.  Maana yake, hata hivyo, ni kwamba mchanganyiko wa bidhaa tofauti ambazo ukweli ni kwamba zinazalishwa, kiasi kinachozalishwa kama kinachoweza kutengenezwa kwa mbinu yoyote tunayoifahamu.  Na hicho bila shaka sio kama ambacho tungezalisha kama kwa ukweli kama maarifa yote aliyonayo mtu au ambayo angepata yangepatikana katika kituo cha kati na kutoka

hapo yaingizwe kwenye kompyuta.  Gharama ya utaratibu wa ugunduzi ambayo tunatumia inastahili.  Lakini sio haki kuamua ufanisi wa soko kwa namna fulani “kutoka chini juu”, zinazotajwa kwa kulinganisha na kiwango cha wazo kwamba hatuwezi kufikia kwa namna yoyote inayofahamika.  Kama tunaamua ufanisi wa soko “kutoka juu chini” (ambayo inaonekana kwamba ndiyo njia inayokubalika), k.v. kwa kulinganisha na tunachoweza kufikia kwa njia ya mbinu nyingine yoyote tuliyonayo, hususan kwa kulinganisha na ambacho kingezalishwa kama ushindani ungezuiwa – kwa mfano, kama bidhaa ingezalishwa na wale tu walioruhusiwa na mamlaka kufanya hivyo – ufanisi wa soko lazima uamuliwe kama unaofaa sana.  Tunahitaji tu kukumbuka jinsi gani ilivyo vigumu kwenye uchumi wenye ushindani mkubwa kugundua njia za kuwapa watumiaji bidhaa bora au za bei nafuu kuliko ilivyo sasa.  Kama, kwa muda, tunaamini tumegundua fursa hizo zisizotekelezwa, tunaona kwa ujumla kuwa mamlaka ya serikali au zoezi lisilofaa la utawala binafsi mpaka sasa vimezuia unyonyaji wao.

 

Bila shaka, tusisahau pia kwamba soko halitoi zaidi ya makadirio ya kiwango chochote kuhusu sehemu ya ukubwa – ambayo nadharia halisi inaelezea uwezekano unaoweza kufikiwa katika uzalishaji wa mchanganyiko wowote wa bidhaa na huduma; lakini soko linaruhusu mchanganyiko mahsusi wa bidhaa mbalimbali na usambazaji wake miongoni mwa watu uamuliwe kimsingi na mazingira yasiyotabirika na kwa ajili hii yaamuliwe na bahati.  Kama Adam Smith alivyotambua6, hali ni kama vile kukubali kucheza mchezo unaozingatia ustadi kwa sehemu na bahati kwa sehemu.  Sheria za mchezo zinahakikisha kuwa kwa bei kama vile kila hisa ya mtu inategemea takriban bahati, ulinganifu halisi wa hisa ya kila mtu, kutegemea kwa sehemu bahati, kunakuwa dhahiri.  Kwa msamiati wa kisasa tunaweza kusema kwamba tunacheza mchezo wa hesabu isiyo na sifuri ambao sheria zake zina lengo la kuongeza muda wa kumaliza deni lakini kuacha kwa sehemu hisa ya watu kwa bahati.  Mtu aliyejaliwa kuwa na taarifa kamili bila shaka angechagua kila hatua ya sehemu ya ukubwa –  ambayo angeitaka na kisha kusambaza kwa atakavyoona inafaa bidhaa   ya mchanganyiko anaochagua.  Lakini hatua pekee kuhusu (au angalau mahali karibu) sehemu tunayoweza kuifikia kwa kutumia utaratibu tunaoufahamu ndiyo tunayofikia tunapoliachia soko uamuzi.  Kile tunachoita “kiwango cha juu” tunachofikia kwa namna hii hakiwezi kuelezewa kama hesabu ya idadi fulani ya bidhaa, bali tu kwa fursa kinachowapa watu wasioainishwa kupata hisa kubwa iwezekanavyo inavyoamuliwa kwa sehemu kubwa na bahati.

 

_________________________

6  Tazama A. Smith, Theorie der athischen Gefühle, W. Eckstein, trans. (Leipzig, 1926) Vol. 2, Uk. 396,467.

 

 

Ukweli kwamba matokeo haya hayawezi kutathminiwa kwa kuzingatia ngazi ya thamani inayolingana ya malengo thabiti yanayotakiwa ni mojawapo ya sababu kuu zinazoelekea kunipotosha katika kuamua matokeo ya utaratibu wa soko au katalaksi kama vile ulikuwa na uhusiano wowote na uchumi katika maana halisi.

 

V.

Matokeo ya tafsiri hii isiyo sahihi ya mfumo wa soko kama uchumi ambao jukumu lake ni kukidhi mahitaji mbalimbali kulingana na utaratibu wa daraja lililotolewa yanaakisiwa kwenye jitihada za kisiasa za kurekebishia bei na mapato katika huduma ya ile inayoitwa “haki katika jamii”.  Hata hivyo, maana mbalimbali ambazo wanafalsafa wa jamii walijitahidi kuingiza dhana hii, kiutendaji ni moja tu: kulinda baadhi ya makundi ya watu wasishuke kutoka kwenye mtindo wa maisha kamili au husianifu ambao walifurahia hapo awali.  Hata hivyo, kanuni hii haiwezi kutekelezwa kwa ujumla bila ya kuharibu misingi ya mfumo wa soko.  Sio tu ukuaji unaoendelea, bali katika mazingira fulani hata kuhifadhi kiwango cha mapato ya wastani kilichofikiwa kunategemea michakato ya marekebisho ambayo yanahitaji mabadiliko sio tu ya hisa husianifu bali pia hisa kamili za watu na makundi binafsi, ingawaje watu na makundi hayo hayawajibiki na umuhimu wa mabadiliko hayo.

 

Katika hatua hii ni muhimu kukumbuka kwamba maamuzi yote ya kiuchumi yanafanywa kuwa muhimu na mabadiliko yasiyotarajiwa, na kwamba uhalali wa kutumia utaratibu wa bei ni kwa kuwa tu unawaonyesha watu kwamba walichokifaya hapo awali au wanachoweza kufanya sasa kimekuwa kwa kiasi fulani muhimu, kwa sababu ambazo – hawana shughuli nazo.  Mabadiliko ya mfumo wa jumla wa amali za binadamu katika mazingira yanayobadilika msingi wake ni ukweli kwamba fidia ya huduma mbalimbali hubadilika bila ya kuzingatia faida au kasoro za wale wanaohusika.

 

Katika uhusiano huu mara nyingi neno “vivutio” linatumika kwa namna ambayo inalifanya lisieleweke kwa urahisi, kama vile madhumuni yake makuu yalikuwa kushawishi watu kufanya jitihada za kutosha.  Kazi muhimu sana ya bei, hata hivyo, ni kwamba zinatuambia tunachopaswa kufanikisha, sio kiasi gani.  Katika dunia inayoendelea, kubadilika siku zote, hugharimia tu kiwango cha ustawi unaohitaji marekebisho ya mara kwa mara kwa namna jitihada za watu wengi zinavyoelekezwa; na haya yatatokea tu wakati fidia wianifu ya shughuli hizi inapobadilika.  Chini ya masharti yasiyobadilika, hata hivyo, marekebisho haya – yanayohitajika kwa ajili tu ya kuendeleza mtiririko wa mapato katika ngazi yake ya awali – hayatazalisha ziada ambayo itatumika kufidia wale ambao wanaathiriwa na mabadiliko ya bei.  Ni katika uchumi unaokuwa haraka tu ndipo tunaweza kutumaini kuzuia kushika kabisa kwa kiwango cha vitu cha makundi maalum.

 

Hivi leo, ushughulikiaji uliozoeleka wa matatizo haya mara kwa mara umeshindwa kuona ukweli wa kwamba hata uthibiti husianifu wa mikusanyiko mbalimbali inayoshughulikiwa na uchumi mkubwa kwa kuwa data ni matokeo ya michakato ya uchumi mkubwa ambamo mabadiliko ya bei husianifu yana dhima ya kuamua.  Ni matokeo ya utaratibu wa soko ambao mtu anashawishiwa kujaza pengo linalotokea wakati mtu mwingine hakidhi matarajio kwa kuzingatia mipango iliyofanywa na mtu wa tatu.  Kwa ajili hii usambazaji wote wa pamoja na maeneo ya mahitaji (demand curves) tunayofurahia wakati wa kutumia sio dara halisi, bali ni matokeo ya mchakato unaoendelea wa ushindani.  Hivyo, taarifa za kitakwimu haziwezi kutufunulia kamwe ni mabadiliko gani ya bei au mapato yatakayohitajika kuleta marekebisho muhimu kwenye mabadiliko ya data yasiyoepukika.

 

Hata hivyo, kipengele kinachoamua, ni kwamba kwenye jamii ya kidemokrasia itakuwa haiwezekani kabisa, kutumia amri ambazo zingeweza kuonekana kuwa haki, katika kuleta mabadiliko hayo ambayo bila shaka ni ya lazima, bali ulazima ambao usingeweza kuonyeshwa hasahasa katika suala mahususi.  Katika mfumo kama huo, mwelekeo wa makusudi wa uchumi wakati wote ungelenga katika bei zinazoonekana kuwa zinaridhisha, na kwa mazoea ambazo zinaweza kumaanisha kuhifadhi bei zilizopo na mfumo wa mapato.  Mfumo wa uchumi ambamo kila mtu alipata ambacho wengine walihisi kwamba alistahili usingesaidia bali kuwa mfumo usio na ufanisi, mbali na ukweli kwamba ungeweza pia kuwa udhalimu usiozuilika.  Kwa sababu hiyohiyo, inaogofya vilevile kuwa “sera ya mapato” yoyote ingeelekea zaidi kuzuia kuliko kuwezesha marekebisho hayo katika mfumo wa bei na mapato yanayohitajiwa na mabadiliko kwa mabadiliko yasiyotarajiwa katika masharti.

 

Ni mojawapo ya kweli kinza za zama zetu kwamba nchi za kikomunisti, kwa ajili hiyo, yawezekana hazina mzigo mkubwa wa mawazo ya “haki katika jamii” kuliko ilivyo kwa nchi za “kibepari” na kidemokrasia, na hivyo kuelekea zaidi kuruhusu wale walioathiriwa na maendeleo kuteseka.  Katika angalau baadhi ya nchi za Magharibi hali haina matumaini kama ilivyo kwa sababu itikadi inayoamua sera inayafanya mabadiliko kutokuwezekana ambayo yangekuwa muhimu kwa ajili ya kuboresha hali ya tabaka la wafanyakazi haraka kiasi cha kutosha kuifanya itikadi hiyo itoweke.

 

VI.

Hata katika uchumi uliokua sana ushindani ni muhimu kimsingi kama mfumo wa ugunduzi ambapo wajasiriamali mara kwa mara hutafuta fursa ambazo hazijatumiwa ambazo zinaweza  vilevile kutumiwa kwa manufaa ya wengine, na hii ni kweli bila shaka kwa kiasi kikubwa kwa kuziangalia jamii zinazoendelea.  Kwa makusudi nilianza kwa kuzingatia matatizo ya kudumisha mfumo katika jamii ambamo mbinu nyingi na kazi za uzalishaji zinafahamika kwa ujumla, bali pia mfumo ambao unahitaji marekebisho ya kuendelea ya shughuli kwa mabadiliko madogomadogo yasiyoepukika kwa ajili ya kuendeleza kiwango cha awali kilichofikiwa.  Katika hatua hii sitaki kuuliza dhima iliyoonyeshwa kwenye ushindani katika uendelezaji wa teknolojia iliyopo.  Ningependa hata hivyo, kusisitiza kuwa kwa umuhimu wowote utakavyokuwa ushindani lazima uwe popote lengo la kwanza lilipo iligundua uwezekano ambao bado haufahamiki katika jamii ambako ushindani ulikuwa mdogo wakati kwa sehemu kubwa uongo, unaweza usiwe upuuzi kabisa kutegemea kwamba tunaweza kutabiri na kudhibiti maendeleo na mfumo wa jamii ambao tayari umeendelezwa kwa kiasi kikubwa.  Lakini inaelekea kutokuamini kushikilia kwamba tunaweza kuamua mapema mfumo wa jamii wa hapo baadaye ambamo tatizo kubwa bado ni kutafuta ni aina gani ya vifaa na nguvu za uzalishaji za binadamu zilizopo, au kwamba tunapaswa kuwa katika nafasi, kwenye nchi kama hiyo, kutabiri matokeo maalumu ya kipimo kilichotolewa.

 

Licha ya ukweli kwamba bado kuna mambo ya kugundua katika nchi kama hiyo, ninaona kwamba kuna kitu kingine cha kuzingatia katika kuufanya uhuru mkubwa zaidi wa ushindani kuwa muhimu zaidi hapa kuliko katika nchi zilizoendelea sana.  Ukweli wa kukumbuka ni kwamba mabadiliko ya lazima katika tabia na mila yatatokea tu pale ambapo wale walioko tayari na kuweza kufanya majaribio ya taratibu mpya wanaweza kufanya iwe lazima kwa wengine kuwaiga, wakati wa awali wa kuoinyesha njia; lakini kama walio wengi wako katika nafasi ya kuwazuia wachache wasifanye majaribio, mfumo wa ugunduzi wa lazima utadhoofishwa.  Ukweli kwamba ushindani sio tu unaonyesha namna mambo yanavyoweza kuboreshwa, bali pia huwalazimisha wale wote ambao kipato chao kinategemea soko kuigiza maboresho, bila shaka ni moja ya sababu kubwa ya kutokuwa na ari ya kushindana.  Ushindani unawakilisha aina fulani ya udhibiti ambao utasababisha watu wengi kubadilisha mwenendo wao kwa namna ambayo isingeletwa na aina yoyote ya maelekezo au amri.  Mipango mikuu katika huduma ya “haki katika jamii” inaweza kuwa ya kifahari ambayo nchi tajiri zinaweza kumudu, lakini ni hakika hakuna mbinu kwa ajili ya nchi maskini za kuleta marekebisho katika mazingira yanayobadilika haraka zinazotegemewa katika ukuaji.

 

Aidha, katika uhusiano huu ingefaa kutaja kwamba jinsi fursa zilizopo za nchi zinavyozidi kubakia bila kutumiwa, ndivyo fursa za ukuaji zinakuwa kubwa sana; mara nyingi hii ina maana kiwango kikubwa cha ukuaji ni alama ya sera mbovu hapo siku za nyuma kuliko sera nzuri za hivi sasa.  Vilevile, inaelekea kwamba kwa ujumla mtu hawezi kutegemea nchi ambayo tayari iko mbali kimaendeleo kuwa na kiwango kikubwa cha ukuaji kama nchi ambayo utumiaji wake kamili wa raslimali zake umezuiwa na vikwazo vya kisheria na kiasasi.

 

Baada ya kuona niliyonayo kuhusu dunia, ninaona kwamba uwiano wa watu ambao wako tayari kujaribu uwezekano mpya ambao unaleta matumaini ya kuboresha hali zao – mradi wengine hawawazuii kufanya hivyo – hii karibu ni sawa kila mahali.  Ninaona kwamba ukosefu uliolalamikiwa sana wa ari ya ujasiriamali katika nchi nyingi changa sio tabia isiyobadilika ya watu, bali ni matokeo ya mipaka iliyowekwa juu ya watu na mtazamo uliopo.  Ndiyo sababu hii hasa, athari zinakuwa mbaya, katika nchi hizo, utashi wa pamoja wa wengi ulikuwa ni dhabiti juhudi za watu, licha ya hayo nguvu ya umma inajiwekea yenyewe mpaka wa kumlinda mtu dhidi ya shinikizo la jamii – na ni asasi ya milki binafsi tu, na asasi zote zenye kupenda mabadiliko za utawala wa sheria zinazohusiana, ndizo huweza kuleta hizi za sasa.

 

Ingawa kwa kiasi kikubwa ushindani ni kielelezo cha uthabiti kuhusiana na makampuni binafsi – mmoja ambao unajitokeza tena ni kwa namna isiyotegemewa baada ya jitihada za kuzuia – manufaa yake kuhusiana na kipengele kimoja cha uzalishaji kinachoonekana kila mahali , kinachoitwa kazi za binadamu, kimefanywa karibu kukosa ufanisi katika Nchi zote za Magharibi.  Ni ukweli unaofahamika kote kuwa matatizo makubwa zaidi na hakika yanayoonekana magumu kuyatatua ya sera ya uchumi ya hivi leo, yanayowashughulisha wachumi zaidi kuliko matatizo mengine yote, ni matokeo ya kile kinachoitwa kutokubadilika kwa mishahara.  Maana yake kimsingi ni kwamba muundo wa mishahara pamoja na ngazi ya mishahara vimekuwa vikiendelea mbali na masharti ya soko.  Wachumi wengi wanaiona hii hali kama maendeleo yasiyobadilika ambayo hatuwezi kuyabadilisha na ambayo kwake ni lazima tubadilishe sera zetu.  Sio kutia chumvi kusema kwamba kwa miaka 30 iliyopita, majadiliano kuhusu sera ya fedha hususan yameshughulikia karibu matatizo tu ya kuepuka ugumu uliosababishwa na mishahara isiyobadilika.  Kwa muda mrefu nimekuwa na fikra kuwa hii imekuwa kutibu tu dalili.  Kwa sasa hivi, tunatakiwa kushughulikia matatizo ya msingi, lakini hii sio tu kuiahirisha muda ambao tunapaswa kukabiliana moja kwa moja na tatizo la kwanza, bali pia ni kuufanya ufumbuzi wa lililotangulia kuongezeka ugumu.  Hii ni kwa sababu kuukubali ugumu huu kama ukweli usiozuilika sio tu matokeo katika kuyaongeza, lakini pia yanaonyesha hali inayoashiria wema au ubaya wa uhalali katika mifumo inayopingana na jamii na yenye uharibifu.  Lazima nikiri kwamba matokeo yake mimi mwenyewe nimepoteza kabisa raghaba na majadiliano yanayoendelea ya sera ya fedha, ambayo hapo mwanzo ilikuwa mojawapo ya maeneo yangu ya utafiti, kwa sababu uepukaji huu wa suala kuu ninaona ni kuwabebesha mzigo warithi wetu kwa namna ya kutokuwajibika.  Kwa namna fulani, bila shaka, tunavuna hapa yale tu mwanzilishi wa mtindo huu aliyopanda, kwani kwa kawaida tuko tayari ndani “hatimaye” ambamo alijua angekuwa amefariki.

 

Ilikuwa bahati mbaya kwa dunia kwamba nadharia hizi zimetokana na hali isiyokuwa ya kawaida na, hakika, labda ya pekee ya Uingereza miaka ya 1920 – hali ambayo ilionyesha wazi kuwa ukosefu wa ajira ulikuwa ni matokeo ya kiwango cha juu mno cha mshahara halisi, na kwa tatizo la kutokubadilika kwa muundo wa mishahara lina umuhimu mdogo.  Kama matokeo ya kurejea kwa Uingereza kupanda kwa gharama za maisha wakati wa vita katika mlingano wa 1914, ingeweza, kudaiwa pamoja na uthibitisho kwamba mishahara yote halisi katika nchi hiyo ilikiuwa juu sana kulinganisha na sehemu nyingine duniani kufikia wingi unaohitajika wa bidhaa za kusafirisha nje.  Sishawishiki kuwa hii ilikuwa kweli tupu hata hivyo.  Hata katika wakati huo, kwa uhakika, Uingereza ilikuwa na chama cha wafanyakazi cha zamani zaidi, kilichokuwa na mizizi ya kina na kilichojumuisha wote, ambacho kupitia sera yake ya mishahara kimefanikiwa kudumisha muundo wa mishahara ambao uliamuliwa zaidi kwa mazingatio ya “haki” kuliko uchumi unaofaa.  Maana yake ni kwamba uhusiano unaoheshimiwa kutokana na ukale wake baina ya mishahara tofauti ulidumishwa, na kwamba mabadiliko yoyote kama hayo katika mishahara hiyo ya makundi mbalimbali kama yalivyotakiwa na mazingira yaliyobadilishwa yakawa hayawezekani kabisa.  Mambo yaliposimama basi, ajira kamili ingeweza kupatikana bila shaka kwa kuleta mishahara kamili – yawezekana ile ya makundi mengi ya wafanyakazi – duni kutoka kwenye kiwango walichofikia kama matokeo ya upunguzaji jumla ya fedha zitumiwazo ili kudhibiti bei.  Hata hivyo, sio hakika kwamba hii ingemaanisha kushuka kwa kiwango cha wastani cha mishahara halisi.  Labda marekebisho ya muundo wa uchumi kamili yaliyoletwa na mabadiliko ya mishahara yangefanya haya kutokuwa ya lazima.  Katika tukio lolote, msisitizo kuhusu kiwango cha wastani cha mshahara halisi wa wafanyakazi wote wa nchi walionyimwa uwezekano huu wa hata kutiliwa maanani.

 

Labda itaonekana inafaa kulichukulia tatizo hili kwa mtazamo mpana zaidi.  Kwangu mimi ninaona kuwa haiwezekani kutia shaka kuwa tija ya kazi ya nchi, na hivyo basi kiwango cha mshahara ambacho mshahara kamili unawezekana, hutegemea mgawanyo wa wafanyakazi katika matawi mbalimbali ya tasnia, na kwamba mgawanyo kwa upande mwingine unaamuliwa na muundo wa mshahara. Lakini kama muundo huu wa mishahara umekuwa mgumu zaidi kubadilika, hali hii itazuia au kuchelewesha marekebisho ya uchumi kwa mazingira yaliyobadilishwa.  Hivyo ichukuliwe kuwa, katika nchi ambayo uhusiano baina ya mishahara mbalimbali umewekwa thabiti kwa muda mrefu, kiwango halisi cha mshahara cha kufikia ajira kamili kitaonekana cha chini ya vile ambavyo kingekuwa kama mishahara ingebadilikabadilika kiurahisi.

 

Kwangu mimi ninaona muundo usiobadilika kabisa wa mishahara ungezuia marekebisho kwa mabadiliko katika masharti mengine, hususan bila ya maendeleo ya kiteknolojia tuliyozoea hivi leo.  Hili pia linahusu hasa marekebisho ya mabadiliko hayo ambayo lazima yatokee hasa ili kuweka thabiti kiwango cha mapato.  Muundo wa mishahara usiobadilika kabisa unastahili kuelekeza kwenye kushuka kwa polepole kwa kiwango cha mishahara halisi ambacho ajira kamili huweza kufanywa.  Kwa bahati mbaya siufahamu uchunguzi wowote wa majaribio wa uhusiano baina ya kubadilika kwa urahisi na kuongezeka kwa mishahara.  Ningetegemea uchunguzi huo kufichua uhusiano mzuri baina ya mabadiliko haya mawili – sio sana kwa sababu ukuaji unapelekea kwenye mabadiliko katika mishahara husika, bali juu ya yote kwa sababu mabadiliko hayo ni masharti ya mwanzo ya lazima kwa ajili ya marekebisho hayo kwa masharti yaliyobadilishwa yanayohitajika katika ukuaji.

 

Lakini jambo muhimu, ninaamini, ni kwamba kama ni sahihi kwamba kiwango cha mshahara halisi ambacho kinawezekana kutokana na ajira kamili hutegemea muundo wa mishahara, na kama uwiano kati ya mishahara mbalimbali utabakia bila kubalika kama masharti yanavyobadika, basi kiwango halisi cha mshahara kinachotokana na kuwepo kwa ajira kamili ama kitaendelea kushuka au hakitapanda haraka kama ambavyo vinginevyo kingewezekana.  Hii ina maana kwamba kushawishi kiwango cha mshahara halisi kunakofanywa na sera ya fedha hakuleti njia yoyote ya kusaidia kutoka kwenye matatizo yaliyosababishwa na kutokubadilika kwa muundo wa mishahara.  Wala njia haiwezi kuletwa na “sera yoyote ya mapato” inayowezekana.  Badala yake, jinsi mambo yanavyogeuka, ni kutokubadilika hasa kwa muundo wa mishahara kulikoletwa na sera ya mishahara ya vyama vya wafanyakazi kwa maslahi yaliyopendekezwa ya wafanyakazi wao (au dhana yoyote ya “haki katika jamii”) ambayo imekuwa moja ya vipingamizi vikubwa katika kuongezeka kwa mapato halisi ya wafanyakazi kwa ujumla; kwa maneno mengine, kama mishahara ya wafanyakazi kwa ujumla hakitapanda haraka kama ambavyo vinginevyo kingewezekana.

 

Wazo bora kabisa ambalo John Sturt Mill alilielezea katika tawasifu yake kama “ajira kamili kwa mishahara mikubwa kwa wafanyakazi wote kwa ujumla” linaweza kutekelezwa tu kwa kutumia kazi kiuchumi ambao badala yake hupendekeza mishahara inayobadilikabadilika kiurahisi.  Mahali pa wazo hili, mtu mashuhuri ambaye jina lake yumkini litaingizwa kwenye historia kama mchimba kaburi wa uchumi wa Uingereza ameeneza kushuka kwa kiwango cha mshahara halisi kupitia kushuka kwa thamani ya fedha kama mbinu ya kufikia ajira kamili wakati akitambua kutokubadilika kwa muundo wa mishahara midogo.  Kwa maoni yangu, hata hivyo, uzoefu wa miaka ya hivi karibuni unaonyesha wazi kuwa mbinu hii inatoa nafuu ya muda tu.  Ninaamini hatupaswi kuchelewa tena kukishambulia chanzo cha tatizo.  Hatutaendelea zaidi kuyafumba macho yetu katika ukweli kwamba maslahi ya kazi kwa ujumla yanahitaji kwamba nguvu ya vyama binafsi vya wafanyakazi kudumisha msimamo wianifu wa wanachama wao dhidi ya wafanyakazi wengine iondolewe.  Jukumu muhimu sana sasa hivi linaonyesha kushawishi kazi kwa ujumla kwamba kuondoa ulinzi wa msimamo wianifu wa makundi binafsi hakutahatarisha tu matarajio ya ongezeko la haraka katika mshahara halisi wa kazi kwa ujumla, bali ukweli ni kwamba kunaongeza matarajio.

 

Kwa hakika, hapa sitajadili kwamba kwa kipindi cha karibuni, ambacho matokeo yake yanatabirika bado kisiasa itabakia kutokuwezekana kurejesha soko huria la kazi halisi.  Jaribio lolote lingepelekea kwenye migogoro mikubwa sana kiasi kwamba lisingeweza kuzingatiwa kwa makini – angalau mradi waajiri hawatoi uhakikisho wa pamoja wa kudumisha kipato halisi cha wastani cha wafanyakazi wao.  Lakini uhakikisho huo hasa, ninaamini, ndiyo njia pekee ya kurejesha soko kwenye kazi yake ya kuamua mishahara wianifu ya makundi mbalimbali.  Ni kwa njia hii, ninavyoona mimi, tungeweza kutumaini kushawishi makundi binafsi ya wafanyakazi kuacha dhamana ya viwango vya mishahara yao mahususi, ambayo imekuwa kikwazo kikubwa kwa muundo wa mishahara unaoweza kubadilika kwa urahisi.  Makubaliano hayo ya pamoja baina ya waajiri kwa ujumla na wafanyakazi kwa ujumla mimi ninaona ni hatua ya mpito inayohitaji kuzingatiwa kwa makini, kwa sababu matokeo yangeweza pengine kuwaonyesha wafanyakazi ni kiasi gani wangeweza kunufaika kutokana na soko la kazi linalofanyakazi kikamilifu.  Badala yake lingeleta matarajio na hatimaye kukiondosha chombo chenye usumbufu na kisichoeleweka ambacho kingeundwa hapo mwanzo.

 

Nilichonacho akilini ni mkataba wa jumla ambao  utawaahidi wafanyakazi kwa ujumla, mwanzoni mwa mwaka, jumla ya mishahara yao halisi ya awali pamoja na hisa ya faida iliyoongezeka.  Kila kundi binafsi au mfanyakazi binafsi, hata hivyo, angepokea kwenye hundi yake ya malipo ya kila mwezi sehemu fulani tu, tuseme tano ya sita ya mshahara wake wa awali.  Kiasi kilichobakia (pamoja na hisa iliyokubaliwa ya jumla ya faida iliyoongezeka ya shughuli zote)  kingegawanywa katika malipo ya miezi miwili ya nyongeza – mwishoni mwa mwaka na baada ya vitabu kufungwa – kwa wafanyakazi wa mashirika na matawi mbalimbali ya uchumi, kwa uwiano katika mabadiliko katika faida inayotokana na msingi wa tano ya sita ya mishahara iliyogawanywa.  Nimependekeza tano ya sita kama sehemu ya malipo yanayoendelea, kwani hii ingewezesha malipo ya bonasi ya Krismasi kwa kiwango cha wastani cha mapato ya mwezi kwa msingi wa makisio ya awali ya faida, na ya bonasi ya pili ya likizo ya karibu kiwango hichohicho wakati vitabu vinapofungwa kwa ajili ya mwaka wa fedha.  Kwa ajili ya mwaka utakaofuatia mishahara ya wastani ya mwaka wa kwanza ingethibitishwa tena, lakini hadi mwishoni mwa mwaka kila kundi lingelipwa tano ya sita tu ya jumla ya kiasi kilicholipwa mwaka uliotangulia, pamoja na ziada mwishoni mwa mwaka kwa kila kundi kwa kuzingatia faida zilizopatikana katika kiwanda au shirika husuika, na kadhalika.

 

Kwa namna fulani, utaratibu kama huu ungeweza kuwa na athari sawa na urejeshaji wa soko huria la kazi, isipokuwa kwamba kazi ingejua kwamba mishahara yake halisi ya wastani isingeshuka, bali kuongezeka tu.  Ningetegemea kuwa kuanzishwa tena huko kusiko kwa moja kwa moja kwa mfumo wa soko kwa ajili ya kuamua mgawanyo wa wafanyakazi miongoni mwa viwanda na mashirika ungeleta mchapuko wa ongezeko katika mishahara halisi ya makundi binafsi.

 

Utaniamini nikisema kwamba sifanyi pendekezo lisilo la kawaida kwa wepesi tu.  Bali hatua kama hii, ninaamini, ndiyo njia pekee iliyobakia ya kutoka kwenye kutokubadilika kunakoongezeka kwa muundo wa mishahara.  Kutokubadilika nionavyo mimi sio tu chanzo kikubwa cha matatizo ya kiuchumi yanayoongezeka ya nchi kama Uingereza.  Aidha, kunaongoza nchi hizo kwa kina zaidi kwenye muundo tosha kwenye alama za kujifanyia kupitia “sera za mapato” na nyingine kama hizo.  Inaelekea idara ya kazi inaweza kunufaika kutokana na ufumbuzi huo, lakini ninatambua bila shaka kwamba viongozi wa vyama vya wafanyakazi wangepoteza sehemu kubwa ya uwezo wao na hivyo kuukataa moja kwa moja.

 

RELATED ARTICLES