F. A. Hayek’s, “The Use of Knowledge in Society”

F.A. Hayek, Utumiaji wa Maarifa katika Jamii” Uhakiki wa Uchumi wa Marekani, XXXV, Na. 4; Septemba, 1945, Uk. 519-30

 

I

Ni tatizo gani tunalotaka kutatua tunapojaribu kujenga mpango wa uchumi wenye uwiano?  Kwa baadhi ya dhana zilizozoeleka jibu ni rahisi sana.  Kama tuna taarifa zote zinahusika iwapo tunaweza kuanza kutoka kwenye mfumo wa upendeleo, na kama tunaamuru maarifa kamili ya njia zilizopo, tatizo linalobakia ni lile la kimantiki kabisa.   Ndiyo kusema, jibu la swali kuhusu matumizi bora zaidi ya njia zilizopo limo kwenye mawazo yetu.  Masharti ambayo ufumbuzi wa tatizo hili kubwa lazima yakidhi yamefanyiwa kazi na yanaweza kuelezwa vizuri zaidi kwa njia ya kimahesabu: kwa muhtasari, ni yale ambayo viwango vya ziada vya ubadilishaji baina ya bidhaa au vipengele viwili tofauti lazima vilingane katika matumizi yake yote tofauti.

 

Hata hivyo, kwa dhahiri hili sio tatizo la kiuchumi ambalo jamii inakabiliwa nalo.  Na kalkulasi ya kiuchumi ambayo tumeanzisha kwa ajili ya kutatua tatizo hili la kimantiki ijapokuwa ni hatua muhimu katika kutatua tatizo la kiuchumi katika jamii, bado haijatoa jibu.  Sababu ya hili ni kwamba “data” ambazo kalkulasi ya kiuchumi inaanzia, kamwe haziko kwa ajili ya jamii nzima “inayotolewa” kwa lengo moja ambalo linaweza kushughulikia vidokezi na kamwe havitatolewa hivyo.

 

Tabia ya pekee ya tatizo la mfumo wa uchumi wenye uwiano inaamuliwa hasa kwa ukweli kwamba maarifa ya mazingira ambayo lazima tutumie hayajawahi kuwepo kwa maana ya kuunganishwa au kufungamanishwa bali kama sehemu tu zilizotawanyika za maarifa yasiyokamilika na mara kwa mara yanayokinzana ambayo watu wote mmojammoja wanazo.  Tatizo la kiuchumi katika jamii sio tu tatizo la namna ya kutenga raslimali “zinazotolewa” – kama zinapotolewa zinachukuliwa kumaanisha kutolewa kwa lengo moja ambalo kwa makusudi linatatua tatizo lililoletwa na “data” hizi.  Badala yake ni tatizo la jinsi ya kupata matumizi bora zaidi ya raslimali yanayojulikana na mwanajamii yeyote, kwa madhumuni ambayo umuhimu wake wa uwiano unafahamika tu kwa watu hawa.  Au, kwa muhtasari, ni tatizo la utumiaji wa maarifa ambayo hayatolewi kwa mtu yeyote katika ujumla wake.

 

Nina hofu, tabia hii ya tatizo la msingi, imetiwa  gizagiza badala ya kuangaziwa na wataalamu wa hivi karibuni wa nadharia za kiuchumi, hususan na matumizi mengi ya hesabu.  Ingawa tatizo ambalo ninataka kulishughulikia kwanza kwenye makala hii ni tatizo la mfumo wa kiuchumi wenye uwiano, lakini hatimaye nitaelekezwa tena na tena kuonyesha uhusiano wake na baadhi ya maswali ya kimetodolojia.  Vipengele vingi ninavyotaka kueleza ni hakika mahitimisho kuelekea njia mbalimbali za uwazaji wa kimantiki vimeelekezwa bila kutazamiwa.  Lakini kama ninavyoyaona sasa matatizo haya, hii sio ajali.  Ninavyoona ni kwamba migogoro mingi ya sasa kuhusiana na nadharia zote mbili za kiuchumi na sera za kiuchumi zina asili yao moja kwenye dhana potofu kuhusu aina ya tatizo la kiuchumi katika jamii.  Dhana hii potofu badala yake inatokana na uhamishaji usio sahihi kuelekea tatizo la kijamii la tabia ya dhana tulizojitafutia katika kushughulikia majanga asilia.

 

 

[Rejea kwenye Yaliyomo]

 

II

Katika lugha ya kawaida tunaelezea neno “mipango” kama mchangamano wa maamuzi yanayohusiana kuhusu ugawaji wa raslimali zilizopo. Kwa maana hii shughuli zote za kiuchumi ni mipango, na katika jamii yoyote ambamo watu wengi wanashirikiana, mipango hii, yeyote anayeifanya, kwa baadhi ya hatua atapaswa kuzingatia maarifa ambayo, kwanza, hayatolewi kwa mpangaji bali kwa mwingine, ambayo kwa namna fulani hayana budi kuwasilishwa kwa mpangaji.  Njia mbalimbali ambazo maarifa ambayo watu hutegemeza mipango yao huwasilishwa kwao ni tatizo muhimu kwa nadharia yoyote inayoelezea mchakato wa kiuchumi, na tatizo ambalo ndiyo njia bora zaidi ya utumiaji maarifa ambayo awali yalitawanywa miongoni mwa watu wote angalau ni mojawapo ya matatizo makuu ya sera ya kiuchumi – au ya kubuni mfumo wa uchumi wenye ufanisi.

 

Jibu la swali hili linakaribia kuhusiana na swali lile lingine linalojitokeza hapa, ambalo linahusu nani apange mipango.  Ni kuhusu swali hili ambalo ni msingi wa mabishano kuhusu ama mipango ifanywe au isifanywe.  Ni mabishano kuhusu ama mipango ifanywe hasa, na mamlaka moja kwa ajili ya mfumo mzima wa uchumi, au igawanywe miongoni mwa watu wengi.  Mipango katika maana maalumu ambayo neno linatumika katika mabishano ya siku hizi kumaanisha upangaji mkuu – muelekeo wa mfumo mzima wa uchumi kulingana na mpango mmoja uliounganishwa. Ushindani, kwa upande mwingine, maana yake mipango inayogatuliwa na watu wengi tofauti.  Mgawanyo wa nusu nyumba baina ya mbili, ambao watu wengi wanazungumzia lakini wachache wanaipenda wanapoiona, ni mgawanyo wa mipango kwa viwanda vilivyopangwa, au, kwa maneno mengine, kuhodhi.

 

Ni mfumo gani kati ya hii unaelekea kuwa na ufanisi mkubwa unategemea swali ambalo tunaweza kutegemea kwamba kuwepo na utumiaji kamili wa maarifa yaliyopo ufanyike.  Na badala yake, huu unategemea kama tunaelekea zaidi kufanikiwa katika kuweka kwenye mamlaka moja kuu maarifa yote ambayo yanapaswa kutumiwa lakini ambayo mwanzoni yalitawanywa kwa watu wengi tofauti, au katika kuwasilishwa kwa watu maarifa hayo ya nyongeza kama wanavyoyahitaji ili kuwawezesha kuingiza mipango yao na ile ya wengine.     

[Rejea kwenye Yaliyomo]

 

III     

Mara moja itakuwa wazi kuwa kuhusiana na jambo hili, msimamo utakuwa tofauti kuhusiana na aina tofauti za maarifa; na jibu la swali letu kwa hiyo litageukia kwa kiwango kikubwa umuhimu wa uhusiano wa aina tofauti za maarifa; wale ambao wanaelekea zaidi kuwa kwa ajili ya watu mahsusi na wale ambao kwa imani kubwa tutegemee kuwakuta wakimilikiwa na mamlaka yanayoundwa na wataalamu waliochaguliwa vizuri.  Kama ni hivi leo inayodhaniwa kote kuwa anayefuatia atakuwa katika nafasi nzuri sana, ni kwa sababu aina moja ya maarifa, iitwayo, maarifa ya kisayansi, yanachukua nafasi muhimu katika fikra za watu kiasi kwamba tuna kawaida ya kusahau kuwa sio aina pekee ambayo inafaa.  Inaweza kukubalika kuwa, kuhusiana na maarifa ya kisayansi, jopo la wataalamu wanaweza kuwa katika nafasi bora zaidi ya kushika maarifa yote bora yanayopatikana – ingawaje hili bila shaka ni kuhamisha ugumu katika tatizo la kuchagua wataalamu.  Ninachotaka kueleza ni kwamba, hata kudhania kuwa tatizo hili linaweza kutatuliwa, ni sehemu ndogo tu ya tatizo kubwa sana.

 

Hivi leo ni karibu uasi kupendekeza kuwa maarifa ya kisayansi sio jumla ya maarifa yote.  Mawazo kidogo yataonyesha kuwa bila shaka kuna chombo cha maarifa muhimu lakini yasiyopangwa ambayo yawezekana hayawezi kuitwa ya kisayansi kwa maana ya maarifa ya kanuni: maarifa ya mazingira mahsusi ya muda na mahali.  Ni kuhusiana na hili kwamba kila mtu ana manufaa zaidi ya wengine wote kwa sababu anazo taarifa pekee ambazo matumizi yanayofaa yangeweza kufanywa, lakini ambayo matumizi yanaweza tu kufanyika kama tu maamuzi yanayoyategemea yanaachwa kwake au yanafanywa kwa ushirikiano wake mkubwa.  Tunahitaji kukumbuka tu ni kiasi gani tunapaswa kujifunza katika kazi yoyote inatubidi tujifunze kiasi gani baada ya sisi kukamilisha mafunzo yetu ya kinadharia, ni muda mkubwa kiasi gani katika maisha yetu ya kazi tunautumia kujifunza kazi mahsusi,  na ni kiasi gani raslimali ya thamani katika nyanja zote za maisha ni maarifa ya watu, ya hali ya eneo, na ya mazingira maalumu.  Kuifahamu mashine na kutokuitumia kikamilifu, au ujuzi wa mtu ambao hautumiwi vizuri, au kufahamu kuwa kuna akiba ya ziada ambayo inaweza kuchukuliwa wakati kuna upungufu wa bidhaa, kuna manufaa sawa kama maarifa ya mbinu bora mbadala.  Na msafirishaji shehena anayepata kipato chake kwa kutumia mashua sanyi tupu au zenye nusu mzigo kwa safari, au wakala wa serikali ambaye maarifa yake yote ni takriban yale ya fursa za muda pekee, au “arbitrageur” anayepata faida kutokana na tofauti za eneo za bei za bidhaa, wote wanafanya shughuli muhimu zinazozingatia maarifa maalumu ya mazingira ya muda unaokwenda kasi usiojulikana na wengine.

 

Ni kitu cha ajabu kwamba aina hii ya maarifa hivi leo inapaswa kwa ujumla kuchukuliwa kama aina ya dharau na kwamba mtu yeyote ambaye kwa maarifa hayo anapata manufaa zaidi ya mwingine aliyejaa nadharia au maarifa ya ufundi anafikiriwa kuwa amekosa heshima.  Kupata manufaa kutokana na maarifa mazuri ya huduma za mawasiliano au usafiri wakati mwingine huchukuliwa kama udanganyifu, ingawa ni muhimu sawia kwamba jamii itumie fursa katika hili kama katika kutumia ugunduzi mpya wa kisayansi.  Kwa kiasi kikubwa maoni haya yaliathiri mkabala wa kuelekea kwenye biashara kwa ujumla, ikilinganishwa na ule wa uzalishaji.  Hata wachumi wanaojiona kuwa hawawezi kuathiriwa na uwongo wa yakinifu wa zamani mara kwa mara hufanya kosa hilohilo – pale ambapo shughuli zinazoelekezwa  katika upataji wa maarifa hayo zinahusika – ni dhahiri kwa sababu katika mpango wao wa vitu maarifa yote ya aina hiyo yanapaswa “kutolewa”.  Wazo la jumla sasa linaelekea kuwa maarifa yote ya aina hiyo yanapaswa hasa kuwa stahili ya kila mtu, na shutuma za kukosa  mantiki zinazolinganishwa dhidi ya mfumo wa uchumi uliopo zinazingatia mara kwa mara ukweli kwamba haupatikani hivyo.  Mtazamo huu unapuuza ukweli kwamba mbinu za kueneza maarifa hayo kote iwezekanavyo hasa ni tatizo ambalo tunapaswa kulitafutia jibu.

 

[Rejea kwenye Yaliyomo]

 

IV

Iwapo siku hizi za kupunguza umuhimu wa maarifa ya mazingira mahususi ya muda na mahali, hili linahusishwa kwa karibu na umuhimu mdogo zaidi ambao unaambatishwa na mabadiliko.  Hakika, kuna vipengele vichache vya dhana (kwa kawaida vilivyodokezwa tu) vilivyoundwa na “wapangaji wa mipango” vinavyotofautiana na vile vya wapinzani wao hasa kuhusiana na umuhimu na mabadiliko makubwa ya mipango ya uzalishaji kuwa lazima.  Bila shaka, kama mipango ya uchumi ya kina ingeweza kupangwa mapema kwa muda mrefu kiasili na kufuatwa, ili kwamba maamuzi muhimu zaidi ya kiuchumi yatahitajika, jukumu la kubuni mpango mpana unaotawala shughuli zote za kiuchumi lingekuwa sio gumu sana.

 

Labda, ni muhimu kusisitiza kuwa matatizo wakati wote katika uchumi yanatokea tu kwa ajili ya mabadiliko.  Ili mradi mambo yanaendelea kama mwanzo, au angalau kama yalivyokusudiwa, hakukutokea matatizo mapya yanayohitaji uamuzi, hakuna umuhimu wa kupanga mpango mpya.  Imani ya kwamba mabadiliko, au angalau marekebisho ya siku hadi siku, yamekuwa na umuhimu mdogo siku hizi inaonyesha ubishani kuwa matatizo ya kiuchumi yamekuwa pia na umuhimu mdogo.  Imani hii katika kupungua kwa umuhimu wa mabadiliko ni, kwa ajili hiyo, inashikiliwa na watu haohao wanaodai kuwa umuhimu wa uzingativu wa kiuchumi umerudishwa nyuma na umuhimu unaongezeka wa maarifa ya kiteknolojia.

 

Ni kweli kwamba, kwa zana bora katika uzalishaji wa kisasa, maazimio ya kiuchumi yanahitajika katika vipindi virefu tu, kama pale kiwanda kipya kinapotakiwa kujengwa au mchakato mpya kuanzishwa?  Ni kweli kwamba, mara mtambo unapokuwa umejengwa, kinachobakia ni karibu ufundi, unaoamuliwa na sifa ya mtambo, na kuacha kiasi kidogo kubadilishwa katika kufuata mazingira yanayoendelea kubadilika ya wakati?

 

Imani iliyoenea kiasi ya kuthibitisha, kwa jinsi ninavyoweza kuhakikisha, haikutokana na uzoefu wa kiutendaji wa mfanyabiashara.  Kwenye tasnia ya ushindani katika kiwango chochote na tasnia hiyo pekee inaweza kuwa kama jaribio – jukumu la kuifanya gharama isipande inahitaji mapambano ya siku zote, yanayochukua sehemu kubwa ya nguvu ya meneja.  Ni rahisi kiasi gani kwa meneja mzembe kutapanya viwango mbalimbali vinavyotegemewa ili kupata faida, na kiufundi, kuzalisha kwa kiwango kikubwa cha gharama, miongoni mwa maeneo ya pamoja ya uzoefu wa biashara ambao hauelekei – kufahamika sawa katika utafiti wa mchumi.  Nguvu halisi ya shauku, inayoelezewa mara kwa mara na wazalishaji na wahandisi, kuruhusiwa kuendelea bila kuzuiwa na fikra za gharama za fedha, ni ushuhuda dhahiri kwa kiasi ambacho vipengele hivi vinaingia kwenye kazi zao za kila siku.

 

Sababu moja kwa nini wachumi wanazidi kuelekea kusahau  mabadiliko madogomadogo ya mara kwa mara ambayo yanatengeneza picha nzima ya kiuchumi labda ni kuongezeka kwa shughuli zao na mikusanyiko ya takwimu, ambazo zinaonyesha uthabiti mkubwa sana kuliko mzunguko wa maelezo.  Uthabiti linganifu wa mkusanyiko hauwezi, hata hivyo, kutolewa maelezo – kwa kuwa mara nyingi watakwimu wanaelekea kufanya – kwa “sheria ya idadi kubwa” au fidia ya pamoja ya mabadiliko ya jumla.  Idadi ya vipengele ambavyo tunapaswa kushughulikia sio kubwa ya kutosha kwa kani hizo za bahati kutengeneza uthabiti.  Mtiririko unaoendelea wa bidhaa na huduma unadumishwa na marekebisho ya makusudi ya mara kwa mara, kwa mielekeo mipya inayotolewa kila siku kwa kuzingatia mazingira ambayo hayakufahamika siku iliyotangulia, kwa B kuingia mara moja wakati A anaposhindwa kuwasilisha.  Hata mtambo mkubwa na unaotumia mashine za hali ya juu huendelea kutembea hasa kwa sababu ya mazingira ambayo huweza kuchukua aina zote za mahitaji yasiyokusudiwa; vigae kwa ajili ya paa lake, viandikio kwa ajili ya fomu zake, na maelfu yote na aina ya zana ambamo huweza kujitosheleza na ambayo mipango ya uendeshaji wa mtambo inahitaji kupatikana tayari katika soko.

 

Labda, pengine hii ni hoja ambayo napaswa kuitaja kwa muhtasari ya ukweli kwamba aina ya maarifa ambayo nimekuwa nikihusika nayo ni maarifa ambayo kwa aina yake hayawezi kuingia kwenye takwimu na kwa hiyo hayawezi kupelekwa kwenye mamlaka yoyote kuu kwa namna ya takwimu.  Takwimu ambazo zingeweza kutumiwa na mamlaka hiyo kuu zitahitajika kufikiwa kwa usahihi kwa kutoa kutoka kwenye tofauti ndogo kati ya vitu, kwa kujumuisha pamoja, kama raslimali za aina moja, vitu vinavyotofautiana kulingana na eneo, ubora, na maelezo mengine, kwa namna ambayo inaweza kuwa muhimu sana kwa uamuzi mahsusi.  Inafuatia kutokana na hili kwamba upangaji mkuu unaozingatia taarifa za kitakwimu kwa namna yake haziwezi kuzingatia mazingira haya ya muda na mahali na kwamba mpangaji mkuu atapaswa kutafuta njia au nyingine ambayo maamuzi yanayoyategemea yataweza kuachwa kwa “mtu papohapo”.

 

[Rejea kwenye Yaliyomo]

 

V

Kama tunaweza kukubali kwamba tatizo la msingi la uchumi la jamii ni lile la kubadilika kutokana na mabadiliko katika mazingira maalumu ya muda na mahali, yaelekea kukubali kwamba maamuzi ya mwisho lazima yaachwe kwa watu ambao ndio wanaoyafahamu mazingira haya, ambao wanafahamu moja kwa moja kuhusu mabadiliko husika na kuhusu raslimali zinazopatikana mara moja kuweza kuwafikia.  Hatuwezi kutarajia kwamba tatizo hili litatatuliwa kwa kuwasilisha kwanza maarifa yote haya kwa bodi kuu ambayo, baada ya kuingiza maarifa yote, inatoa maagizo yake.  Lazima tulitatue kwa namna ya ugatuaji madaraka.  Lakini hili linajibu sehemu tu ya tatizo letu.  Tunahitaji ugatuaji madaraka kwa sababu ni kiwa njia hiyo ndiyo tutaweza kuhakikisha kuwa maarifa ya mazingira maalumu ya muda na mahali yatatumiwa papo hapo.  Lakini “Mtu papo hapo” hawezi kuamua peke yake kuhusu misingi ya ukomo wake bali maarifa kamili ya ukweli wa mazingira yake yaliyopo.  Bado linabakia tatizo la kuwasilisha kwake taarifa hizo zaidi kama anavyohitaji kukidhi maamuzi yake kwenye mpangilio mzima wa mabadiliko ya mfumo mkubwa zaidi wa uchumi.

 

Ni maarifa kiasi gani anahitaji ili kupata  mafanikio?  Ni matukio yapi ambayo yanatokea mbali ya upeo wa maarifa yake ya sasa hivi ambayo ni muhimu kwa uamuzi wake wa sasa, na ni kiasi gani anahitaji kufahamu?

 

Karibu hakuna kitu kinachotokea popote duniani ambacho hakina athari kuhusiana na uamuzi anaopaswa kufanya.  Lakini hahitaji kujua matukio haya kama yalivyo, wala athari zake zote.   Kwake haijalishi kwa nini katika wakati fulani skurubu za ukubwa mmoja zinahitajika kuliko nyingine, kwa nini mifuko ya karatasi inapatikana kwa urahisi zaidi kuliko mifuko ya maturubai, au kwa nini kazi za ujuzi, au vifaa fulani vya mashine, kuna wakati zinakuwa ngumu kupatikana.  Yote yaliyo muhimu kwake yeye ni jinsi gani ilivyo vigumu zaidi au afadhali zaidi kununua, zikilinganishwa na vitu vingine ambavyo pia anahusika navyo, au ni kwa haraka kiasi gani vitu mbadala anavyozalisha au kutumia vinahitajika.  Wakati wote ni swala tu la umuhimu wa vitu mahsusi anavyohusika navyo, na sababu zinazobadilisha umuhimu wake hazina maana kwake mbali na athari kwa vitu dhahiri katika mazingira yake mwenyewe.

 

Ni katika uhusiano huu ndio kile mlichokiita “kalkulasi za kiuchumi” halisi zinatusaidia angalau kwa analojia, kuona jinsi tatizo hili linavyoweza kutatuliwa, na ukweli ni kwamba linatatuliwa, kwa mfumo wa bei.  Hata mtu mmoja anayedhibiti, anayemiliki data zote kwa ajili ya mfumo wa uchumi mdogo, unaojitosheleza hatapaswa – wakati wote marekebisho madogo katika mgawanyo wa raslimali unapohitajika – kupitia uhusiano wote baina ya madhumuni na njia ambavyo yawezekana vikaathiriwa.  Hakika ni mchango mkubwa wa mantiki halisi ya uchaguzi ambao umeuonyesha kwa kuthibitisha kuwa hata kichwa kimoja hicho kingeweza kutatua aina hii ya tatizo kwa kupanga na mara kwa mara kutumia viwango vya ulinganifu (au “thamani”, au viwango vya pembeni vya mbadala”), yaani kwa kuambatisha kwenye kila raslimali adimu alama ya numerali ambayo haiwezi kutokana na mali yoyote inayomilikiwa na kitu hicho, bali inayoakisi, au ambamo imepunguzwa, umuhimu wake kwa ajili ya muundo mzima wa njia – madhumuni.  Katika mabadiliko yoyote madogo atapaswa tu kuzingatia vielelezo hivi vya idadi (au “thamani”) ambamo taarifa zote muhimu zimeminywa, na kwa kurekebisha idadi moja hadi nyingine, anaweza kupanga upya ipasavyo mielekeo yake bila ya kuhitajika kutatua fumbo zima kwanza au bila ya kuhitaji katika hatua yoyote ile kulipima mara moja kwenye vipengele vyake vyote.

 

Kimsingi, katika mfumo ambamo maarifa ya mambo husika yanasambazwa – miongoni mwa watu wengi, bei huweza kutumika kuratibu shughuli tofauti za watu tofauti kwa namna hiyohiyo ambayo thamani nafsi huratibu sehemu za mpango wake.  Inafaa kutafakari kwa muda mfano rahisi sana na eneo la pamoja la tendo la mfumo wa bei kuona ni nini unafanikisha hasa.  Chukulia kwamba mahali fulani duniani fursa mpya ya utumiaji wa baadhi ya mali ghafi, kama vile, bati, imepanda, au kwamba mojawapo ya vyanzo vya usambazaji wa bati kimeondolewa.  Haidhuru kwa madhumuni yetu – na ni muhimu sana kwamba isituletee shida – ni sababu ipi kati ya hizi mbili iliyosababisha bati liwe adimu sana.  Wanachohitaji tu watumiaji wa bati kufahamu ni kuwa bati walilozoea kutumia sasa linatumika sehemu nyingine kwa faida zaidi na kwamba, matokeo yake, lazima kubana matumizi ya bati.  Hakuna umuhimu wa wengi wao hata kufahamu ni wapi mahitaji ya haraka yametokea, au kwa ajili ya mahitaji mengine wanayopaswa kutumia kwa uangalifu.  Laiti baadhi yao wangeyafahamu moja kwa moja mahitaji mapya, na kuhamishia raslimali huko, na kama watu ambao wanalifahamu pengo jipya na hivyo kuliziba kwa raslimali nyingine, athari zitaenea haraka kwenye mfumo mzima wa uchumi na kuathiri sio tu matumizi yote ya bati bali pia yale ya mbadala wake na mbadala wa mbadala  huu, usambazaji wa vitu vyote vinavyotengenezwa kwa bati, na mbadala wake, na kadhalika;  na vyote hivi bila ya wingi wa vifaa hivyo katika kuleta mbadala huu kwa kutokujua chochote kabisa kuhusu chanzo cha mabadiliko haya.  Yote yanakuwa kama soko moja, sio kwa sababu mmoja wao yeyote amechunguza – uwanja mzima, bali kwa sababu nyanja zao chache za maono binafsi zinapishana ili kupitia watu wengi wakati taarifa husika inasilishwa kwa wote.  Ukweli mtupu ni kwamba kuna bei moja kwa bidhaa yoyote – au tuseme kuwa bei za eneo fulani zinahusiana kwa namna inayoamuliwa na gharama ya usafiri, n.k. – kuleta ufumbuzi ambao kidhana ungeweza kufikiwa na kichwa kimoja chenye taarifa yote ambayo kwa ukweli husambazwa miongoni mwa watu wote wanaohusika katika mchakato.

 

[Rejea kwenye Yaliyomo]

 

VI

Lazima tuuangalie mfumo wa bei kama utaratibu wa kuwasilisha taarifa kama tunataka kuelewa kazi yake halisi – kazi ambayo, bila shaka, haina ufanisi kwa kuwa bei zilizotajwa zimekuwa hazibadiliki kabisa.( Hata pale ambapo bei zimekuwa hazibadilikibadiliki, hata hivyo nguvu ambayo ingefanya kazi kupitia mabadiliko ya bei bado inafanya kazi kwa kiwango kupitia mabadiliko ya masharti mengine ya mkataba).  Ukweli muhimu kuhusu mfumo huu ni uchumi wa maarifa ambao unafanya kazi, au kiasi gani kidogo ambacho washiriki mmojammoja wanahitaji kufahamu ili kuweza kuchukua hatua sahihi.  Kwa namna iliyofupishwa, kwa aina ya alama, taarifa tu muhimu sana hupitishwa na kupitishwa tu kwa wale wanaohusika.  Ni zaidi ya sitiari kuelezea mfumo wa bei kama aina ya mashine ya kuorodheshea mabadiliko, au mfumo wa mawasiliano ya simu unaowezesha wazalishaji mmojammoja kutazama mwenendo wa waelekezaji wachache, kama mhandisi anavyoweza kutazama mikono ya bamba linaloonyesha vipimo, ili kurekebisha shughuli zao kwa mabadiliko ambayo wanaweza kamwe wasiyafahamu zaidi ya yalivyoakisiwa kwenye mwenendo wa bei.

 

Bila shaka, marekebisho haya yawezekana sio “kamili” kwa maana ambayo mchumi anayafikiria kwenye uchambuzi wake ulio linganifu.  Lakini nina hofu kuwa tabia zetu za kinadharia za kukabili tatizo kwa dhana ya takriban maarifa kamili kwa upande wa karibu kila mtu zimetufanya kwa kiasi fulani vipofu kwa kazi halisi ya utaratibu wa bei na kusababisha tutumie viwango vinavyopotosha katika kuamua ufanisi wake.  Jambo la kushangaza ni kwamba katika tukio kama hilo la uhaba wa mali ghafi moja, bila ya agizo kutolewa, bila ya labala ya watu kadhaa kufahamu chanzo, makumi elfu ya watu ambao utambulisho wao usingeweza kuthibitishwa baada ya miezi ya uchunguzi, wanafanywa watumia vitu au bidhaa zake kwa ubanifu zaidi, yaani wanaelekea katika mwelekeo sahihi.   Bado inashangaza kama, katika dunia inayobadilika mara kwa mara, sio wote wakataopatana kuwa viwango vyao vya faida vibakie katika ngazi hiyohiyo isiyobadilika au ya “kawaida”.

 

Nimetumia neno “kushangaza” kwa makusudi kabisa kumshtua msomaji mbali na ridhaa ambayo mara nyingi huchukulia utendaji wa chombo hiki kuwa wa kawaida tu.  Ninashawishika kuwa kama ungekuwa matokeo ya ubunifu wa makusudi wa binadamu, na kama watu wanaoongozwa na mabadiliko ya bei wangeelewa kuwa uamuzi wao unakwenda mbali ya lengo la sasa, utaratibu huu ungepelekea kuwa ni mojawapo ya ushindi mkubwa sana wa akili ya binadamu.  Balaa lake ni mara mbili kwamba sio zao la ubunifu wa binadamu na kwamba wanaoongozwa nao kwa kawaida hawajui kwa nini wamefanywa kufanya kile wanachokifanya.  Lakini wale wanaopigia kelele “mwelekeo wa ufahamu” – na ambao hawawezi kuamini kwamba kitu chochote kimetokea bila kupangwa (na hata bila ya sisi kuuelewa) kinapaswa kutatua matatizo ambayo tusingeweza kuyatatua kwa ufahamu – wakumbuke haya:  Tatizo ni hasa namna ya kuongeza muda wa udhibiti wa kichwa chochote kimoja; na kwa hiyo, namna ya kuachana na umuhimu wa udhibiti wa ufahamu, na namna ya kutoa vivutio ambavyo vitawafanya watu wafanye vitu vya kufaa bila ya yeyote kuwaambia wafanye nini.

 

Kwa vyovyote tatizo tunalopata hapa si la kipekee kwa wachumi lakini hutokea kwa kuhusishwa na karibu na mambo yote halisi ya kijamii, pamoja na lugha na vipengele vyetu vingi vya urithi wa utamaaduni, na kuleta tatizo la msingi la kinadharia la sayansi jamii yote.  Kama Alfred Whitehead alivyosema katika uhusiano mwingine,” nakala – vitabu na watu mashuhuri wanapotoa hotuba, kwamba lazima tuanzishe tabia ya kufikiria kile tunachokifanya.  Na kinyume chake.  Ustaarabu unaendelea kwa kuongeza idadi ya shughuli ambazo tunaweza kuzifanya bila ya kufikiria kile tunachokifanya.  Na kinyume chake.  Ustaarabu unaendelea kwa kuongeza idadi ya shughuli ambazo tunaweza kuzigawanya bila ya kufikiria.”  Hili lina umuhimu mkubwa katika uwanja wa jamii.  Mara kwa mara tunatumia fomyula, alama na kanuni ambazo maana zake hatuzielewi na kwa matumizi ambayo tunajinufaisha na msaada wa maarifa ambayo binafsi hatuna.  Tumeanzisha taratatibu na asasi hizi kwa kujenga tabia na asasi ambazo zimeonyesha mafanikio katika uwanja wake na ambazo badala yake zimekuwa msingi wa ustaarabu tulioujenga.

 

Mfumo wa bei ni mojawapo tu ya miundo ambayo mtu amejifunza kuutumia (ingawa bado yuko mbali katika kujifunza kuutumia vizuri) mara baada ya kuhangaika nao bila ya kuuelewa.  Kupitia huo sio tu mgawanyo wa kazi bali pia utumiaji uliodhibitiwa wa raslimali unaozingatia maarifa yanayogawanywa sawa ambao umewezekana.  Watu wanaopenda kukejeli pendekezo lolote kuwa hili linaweza kuwa hivyo kwa kawaida wanapotosha hoja kwa kusingizia kwamba inadai kuwa kwa muujiza mfumo huo umekuwa wenyewe ambao unafaa zaidi ustaarabu wa kisasa.  Ni kinyume chake: mtu ameweza kuanzisha mgawanyo huo wa kazi ambao unazingatia ustaarabu wetu kwa kuwa amewahi kuhangaikia mbinu iliyowezesha.  Asingefanya hivyo, bado angeweza kuanzisha mwingine, yote pamoja tofauti, aina ya ustaarabu, kitu kama “hali” ya mchwa, au aina nyingine pamoja isiyofikirika.  Tunayoweza kusema yote ni kwamba hakuna ambaye amefanikiwa kubuni mfumo mbadala ambao baadhi ya tabia za ule uliopo zinaweza kuhifadhiwa ambazo zinapendwa hata na wale ambao walizishambulia – hasa kiasi cha mtu kuweza kuchagua kazi zake na hatimaye kutumia kwa uhuru maarifa na stadi yake mwenyewe.

 

[Rejea kwenye Yaliyomo]

 

VII

Ni bahati katika njia nyingi kwamba mabishano kuhusu ulazima wa mfumo wa bei kwa ajili ya mkokotoo wowote wa uwiano katika jamii changamano sasa hayafanywi tu baina ya kambi zenye maoni tofauti ya kisiasa.  Hoja kwamba bila ya mfumo wa bei tusingeweza kuhifadhi jamii inayozingatia mgawanyo huo mkubwa wa kazi wakati ulipotambulishwa mara ya kwanza na Von Mises, miaka ishirini na mitano iliyopita.  Hivi leo ugumu ambao baadhi ya watu bado wanaupata katika kuukubali sio tena wa kisiasa, na huu unafanya mazingira yanayofaa zaidi kwa majadiliano yenye mantiki.  Tunapomkuta Leon Trosky akihoji kuwa “hesabu za kiuchumi zisingewazika bila ya kuwa na uhusiano wa masoko”; Profesa Oscar Lange anapomwahidi Profesa Von Mises sanamu kwenye ukumbi wa marumaru wa Bodi kuu ya Mipango ya hapo baadaye; na Profesha Abba P. Lerner alipomgundua upya Adam Smith na kusisitiza kuwa utumiaji muhimu wa mfumo wa bei unajumuisha kumshawishi mtu, wakati huohuo akitafuta faida yake mwenyewe, tofauti hazitaweza tena kupachikwa kwenye athari za kisiasa.  Maoni yaliyobakia yanaonyesha wazi kutokana na tofauti za kisomi, na hususan za kimethodolojia.

 

Taarifa ya hivi karibuni iliyotolewa na Profesa Joseph Schumpeter kuhusu Capitalism, Soialism and Democracy inaonyesha wazi moja ya tofauti za kimethodolojia ambazo ninazo katika kumbukumbu.  Mwandishi wake ana sifa nyingi miongoni mwa wachumi ambao wanalikabili suala la kiuchumi kulingana na tawi fulani la falsafa umbile.  Kwake yeye jambo hili linaonekana kama halisi kwa kupewa idadi ya bidhaa zinazohusiana moja kwa moja, takriban, lingeonekana, bila ya afua yoyote ya akili ya binadamu.  Ni kwa kupingana tu na usuli huu ndipo ninaweza kutoa maelezo ya (kwangu mimi ya kushtua) kauli ifuatayo.  Profesa Schumpeter anahoji kuwa uwezekano wa mkokotoo wa uwiano kama hakuna masoko kwa ajili ya vipengele vya uzalishaji unafuatia kwa mnadharia “kutokana na suala la mwanzo kwamba watumiaji katika kutathmini (‘kuhitaji’) bidhaa za watumiaji, ipso facto pia hutathmini maana ya uzalishaji ambao unaingia katika uzalishaji wa bidhaa hizi”1.

 

Tukichukulia kikawaida tu, kauli hii sio kweli.  Watumiaji hawafanyi chochote kama hicho.  Anachomaanisha Profesa Schumpeter “ipso facto” ni kwamba tathmini ya vipengele vya uzalishaji imeonyeshwa katika, au inafuatia kutoka, kwenye tathmini ya bidhaa za mtumiaji.  Lakini hili pia sio sahihi.  Uhusishaji ni uhusiano wa kimantiki ambao unaweza kuelezwa tu kwa mawazo yaliyomo wakati huo huo kwa kichwa kimoja na hiyohiyo.  Ni wazi, hata hivyo, kwamba thamani za vipengele vya uzalishaji hazitegemei tu thamani ya bidhaa za watumiaji bali pia kuhusu masharti ya usambazaji wa vipengele mbalimbali vya uzalishaji.  Ni kwa akili tu ambayo inafahamu vidokezi vyote hivi ndio jibu litafuatia kutoka kwenye maelezo yaliyotolewa kwake.  Tatizo lililopo hata hivyo, linatokea kwa sababu maelezo haya hayatolewi hivyo kamwe kwa kichwa kimoja, na kwa sababu, matokeo yake, ni muhimu kwamba katika utatuzi wa matatizo maarifa yanapaswa kutumiwa yaani kusambazwa miongoni mwa watu wengi.

 

Hivyo, tatizo haliwezi kutatuliwa kwa namna yoyote kama tunaweza kuonyesha kuwa maelezo yote, kama kichwa kimoja kingeyafahamu (kama kinadharia tete tunayadhania kutolewa kwa mchumi mchunguzi), kwa kutafuta ufumbuzi; badala yake lazima tuonyeshe jinsi ufumbuzi unavyotolewa kwa mwingiliano wa watu ambao kila mmoja ana maarifa kwa sehemu tu.  Kuona maarifa yote ya kutolewa kwa kichwa kimoja kwa namna hiyohiyo tunayaona yakitolewa kwetu kama wachumi wanavyoelezea wanavyoliona matatizo mbalimbali na kupuuza kila kitu ambacho ni muhimu na cha maana katika dunia halisi.

 

Kwamba mchumi wa msimamo wa Profesa Schumpeter angeangukia kwenye mtego ambao utata wa neno “datum” (data) zilizopangwa katika hadhari usingeweza kuelezewa tu kama kosa la kawaida.  Inamaanisha kwamba kuna kitu ambacho kimsingi sio sahihi pamoja na mkabala ambao kwa kawaida unapuuza sehemu muhimu ya jambo ambalo tunapaswa kulishughulikia:  hali isiyotimilifu ambayo haiepukiki ya maarifa ya mtu na umuhimu unaofuatia kwa ajili ya mchakato wa kuwasilishia na kupata maarifa mara kwa mara.  Mkabala wowote, kama ule uchumi wa kimahesabu pamoja na mlinganyo sawia ambao huanzia kwenye dhana kwamba maarifa ya watu yanahusiana na lile ambalo ni jukumu letu kuu kuelezea.  Ninakubali kuwa uchambuzi wa ulinganifu wa mfumo una kazi kubwa ya kufanya.  Lakini inapofikia kiwango cha kupotosha baadhi ya wanafalsafa wetu kuamini kwamba hali inayoelezewa ina umuhimu wa moja kwa moja katika utatuzi wa matatizo ya kiutendaji, wakati umefika tukumbuke kuwa haishughulikii kabisa mchakato wa kijamii na kwamba sio zaidi ya utangulizi muhimu katika uchunguzi wa tatizo kuu.

 

Maelezo

[1] J. Schumpeter, Capitalism, Socialism, and Democracy (New York; Harper, 1942), uk. 175. Ninaamini Profesa Schumpter, pia ni mwandishi wa awali wa hoja ya uongo inayosema kuwa Pareto na Barone wametatua tatizo la mkokotoo wa kijamaa.  Walichofanya wao, na wengine wengi ni kutaja tu masharti ambayo mgawanyo wianifu wa raslimali ungekidhi na kueleza kuwa haya yalikuwa sawa na masharti ya ulinganifu wa soko la ushindani.  Hiki ni kitu ambacho ni tofauti na kufahamu jinsi mgawanyo wa raslimali unaokidhi masharti unavyoweza kutekelezwa.  Pareto mwenyewe (ambaye kwake Barone amechukua karibu kila kitu atapaswa kusema), mbali na kudai kuwa ametatua tatizo la kiutendaji, ukweli anakana kwamba linaweza kutatuliwa bila ya msaada wa soko.  Tazama kitabu chake Manuel d’ e’conomie pure (2nd et., 1927), uk. 233-34. Njia inayofaa imenukuliwa kwenye tafsiri mwanzoni mwa makala kuhusu “Socialist Calculation:  ‘Ufumbuzi’ wa kiushindani,’ katika Economica, New Series, Vol. VIII, No. 26 (Mei, 1940) uk. 125.

RELATED ARTICLES