Frederic Bastiat’s, “What Is Seen and What Is Not Seen”

Bastiat, Frederic (1801-1850)

1.1
Kinachoonekana na Kisichoonekana

Katika uwanja wa kiuchumi kitendo, tabia, taasisi, sheria husababisha sio tu athari moja, bali mfululizo wa athari.  Kati ya athari hizi, ya kwanza pekee ndiyo ya moja kwa moja; hutokea papohapo pamoja na chanzo chake; inaonekana.  Athari nyingine hutokea baadaye tu; hazionekani; tuna bahati kama tunaziona kabla.

1.2

Kuna tofautu moja tu baina ya mchumi mbaya na yule mzuri: Mchumi   mbaya anajifungia mwenye katika athari inayoonekana; mchumi mzuri anazingatia athari zote mbili zile zinazoweza kuonekana na zile athari ambazo lazima zionekane kabla.

1.3

Bado tofauti hii ni kubwa mno; kwa kuwa karibu wakati wote hutokea     hutokea wakati matokeo ya mara moja ni ya kufaa, matokeo ya baadaye ni ya kutisha mno, na kinyume chake.  Kutoka hapo kinafuata kwamba mchumi mbaya hufanya kitafuatiwa na uovu mkubwa kwa ajili ya uovu wa muda mfupi.

1.4

Hakika kitu hichohicho ni kweli kwa afya na maadili.  Mara nyingi,

tunda la kwanza la mazoea linavyokuwa tamu sana, ndivyo matunda yatakayofuatia yatakavyokuwa machungu zaidi: kwa mfano, ufisadi, uzembe, ubadhirifu.  Mtu anapopendezewa na athari ambayo inaonekana na hajajifunza bado kutambua athari ambazo hazionekani, anajiingiza kwenye tabia mbaya, sio tu mwelekeo wa kujisikia, bali wa makusudi.

1.5

Hili linaelezea mabadiliko ya lazima ya uchungu ya mwanadamu.  Ujinga unamzunguka katika chimbuko lake; kwa hiyo, anarekebisha vitendo vyake kulingana na matokeo yake ya kwanza, yale ambayo, katika utoto wake, anaweza kuyaona.  Ni baada tu ya muda mrefu ndipo anapoweza kujifunza kuzingatia mengine**2.  Mabwana wawili tofauti wanamfundisha somo hili uzoefu na uangalifu. Uzoefu unafundisha mambo yanayofaa kuleta matokeo yanayotakiwa lakini kikatili.  Unatuelekeza katika athari zote za jambo kwa kutufanya tuzihisi, na hatimaye hatuwezi kushindwa kujifunza, kutokana na kujichoma wenyewe, kwamba moto unachoma.  Ningependelea kwa jinsi inavyowezekana, kumbadilisha mwalimiu huyu mkali na mwingine ambaye ni mpole zaidi: uangalifu.  Kwa sababu hiyo nitachunguza matokeo ya matukio mengi ya kiuchumi, kutofautisha vile vinavyoonekana na vile visivyoonekana.

 

1.6
1.         Dirisha lililopasuka                                                                                

Je,  umekwishawahi kuwa shahidi wa hasira za raia mashuhuri Goodfellow, *1 wakati mtoto wake wa kiume asiyeonyeka alipovunja kioo cha dirisha?  Ungekuwepo katika tukio hili, hakika lazima pia ungeona kuwa watazamaji, hata kama ni wengi kama thelathini, wangeelekea kukubaliana kumfariji mmiliki huyu mwenye bahati mbaya: Ni upepo mbaya unaotufanyia mabaya.  Ajali kama hizo hufanya viwanda viendelee na kazi kila mtu anatakiwa kupata riziki.  Mafundi wa kutia vioo madirishani wangefanya kama hakuna mtu wa kupasua dirisha?”

1.7

Sasa, fomyula hii ya kuliwaza ina nadharia nzima kwamba ni wazo       kwetu la kufichua, flagrante delicto, katika suala hili rahisi sana kwa kuwa ni sawa kabisa na lile ambalo, kwa bahati mbaya, unahusu taasisi zetu nyingi za kiuchumi.

1.8

Fikiria kwamba itagharimu faranga sita kurekebisha sehemu iliiyoharibika.  Kama una maana kwamba ajali inatoa thamani ya faranga sita za kuunga mkono kiwanda kilichotajwa hapo juu, ninakubali.  Sipingi kwa namna yoyote ile; kujipongeza, na kumbariki moyoni mwake mtoto mzembe.  Hicho ndicho kinachoonekana.

1.9

Lakini, kwa njia ya makato, unahitimisha, kama inavyoonekana         mara kwa mara, kwamba ni vizuri kupasua madirisha, kwamba inasaidia kuzungusha fedha, kwamba matokeo yake ni kukiunga mkono kiwanda kwa ujumla, ninalazimika kupaaza sauti:  Hili halitasaidia kamwe!  Nadharia yako inaishia  katika kinachoonekana.  Haishughulikii kile kisichoonekana.

1.10

Haionekani kwamba, kwa kuwa raia wetu ametumia faranga sita    kwa jambo moja, hataweza kuzitumia kwa kingine.  Hakionekani kwamba kama asingekuwa na kioo cha dirisha cha kurudishia, angerudishia, kwa mfano, viatu vyake vilivyochakaa au kuongeza kitabu cha kwenye maktaba yake.  Kwa ufupi, angeweza kutumia faranga zake sita kwa mambo mengine ambayo asingekuwa nayo sasa.

1.11

Hebu tufikirie sasa kiwanda kwa ujumla.  Kwa kupasuka kwa dirisha,

kiwanda cha vioo kimepata thamani ya faranga sita ya kuungwa mkono; hicho ndicho kinachoonekana.

1.12

Dirisha lisingepasuka, kiwanda cha viatu (au vingine) vingepata thamani    ya faranga sita ya kungwa mkono; hicho ndicho kisichoonekana.

1.13

Kama tunapaswa kuzingatia kisichoonekana, kwa kuwa ni kipengee hasi, pamoja na kinachoonekana kwa kuwa ni kipengee chanya, tunapaswa kuelewa kuwa kwa ujumla hakuna faida kwa kiwanda au kwa ajira ya taifa kwa ujumla, madirisha yapasuke au yasipasuke.

1.14

Sasa ngoja tumfikirie James Goodfellow.                                            

1.15

Katika nadharia tete ya kwanza, ile ya dirisha lililopasuka alitumia faranga sita na kwamba hajanufaika kidogo au zaidi na dirisha moja kama ilivyokuwa mwanzo.

1.16

Katika nadharia ya pili; ambayo ajali haikutokea, angeweza kutumia faranga sita kwa ajili ya viatu vipya na angenufaika na jozi ya viatu pamoja na dirisha.

1.17

Sasa, iwapo James Goodfellow ni sehemu ya jamii, lazima tuhitimishe        kuwa, ukizingatia kazi na manufaa yake, jamii imepoteza thamani ya dirisha lililopasuka.

1.18

Tumefikia kutoka wapi, kwa kujumlisha hitimisho hili  lisilotarajiwa: “Jamii inapoteza thamani ya vitu vilivyoharibiwa bila lazima”, na kwa msemo huu, ambao utazifanya nywele za mfuasi wa sera ya kulinda viwanda nchini zikisimama nchani: kupasua, kuharibu, kutawanya sio kuunga mkono ajira ya taifa”, au kwa muhtasari zaidi: “Uharibifu hauleti faida.

1.19

Je, “Moniteur industriel”*2  atasema nini kuhusiana na hili, au wafuasi wa mheshimiwa M. de Saint – Chamans,*3  ambaye amekokotoa kwa usahihi kile ambacho kiwanda kingenufaika kutokana na kuungua kwa Paris, kwa sababu ya nyumba ambazo zingepaswa kujengwa upya?

1.20

Naomba radhi kwa kuvuruga hesabu zake za kweli, hasa kwa kuwa makusudi yake yamepitishwa kwenye sheria yetu.  Lakini ninamuomba azianze tena, aingize kile ambacho hakionekani kwenye leja kulinganisha na kile kinachoonekana.

1.21

Msomaji lazima ajitahidi kuangalia kwa makini kwamba hakuna watu wawili tu, bali watatu, katika mchezo mdogo ambao mliwasilisha.  Mmoja; James Hoodfellow, anamwakilisha mtumiaji, ambaye uharibifu umemsababishia kunufaika na kitu kimoja badala ya viwili: mwingine katika mfano wa fundi wa kutia vioo katika madirisha, unatuonyesha mzalishaji ambaye kiwanda chake kinaunga mkono ajali.  Wa tatu ni fundi wa viatu (au mtengenezaji mwingine yeyote) ambaye kiwanda chake kimekatishwa tamaa na sababu hiyohiyo.  Ni mtu wa tatu ambaye wakati wote yuko katika kivuli, na ambaye anatoa mfano wa kisichoonekana, ni sehemu ya lazima ya tatizo.  Ni yeye anayetufanya tuelewe ni upuuzi kiasi gani kupata faida kutokana na uharibifu.  Ni yeye ambaye hivi karibuni atatufundisha kuwa ni upuuzi vilevile kupata faida kwenye vikwazo katika biashara, ambayo, sio zaidi au pungufu ya uharibifu kwa sehemu. Kwa hiyo, kama utafungua chanzo cha hoja zote zilizotolewa kwa kuunga mkono hatua za mweka vipingamizi, utapata ufafanuzi tu wa istiari hiyo iliyozoeleka:  Mafundi vioo wangefanya nini kama hakuna mtu anayevunja madirisha?”

 

2.         Utawanyaji                                                                                                        

1.22

Kujitosheleza, atahakikisha kwamba kujitosheleza huko kuna thamani sawa na gharama yake.  Kwa taifa, usalama ni baraka kubwa sana. Kama  kuzipata, watu lakini moja lazima wahamasishwe, na faranga milioni mia moja zitumike, basi sina cha kusema.  Ni starehe iliyonunuliwa kwa bei ya kujitoa kafara.

1.23

Na kusiwe na kutokuelewana, kisha, kuhusiana na hoja ninayotaka  kutoa katika yale nitakayosema kuhusiana na mada hii.

1.24

Mtunga sheria anapendekeza kuruhusu watu laki moja, ambao         watawapokea walipa kodi wa faranga milioni mia moja katika kodi.

1.25

Fikiria kama tunamjibu: “Watu hawa laki moja na faranga hizi           milioni mia moja ni vya lazima sana kwa usalama wa taifa letu.  Ni kafara; lakini bila kafara hili Ufaransa ingevurugwa na kikundi kilichojitenga cha ndani au kuvamiwa kutoka nje”.  Sina kipingamizi chochote kwa hoja hii, ambayo inaweza kuwa ya uongo au kweli kwa namna itakavyokuwa, lakini ambayo kinadharia haina namna yoyote ya uasi kiuchumi.  Uasi unaanza wakati kafara lenyewe linawakilishwa kama manufaa, kwa kuwa linamletea mtu faida.

1.26

Sasa, kama sijakosea mara mwandishi wa pendekezo   atakaposhuka kwenye jukwaa, ndipo msemaji mzuri atakapoharakisha na kusema:

1.27
Waruhusu watu laki moja!  Unafikiria nini?

Kitawatokea nini?  Wataishi vipi?  Kwa kutegemea mapato yao?         lakini hufahamu kuwa kuna ukosefu wa ajira kila mahali?  Kwamba kazi zote zimezidishiwa watu.  Unataka kuwatupia katika soko ili kuongeza ushindani na kushusha viwango vya mishahara?  Katika wakati ambao ni mgumu wa kujipatia japo kipato kidogo, sio bahati kwamba nchi inawapatia riziki watu laki moja?  Fikiria zaidi kwamba jeshi linatumia mvinyo, nguo, na silaha, kwamba bado inasambaza biashara kwa viwanda na miji ya askari walinzi, na kwamba sio kitu kingine isipokuwa bahati kubwa kwa wagavi wake wengi.  Hutetemeki kwa ajili ya wazo hilo la shughuli hizi kubwa za viwanda kufikia mwisho?”

1.28

Tunaona hotuba hii,  inahitimisha kwa kuwa upande wa kuwa na askari

laki moja, sio kwa sababu ya mahitaji ya taifa kwa ajili ya huduma zinazotolewa na jeshi, bali kwa sababu za kiuchumi.  Ni kwa kuzingatia haya tu ndiyo maana napendekeza kubainisha kuwa ni kinyume.

1.29

Watu laki moja wanaowakadiria walipa kodi faranga milioni mia moja,

wanaishi vizuri na kutoa maisha mazuri kwa wagavi wao kama faranga milioni mia moja zitakavyoruhusu: Hicho ndicho kinachoonekana.

1.30

Lakini faranga milioni mia moja, zinazotoka kwenye mifuko ya walipa kodi, zinaacha kuwakimu walipa kodi hawa na wagavi wao, kwa kiwango cha faranga milioni mia moja: hicho ndicho kisichoonekana, kokotoa, piga hesabu na uniambie ni wapi pama faida kwa ajili ya umma wa watu.

1.31

Kwa upande wangu, nitakueleza mahali hasara ilipo, na kurahisisha mambo, badala ya kuzungumzia watu laki moja na faranga milioni mia moja, ngoja tuzungumzie kuhusu mtu mmoja na faranga elfu moja.

1.32

Hapa tuko katika kijiji A. waandikishaji wanazunguka na kupata mtu mmoja.  Wakusanya kodi wanafanya mizunguko yao pia na kukusanya  faranga elfu moja.  Mtu huyo pamoja na kiasi hicho cha fedha kusafirisha kwenda Metz, mmoja akiwa amelengwa kumfanya mwingine aendelee kuishi kwa mwaka mzima bila ya kufanya chochote.  Kama ukitazama tu Metz, ndiyo, uko sahihi mara mia moja; utaratibu una macho yako katika kijiji cha A, utaamua vinginevyo, kwani, labda uwe ni kipofu, utaona kuwa kijiji hiki kimepoteza kibarua na faranga elfu moja ambazo zingelipia kazi yake, na biashara ambayo kwa kutumia faranga hizi elfu moja, angemsambazia.

1.33

Kwa mara ya kwanza, inaonekana kama vile hasara inafidiwa.   Kilichotokea kijijini sasa kinatokea Metz, na ndiyo yote yaliyoko huko.  Lakini hapa ndipo hasara ilipo.  Kijijini mtu alilima na kufanya kazi: alikuwa mfanyakazi; huko Metz anazunguka “Kulia” na Kushoto!:  ni mwanajeshi.  Fedha husika na mzunguko wake ni sawa katika masuala yaote mawili:  lakini kwa moja kulikuwa na siku mia tatu za kazi inayozalisha; na kwa lingine kuna siku mia tatu za kazi isiyozalisha, katika dhana tu, bila shaka, kwamba sehemu ya jeshi sio ya lazima kwa usalama wa wananchi.  

1.34

Sasa unakuja utawanyaji.  Unanionyesha ziada ya wafanyakazi laki moja. Kuzidisha ushindani na shinikizo linalowekwa katika viwango vya mishahara.  Hicho ndicho unachokiona.      

1.35

Lakini hapa ni kile usichokiona.  Huoni kwamba kuwarudisha       nyumbani askari laki moja sio kuondokana na faranga milioni mia moja, bali kurejesha fedha hizo kwa walipa kodi.  Huoni kwamba kutupa wafanyakazi laki moja katika soko kwa namna hii ni sawasawa na kuingiza wakati huohuo faranga milioni mia moja zilizokusudiwa kulipia kazi zao; kwamba, matokeo yake, hatua hiyohiyo inayoongeza usambazaji wa wafanyakazi ndiyo pia inayoongeza mahitaji; ambapo kutokana na hapo inafuatia kwamba kushusha kwako mishahara ni njozi.  Hili ulioni kabla, na pia baadaye, katika utawanyaji kuna faranga milioni mia moja zinazolingana na watu laki moja; na kwamba tofauti yote inajumuisha haya: kwamba kabla, nchi inatoa faranga milioni mia moja kwa watu laki moja kwa kutokufanya chochote; baadaye, inawapa pesa kwa kufanya kazi.  Hatimaye, huoni kwamba mlipa kodi anapotoa pesa zake, ama kwa askari bila kubadilishana na chochote au kwa mfanyakazi kwa kubadilishana na kitu, matokeo yote yaliyopishana sana ya mzunguko wa pesa hizi ni sawa katika masuala yote mawili: katika la pili mlipa kodi anapata kitu; na katika la kwanza hapati kitu.  Matokeo: hasara kubwa kwa taifa.

1.36

Hoja potofu ambayo ninaishambulia hapa haiwezi kuhimili jaribio la matumizi yaliyoongezeka, ambalo ni kigezo cha kanuni zote za nadharia.  Kama mambo yote yakizingatiwa, ikionekana kuna faida kwa taifa katika kuongeza ukubwa wa jeshi, kwa nini wanaume wote nchini wasiitwe jeshini?

1.               Kodi     

1.37                                                                     

Umekwishawahi kumsikia mtu akisema:  kodi ni kitegauchumi kikubwa sana; ni umande unaoleta uhai.  Tazama ni familia ngapi zinazipa uhai, na fuatia kufikiria athari zake zisizo za moja kwa moja kwa viwanda, hazina kikomo, pana kama uhai, maisha yenyewe yalivyo.”

1.38
 

Ili kuipiga vita kanuni hii, ninalazimika kurudia ukanushaji           uliotangulia.  Uchumi wa kisiasa unafahamu zivuri sana kwamba hoja yake haishawishi vya kutosha mtu kuzisemea:  repetita placent; kurudia kunaridhisha.  Kwa hiyo, kama Basile, *4 uchumi wa kisiasa umepanga methali kwa ajili ya matumizi yake, akiridhika kwamba, kutoka kwenye mdomo wake, Repetita docent; kurudia kunafundisho.

1.39

Faida ambazo viongozi wa serikali wanazipata katika kuchukua mishahara yao ni kile kinachoonekana.  Manufaa ambayo yanatokea kwa ajili ya wagavi wao vilevile ni kile kinachoonekana yako mbele yako.

1.40

Lakini hasara ambayo walipa kodi wanajaribu kujitoa ni kile kisichoonekana, na tatizo linalotokana nazo kwa wafanyabiashara wanaowasambazia ni kitu cha zaidi kisichoonekana, ingawaje kinapaswa kuonekana kwa wazi kisomi.

1.41
 

Kiongozi wa serikali anapotumia kwa niaba yake sous mia moja zaidi, ina maana kwamba mlipa kodi anatumia kwa niaba yake sous mia moja pungufu.  Bali utumiaji wa kiongozi wa serikali unaonekana, kwa sababu unafanyika; wakati ule wa mlipa kodi hauonekani, kwa sababu –  lakini! Anazuiwa asifanye.

1.42

Unalinganisha taifa na kipande cha ardhi kilichochomwa moto na kodi kama mvua inayoto uhai.  Kwa hiyo na iwe hivyo.

Lakini unapaswa au jiulize mwenyewe mvua hizi zinatoka wapi, na kama

sio hasa kodi inayovuta unyevu kutoka ardhi maji haya ya thamani  

kutoka kwenye mvua kuliko kuyapoteza kwa njia ya mvukizo?

1.43

Kilicho na uhakika ni kwamba, wakati James Goodfellow anapomhesabia mkusanya kodi sous mia moja, hapati kitu chochote.  Kiongozi wa serikali naye, katika kutumia sous hizi mia moja, anazirejesha kwa James Goodfellow, ni kwa thamani inayolingana katika ngano au katika kazi.  Matokeo ya mwisho ni hasara ya faranga tano kwa James Goodfellow.

1.44

Ni kweli kabisa kwamba, mara kwa mara, karibu wakati wote kama mkipenda, kiongozi wa serikali anatoa huduma inayolingana kwa James Goodfellow.  Kwa ajili hiyo hakuna hasara kwa upande wowote;  kuna kubadilishana tu.  Kwa hiyo, hoja yangu haihusiani kwa namna yoyote na kazi yenye manufaa.  Ninasema haya:  kama unataka kuanzisha ofisi ya serikali, thibitisha manufaa yake.  Onyesha kwamba James kwa Goodfellow ni afadhali ulinganifu wa gharama yake kulingana na huduma inayomfanyia lakini licha matumizi haya halisi, usitaje, kama hoja kuunga mkono kufunguliwa – kwa ofisi mpya, faida inayompatia mrasimu, familia yake, na yule anayempatia mahitaji yake; usidai kwamba inahamasisha ajira.

1.45

James Goodfellow anapompa kiongozi wa serikali sous mia moja  kwa ajili ya huduma yenye manufaa hasa, ni sawa kabisa na anapompa fundi wa viatu sous mia moja kwa jozi ya viatu.  Ni suala la kutoa – na – kuchukua, na pointi ni sawasawa.  Lakini James Goodfellow anapomkabidhi kiongozi wa serikali sous mia moja kwa kutokupata huduma yoyote kutokana nayo au hata kupata usumbufu, ni kama ametoa pesa zake kwa mwizi.  Haifai kusema kwamba kiongozi atatumia sous mia moja hizi kwa faida kubwa sana ya kiwanda cha taifa; jinsi mwizi anavyozihitaji, ndivyo James Goodfellow ambavyo angezihitaji kama angehitaji kufikia lengo lake ama nje ya sheria au mnyonyaji wa kisheria.

1.46

Basi tujizoeshe, kutokuamua vitu kwa kuangalia tu kinachoonekana, bali kwa kuangalia kisichoonekana.

1.47

Mwaka jana nilikuwa kwenye Kamati ya Fedha, kwa kuwa katika       mkutano wenye haki na uwezo wa kubadilisha katiba wajumbe wa upinzani hawakuondolewa kiutaratibu kwenye kamati zote  katika hili watunga katiba walitenda kwa busara.  Tumemsikia M. Thiers*5 akisema: “Nimetumia muda wa maisha yangu kuwapiga vita watu wa chama halali na wa chama cha wabunge.  Kwa kuwa katika kukabiliana na hatari ya pamoja, nimekuja kuwafahamu na kuwa na mazungumzo ya ana kwa ana, ninaona sio majitu kama nilivyodhania.”

1.48

1.49

Ndiyo, uadui hutiwa chumvi na chuki kuzidishwa baina ya vyama ambavyo havishirikiani; na kama walio wengi wangewaruhusu wanachama wachache wa kundi dogo kupenya kwenye mizunguko ya kamati mbalimbali, labda ingetambuliwa katika pande zote mbili kwamba mawazo yao hayako mbali sana, na zaidi ya hayo nia zao sio kinyume, kama ilivyodhaniwa.

1.50

Hata hivyo kwa vyovyote itakavyokuwa, mwaka jana nilikuwa              kwenye Kamati ya Fedha.  Kia wakati mwenzetu mmoja alipozungumzia kupanga kwa kiwango cha wastani mishahara ya Rais wa Jamhuri, wa Mawaziri, na wa mabalozi, angeambiwa:

1.51

Kwa manufaa ya huduma, lazima tunaweza kuzizingira baadhi ya ofisi na hali ya heshima na hadhi kubwa.  Hii ndiyo namna ya kuwavuta watu wenye sifa na maarufu waende huko.  Watu wengi wasio na bahati wanamgeukia Rais wa Jamhuri, na angesikia uchungu kama wakati wote angelazimika kukataa kuwasaidia.  Kiasi fulani cha ufahari katika sebule za kiwaziri na kidiplomasia ni sehemu ya utaratibu wa serikali za kikatiba, n.k.”

1.55
 

Hoja hizi zipingwe au zisipingwe, zinastahili kuchunguzwa kwa         makini.  Msingi wake ni maslahi ya umma, ziwe zimekadiriwa kwa usahihi au kinakosa; na, binafsi, mtajenga zaidi hoja kwao kuliko Catos wetu wengi, wanaoongozwa na msimamo finyu wa ubahili na wivu.

1.56

Lakini kinachoshtua ufahamu wa wachumi wangu, kinachofanya       nifadhaishwe na umashuhuri wa kisomi wa nchi yangu, ni wanapotoka kwenye hoja hizi (kwa kuwa kamwe hawashindwi kufanya hivyo) kwenda kwenye jambo hili lisilofurahisha (wakati wote kupokelewa vizuri).

1.57

“Aidha, ufahari wa viongozi wakuu wa serikali unahimiza sanaa,        viwanda, na ajira.  Mkuu wa Nchi na mawaziri wake hawawezi kuandaa dhifa na tafrija bila ya kuingiza uhai kwenye vena za mwili wa kisiasa.  Kupunguza mishahara yao kutakuwa kudhoofisha viwanda huko Paris na, wakati huohuo, katika taifa zima”.

1.58

Tafadhali, waungwana, angalau mheshimu sayansi ya hesabu na msije mbele ya Bunge la Ufaransa na kusema, kwa hofu kwamba, kwa aibu yake, halitakusaidia, kwamba ongezeko huleta hesabu tofauti liwe linaongezwa kutoka juu kwenda chini au kutoka chini kwenda juu.

1.59

1.60

Vema, sasa fikiria ninapanga na kibarua anichimbie mtaro                 shambani kwangu kwa kiasi cha sous mia moja.  Ninapokaribia tu kufikia makubaliano naye, mkusanya kodi anachukua sous zangu mia moja na kupeleka kwa Waziri wa mambo ya Ndani.  Mkataba wangu unavunjika, lakini Waziri ataongeza chakula kingine kwenye mlo wake wa usiku.  Ni kwa msingi gani unathubutu kuthibitisha kuwa matumizi ya kiongozi huyu ni nyongeza kwa kiwanda cha taifa?  Huo ni kwamba huo ni uhamisho tu wa matumizi na kazi?  Waziri ameandaliwa meza yake kwa vitu tele, ni kweli; lakini shamba la mkulima limekaushwa, huu ni ukweli; Mwandaaji chakula wa Paris amepata sous mia moja, lakini mchimba mtaro amepoteza faranga tano.  Tunachoweza kusema ni kwamba chakula cha kiongozi na mwandaaji chakula aliyeridhika ni kinachoonekana; shamba lililojaa maji na mchimbaji ambaye hakuchimba ni kisichoonekana.  

1.61

Mungu! Wangu!  Ni usumbufu mkubwa kiasi gani kuthibitisha katika uchumi wa siasa kwamba mbili jumlisha mbili ni nne; na kama ukifanikiwa kufanya hivyo, watu wanalia, “Ni wazi kwamba inaudhi.” Kisha wanapiga kura kana kwamba hujawahi kuthibitisha chochote kabisa.

2.      Tamthilia na Sanaa

1.62

Serikali inapaswa kutoa ruzuku kwa sanaa?                                    

1.63
Hakika, kuna jambo kubwa la kusema kuhusiana na ubaya na uzuri wa mada hii.

1.64

Katika kuunga mkono mfumo wa ruzuku, inawezekana kusema         kwamba sanaa inakua, inaongezeka, na kuimbia ushairi roho ya taifa; ambayo wanachukua kutoka shughulikia vitu, kuipa husia za uzuri, na hivyo kuathiri tabia zake, mila zake, maadili yake, na hata viwanda vyake.  Mtu anaweza kujiuliza muziki ungekuwa wapi huko Ufaransa bila ya Théâtre – Italien na Chuo cha Muziki; sanaa ya drama bila ya Théâtre-Français; uchoraji na sanaa ya uchongaji bila ya vitu vyetu tunavyokusanya au makumbusho yetu.  Mwingine anaweza kwenda mbele zaidi kuuliza kama, bila ya mfumo wa uwekaji mamlaka makao makuu na hatimaye utoaji wa ruzuku kwa sanaa, kungeweza kuanzishwa kwa ustaarabu huo bora wa kazi za Kifaransa na kupeleka bidhaa zake duniani kote.  Yakiwemo matokeo hayo haitakuwa kilele cha ujinga kukataa tathmini hii ya wastani kuhusu raia wote, ambayo katika uchambuzi wa mwisho, ndiyo yaliyowaletea sifa kubwa na heshima katika macho ya Ulaya?

1.65

Kwa sababu hizi na nyinginezo, ambazo sipingi uwezo wake wa          kupinga hoja nzito na kubalifu.  Kwanza kabisa, na inawezekana kusema kuwa, kuna suala la haki katika kugawa.  Je haki ya mbunge inafikia kumruhusu kuchukua mishahara ya fundi mchundo ili kujaliza faida ya msanii?

1.66

M. de Lamartine*6 alisema: “kama ukiondoa ruzuku ya sanaa za maonyesho, ni wapi utakaposimama katika njia hii, na hutahitajika kimantiki kufuta vitivo vyako vya chuo kikuu, makumbusho yako, taasisi zako, maktaba zako?” Ingewezekana kujibu:  kama unataka kutoa ruzuku kwa kila kilicho kizuri na chenye manufaa, utasimama wapi katika njia hio, je hutahitajika kimantiki kutengeneza orodha ya raia kwa ajili ya kilimo, viwanda, biashara, ustawi na elimu?  Zaidi ya hayo, ni hakika kwamba ruzuku husaidia maendeleo ya sanaa? Ni suala ambalo ni gumu kutafutwa ufumbuzi, na tunaona kwa macho yetu wenyewe kwamba sanaa za maonyesho zinazostawi ni zile ambazo zinategemea faida zake.  Mwishoni, katika kuendelea kuzingatia zaidi, unaweza ukaona kwamba mahitaji na matarajio vinaanzishana na kuendelea kupanda mikoani na kupunguzwa **3 zaidi na zaidi katika uwiano kwa kuwa, chochote kitakachokuwa sasa utajiri wa taifa, hakiwezi kuchochea viwanda vya kifahari kwa kodi bila ya kuleta madhara kwa viwanda muhimu, ya ustaarabu.  Mtu anaweza vilevile kusema kwamba kutenguliwa huku bandia kwa mahitaji, ustaarabu, kazi na watu kunayaweza mataifa katika hali ya mashaka na hatari, na kuyaacha bila ya msingi imara.

1.67

Hizi ni baadhi ya sababu zinazodaiwa na washindani wa afua ya nchi  kuhusu utaratibu ambao raia wanaamini utatosheleza mahitaji na matarajio yao, na hivyo kuelekeza shughuli yao.  Ninakiri kwamba mimi ni mmojawapo wa wale wanaofikiri kwamba chaguo, shauku, vinapaswa kutoka chini, na sio juu, kutoka kwa wananchi na sio kwa wabunge; na nadharia iliyo kinyume ninaona inaelekea katika kupotea kwa uhuru na utu wa mtu.

RELATED ARTICLES