Hernando de Soto’s, “Bringing Capitalism to the Masses” in Swahili

UJUMBE WA KILA MIEZI

MITATU KUHUSU UHURU Cato

 

Kuleta Upebari kwa Umma

Hernando de Soto

 

Watu
walioanzisha utafiti wa kitaaluma huko Peru kuhusu kwa nini mambo
hayakwenda vizuri baada ya miaka 12 ya serikali ya kijeshi ya siasa za
mrengo wa kushoto walikuwa Rose na Milton Friedman, ambao walikuwa
wageni wangu wa kwanza mwaka 1979.

 

Moja ya mambo ambayo Milton alitufundisha alipokuwa Lima ni kwamba hakukuwepo na chakula cha mchana cha bure.  Ambacho hakusema ni kwamba kulikuwa na vitabu vya bure.  Miaka mitano takriban baada ya ziara yao, Milton na Rose walinitumia kitabu, kilichoitwa The Tyranny of the Status Quo.  Kitabu
hicho kilinivutia sana, kwa sababu kwa wakati ule taasisi yetu ilikuwa
imeandaa mamia ya wachuuzi wa mitaani na ilikuwa ikitafuta njia za
kuanzisha sera za kisiasa ambazo zingewarahisisha kupata riziki.

 

The Tyranny of the Status Quo kilihusu
– miaka michache ya baada ya serikali ya Reagan – jinsi ilivyo vigumu
kuvunja Pembe Tatu ya Chuma ya wafadhiliwa, wanasiasa, na warasimu,
ambayo inalinda hali kama ilivyo na kupinga mabadiliko yanayohitajika.

 

Sisi
katika Taasisi ya Uhuru na Demokrasia tuligundua kwamba kuna jimbo
kubwa sana la uchaguzi kwa ajili ya mabadiliko katika nchi
zinazoendelea.  Ingawa ziliitwa “maskini”, lakini tulielewa kwamba hao maskini wasingekuwepo kama wasingekuwa pia wajasiriamali.

 

 

Picha

 Na  wakati
watu, kama Fareed alivyobainisha, walisema kwamba watu bilioni moja
waliishi kwa dola moja kwa siku na labda watu bilioni tatu waliishi kwa
$ 2 au $ 3 kwa siku, hakuna aliyesema kwamba kuna watu bilioni nne
ambao ni maskini, ambao ni wajasiriamali, na ambao wameondolewa kabisa
kwenye uchumi wa dunia na hata katika uchumi wa taifa, kwa kutokuwepo
na sheria.

 

“Nchi Maskini zinahitaji aina ya ufumbuzi ambao ulifuatwa na Nchi zilizoendelea katika karne ya 19, sio karne ya 21.”

 

 

 

Picha

 

Sio vijiji vya miaka ya 1960 tena katika Dunia ya Tatu.  Idadi ya watu wa Portau – Prince ni mara 17 ya ile ya miaka 35 iliyopita.  Idadi ya watu wa Miji ya Algeria – ni mara 15 ya ilivyokuwa.  Miji ya Equador mara 11.  Na nchi ambazo zilikuwa vijijini kabisa tulipoanza kazi yetu sasa hivi ni miji.  Hao watu wamekuwa wafanyabishara kutokana na mgawanyo wa kazi zilizopo mijini.

www.cato.org

 

KUANZA KWA MIJI

Nchi maskini zinahitaji aina ya ufumbuzi ambao nchi zilizoendelea zilifuata katika karne ya 19, sio karne ya 21.  Kilichotokea Magharibi katika karne ya 19 sasa kinatokea katika nchi zinazoendelea.  “Oliver
Twist” amekuja mjini, lakini yeye na rafiki zake bado hawajatambuliwa
na taasisi za fedha za kimataifa au na programu nyingi za pamoja za
nchi zilizoendelea.  Mbaya zaidi, hajatambuliwa bado na
watu walio wengi wa nchi zinazoendelea wanaodhani kwamba wachuuzi wa
mtaani ni tatizo, kwamba utengenezaji haramu wa bidhaa unaleta bidhaa
zenye kasoro.

 

Jinsi
watu wanavyofahamu hali halisi katika nchi zinazoendelea, ambako kuna
watu bilioni tano miongoni mwa watu bilioni sita wa dunia nzima, ndivyo
wanasiasa watagundua kwamba jimbo lao kubwa sana la uchaguzi kwa ajili
ya mabadiliko ni wafanyabiashara maskini.

 

UTAJIRI WA MATAIFA

Nchi yangu, Peru, ilikuwa na rais aliyekuwa na asili ya Kijapani kwa muda wa miaka 10.  Jina lake alikuwa Alberto Fujimori.  Fujimori ilikuwa moja ya familia ambazo zilitoka Japani kwenda Peru na Brazil miaka ya 1930 na 1940.

 

Sasa, ukweli kwamba Fujimori walikwenda Peru na Yoshiyama Brazil si muhimu.  Swali muhimu zaidi ni: Kwa nini Watoledo na Walula hawakwenda Japan?  Hawakwenda
Japan kwa sababu Peru katika mwaka 1940 ilikuwa na asilimia 25 ya Jumla
ya pato la Taifa (GNP) kwa kila mtu zaidi ya Japan, na Brazil ilikuwa
na asilimia 50 zaidi ya hiyo.  Ni wazi, Japan ilifanya kitu katika miaka 50 iliyopita kilichofanya iwe tajiri sana mara 10 zaidi ya Peru.  Kulitokea nini?

 

Baada ya Vita Kuu vya Pili ya Dunia, mpango ulitekelezwa ambao ulianzia Honolulu mwaka 1942, chini ya usimamizi wa MacArthur.  Kama
Mao zedong nchini China, kimsingi Waamerika waliharibu mfumo wa
kikabaila nchini Japan, ambao walidhani ndio uliokuwa chanzo cha
matatizo ya upanuzi wa Japan huko Asia.  Lakini tofauti na China baada ya vita, walianzisha msingi wa mfumo wa miliki binafsi ulioenea kote.

Kwa
kuuangusha mfumo wa kikabaila na kuunda jimbo kubwa la uchaguzi kwa
uchumi wa soko, waliigeuza Japan, pamoja na makoloni yake mawili,
Taiwan na Korea ya Kusini.  Mnamo mwaka 1978, Deng Xiaoping aligeuka na kusema, “Unajua, sijali paka ana rangi gani mradi awe anakamata panya”.  Na sasa ukubwa wa Asia unageuka kwa njia ya milki.

 

 

 


Tuma

barua ya Cato

kwa Rafiki

Kutoa
zawadi ya mchango wa bure kwa marafiki ambao watafurahia kupata Barua
ya Cato, tafadhali jaza fomu iliyoambatanishwa au orodha ya watu
(orodha ya kadi za likizo, n.k.) kwenye bahasha.  Au tembelea www.cato.org na bofya kwenye “subscriptions”

 

AJABU YA ADOLF BUSCH

Kupitia
sera ya nje kabla, Amerika imegeuza nchi mbalimbali na kubadilisha
uchumi wa kikabaila na wa urithi kuwa uchumi wa kisasa.  Lakini inaonekana kuna tabia ya kusahau vitu hivyo.  Ni
rahisi sana kwa Dunia ya Tatu kuelewa mambo ninayozungumza kuliko
ilivyo kwa Dunia ya kwanza, kwa kuwa watu wa Dunia ya kwanza
wanachukulia mambo kikawaida.

 

Karl Popper alizoea kuiita ajabu hiyo, ajabu ya Adolf Busch.  Siku moja Popper na rafiki yake walikwenda kumsikiliza Busch akitafsiri Vivaldi huko Zurich.  Alipokwenda kutoka mtungo wa tatu kwenda kwa nne, alifanya vizuri sana, kwa namna ambayo hakuna aliyewahi kusikia.  Hivyo
baadaye walimtembelea chumbani mwake na kuuliza, Bingwa wa muziki,
uliwezaje kuhama kutoka kwenye mtungo wa tatu kwenda mtungo wa nne?”  Na Adolf Busch alisema, “Vizuri, ni rahisi tu”.  Aliweka fidla shingoni mwake na kuanza kupiga, na hakuweza kamwe kulipiga tena.

 

KUONGEA NA WASIOHUSIKA

Ninakumbuka mwaka 1988 niliombwa kutoa hotuba katika Jukwaa la Wazi la Katibu wa Nchi.  Mada ilikuwa “Marekani:  kwa nini ninadhani unaongea na Wasiohusika”.  Kwa
maneno mengine Wamarekani walio wengi wanaongea na Watu wa Dunia ya
Tatu walioingizwa kwenye utamaduni wa Magharibi kama mimi.  Lakini wengi wetu tuna maslahi.  Sisi sio mabepari hasa tunaofanya ushindani, ni wafanyabiashara tunaotafuta fursa.  Wale wenye raghaba hasa ndio wajasiriamali halisi lakini ni maskini na wachache na hujafanya mawasiliano nao.

 

Huko
Mexico, kwa mfano, ambako tunafanya kazi na Rais Fox, tumegundua kuwa
takriban asilimia 80 ya watu wa Mexico wako katika uchumi wa nje ya
sheria.  Wanamiliki karibu biashara milioni 6, hekta za ardhi milioni 134, majengo milioni 11.  Na
vyote kwa ujumla vina thamani ya $ milioni 315, ambayo ni mara 7 ya
thamani ya akiba ya mafuta ya Mexico na mara 29 ya thamani ya vitega
uchumi vyote vya nje vya moja kwa moja tangu Spanyola ilipoondoka.

Kwa maneno mengine, uchumi wa kabla ya ubepari, kwa maelekezo ya ubepari, unatokea duniani kote.  Huko Misri, watu maskini wanamiliki nje ya sheria asilimia 92 ya biashara zote, ambavyo vina thamani ya $ 248 bilioni.  Hivyo
ni sawa na mara 55 ya thamani ya vitegauchumi vyote vya nje vya moja
kwa moja nchini Misri tangu Napoleon alipoondoka, ikiwa ni pamoja na
mfereji wa Suez na Bwawa la Aswan na mara 70 ya misaada yote ya
ushirikiano ambayo walipokea.

 

Kwa maneno mengine, raslimali zetu zilizo nyingi hazitoki kwenu Magharibi.  Bila
shaka, nyinyi ni wakarimu sana na tunapokea kile mnachotupatia, lakini
ukweli ni sawa na tone kwenye ndoo kikilinganishwa na kile tulichonacho
tayari.  Utajiri halisi hukua kutokana na jitihada za
wajasiriamali ambao wanaweza kukusanya raslimali pamoja na kufanya kazi
kwa ufanisi ili kuongeza tija.

 

UMUHIMU WA HAKI MILIKI

Pia
tumeitwa sehemu mbalimbali, kama Ghana. Na cha kushangaza sana ni
kwamba, sio tu na Rais Kufuor, bali pia na machifu wa kikabila.  Walisoma maandishi yetu na kusema: “Hatutaki tena mamlaka; tunataka haki miliki.  Mamlaka ni kitu ambacho watu wote wanakikiuka.  Haki
miliki ni imara zaidi, kwa kuwa msingi wake ni maafikiano ya jamii
yanayotokana na makubaliano ya raghaba ya mtu mmoja kwa mwingine, sio
taifa moja kwa lingine.

 

Kama ukiitazama ramani ya Ulaya kwa muda sasa utaona kwamba mamlaka sio imara sana.  Bado
ukitazama Alsace – Lorraine, jimbo ambalo limekuwa likigawanywa kila
siku baina ya Wafaransa na Wajerumani, utaona kwamba, hata limilikiwe
na nani, Monsieiur du Pont bado anaishi alikokuwa akiishi siku zote, na
Herr Schmidt anaishi alikokuwa akiishi siku zote.  Hakimiliki ni matokeo ya maafikiano ya wananchi, na zinadumu hata mamlaka kama yameguke.

 

MILIKI NA UTAWALA WA SHERIA

Hivyo,
tunajaribu kuonyesha kuwa unaweza kuvunja pembetatu ya chuma kwa
kuwaonyesha viongozi wa siasa kwamba wana eneo kubwa sana la kubadilika
kuelekea uchumi wa soko.  Uchumi wa soko ni ujenzi wa
kisheria nao sio vitu vyote vinavyooonekana – barabara, madaraja,
viwanja vya ndege, na bandari – ambao watu wa Magharibi wanataka kuwapa.

Acha

Urithi wa

Uhuru

Je, unahusika na mustakabali wa uhuru nchini Marekani?  Kuendelea
kuwa na urithi wa kudumu wa uhuru, fikiria kuiingiza Cato kwenye wosia
wako au kuacha amana au kumteua Cato kuwa mfadhiliwa katika bima yako
ya maisha au mapato ya mpango wa kustaafu.  Wasiliana na Terry Kibbe katika ofisi yetu ya (202) 218 – 4614 kwa maelezo zaidi kuhusu zawadi kwa Cato.

 

Kama wewe ni maskini, na ulichonacho tu ni kipande cha ardhi na  ndipo unapofanyia kazi, uwe unachuuza barabarani au kumkamua ng’ombe, hakuna kitu kilicho na thamani kwako kama miliki yako.  Lakini
kutunza bila ya sheria unahitaji kuwaridhisha machifu wa kikabila,
askari wasio waaminifu, wanasiasa walarushwa, majaji wabaya, majirani
zako wagumu, na hata magaidi.

 

Lakini
kama sheria ikija na kusema haki hizo sasa zinatambuliwa, sio tu na
majirani, bali na polisi na taifa zima, sasa unaweza hata kuzifanyia
biashara kitaifa na kimataifa na sheria itakulinda, kisha watu
wanapendezewa na utawala wa sheria.

 

Karibuni watauliza, itakuwaje kama watakuwa na mgogoro na kwenda mahakamani?  Kisha, wanataka mfumo mzuri wa sheria.  Na hatimaye watatambua kuwa sheria zinaweza kubadilishwa, kwa hiyo watauliza, nani anatunga sheria?  Na watajali mchakato wa kisiasa.

 

Kwa
hiyo, chanzo cha utawala wa sheria ambao utaruhusu taifa la sasa kukua
na hivyo kuleta amani, utulivu, na ustawi duniani – ni haki miliki.  Na utawala wa sheria utaleta ustawi.

 

MGAWANYO WA KAZI

Adam Smith na baadaye Marx wangesema kuwa tija mpya katika Ulaya ilisaidiwa na mgawanyo wa kazi.  Mfano wa Smith ulikuwa rahisi sana.  Alisema aliona watu kadhaa wakifanya kazi nje ya ukumbi wa Glasgow, wakitengeneza pini.  Wakichukua hatua 18, waliweza kutengeneza sio zaidi ya pini 20 kila siku.  Lakini mahali pengine aliwaona watu 10 wakigawana kazi hizo 18 miongoni mwao wenyewe.  Mtu
mmoja alinunua waya, mwingine akaufunika na bati, na wa tatu aliuvuta
waya, watu wengine wawili walikata waya, na mtu mwingine aliweka alama
kwenye waya, mwingine aliuelekeza, na walitengeneza pini 48,000 kwa
siku.

 

Lakini kama ukienda kwenye nchi zinazoendelea utaona kwamba huna makampuni, kwa sababu sheria haijafika huko.  Walichonacho tu ni familia.  Na familia zina matatizo hata kuwaweka watu 10 kazini.  Zinaweza kuwaweka 4 tu.  Na hao 4, ni kaka yako mvivu na shemeji yako mlevi:  watu ambao hawawezi kutengeneza pini.  Yeyote ambaye ni meneja anafahamu kuwa unavyochanganya raslimali na nani unayemwajiri kufanya kazi ni muhimu sana.

 

Zaidi
ya watu bilioni nne hawana haki miliki juu ya raslimali zao hivyo
hawawezi kupata mikopo na pia hawawezi kufungua kampuni ambayo wanaweza
kugawa kazi.  Maana yake ni kwamba wanaweza kupanga nyenzo kwa ufanisi au kusimamia upataji wa matokeo.   Hawawezi

 

TUZO

YA

MILTON FRIEDMAN

KWA

UHURU

UNAOENDELEA

 

Kutenganisha raslimali za wadau kutokana na mali za wawia na wafanyakazi.

 

Kwa
kuwa na watu wachache waliojiunga vibaya pamoja katika shughuli moja,
hata uwape mikopo midogo kiasi gani, hawatakaa wawe na ufanisi na hivyo
kamwe hawataweza – kushindana katika soko la dunia.  Thamani sio tu watumishi bali pia uwezo wa mtu wa kugawa kazi.  Pamoja
na kwamba Adamu Smith alikuwa mtu mkubwa, watu wenye fikra za kupenda
mabadiliko walituachia urithi kwamba tutapaswa kuondokana na nadharia
ya kazi ya thamani.  Thamani haiji tu kutokana na kazi nyepesi nyepesi.  Inatokana na ufumbuzi wa kisomi wa kisiasa na kiuchumi ambao unaweza kuongeza tija kwa kiasi kikubwa.


 

                    Picha

 

TAASISI YA CATO

 

 

 

 

 

 

 


“Haki za mali ni matokeo ya mikataba ya umma na hushikilia hata mamlaka yanapovunjika vipande vipande”.

 

 

NGUVU YA UHURU

Ili
kujenga mataifa ya kisasa, tunapaswa kujifunza jinsi maskini
wanavyofanya kazi na kisha kutengeneza sheria zinazokidhi mahitaji yao.  Mwishoni, Waperu, Wachina, na Waamerika wanataka kimsingi vitu hivyohivyo: maisha, uhuru na mali.  Na ili kuvipata, unapaswa kujenga uchumi wa soko unaozingatia utawala wa sheria.  Maadui wetu hasa sio Marx na wengine bali ni watu wasioamini katika uwezo wa binadamu aliyekombolewa na utawala wa sheria.

 

Maadui wa utaalamu wetu ni watu waliopendelea sheria za ubunifu ambao walikuwa aina ya wazalendo  wasiojua kuzungumza kuhusu ustaarabu – katika umoja, ambao wakati wote wanaamini aina nyingi za ustaarabu kwa wakati huohuo.  Kwa kuwa ni wazalendo wanaopendelea sheria za ubunifu, waliwaondoa watu kutoka kwenye sheria ya wote ya maendeleo.  Ni
watu kama Samuel Huntington, ambaye ni mtu mwenye siasa akilinganishwa
na wenzetu waliopendelea sheria za ubunifu, wanaoamini kwamba hatuwezi
kufuata mfano wako kwa kuwa Max Weber aliwashawishi kuwa ni mtindo wa
lugha ya Saksoni.

 

Kwa
hiyo, niko hapa Cato, nikijivunia kuwa mgeni wa kwanza kutoka nje
kupokea tuzo yenu, nikizungukwa na wenzangu Walatino na kutambuliwa na
aliyekuwa raia wa India.  Hakika, mko njiani kuelekea kwenye taaluma kwa sababu mnaamini katika uwezo wa watu wote duniani.  Kwa hiyo ninaona fahari kupata tuzo hii kutoka Cato, iliyopewa jina la Great Milton Friedman.  Na ninanyenyekea kwa heshima niliyotunukiwa, ambayo inadhihirisha kazi za wenzangu.

 

RELATED ARTICLES