John Stuart Mill’s , “On Liberty”

KUHUSU UHURU WA KUJIAMULIA 1959 – John Stuart MilI, Mkusanyiko wa Kazi za John Stuart Mill, Juzuu ya XVIII, Insha kuhusu Siasa na Jamii Sehemu ya I [1832]

 

MUHTASARI WA MHARIRI

Toleo la 4:  Longmans, Green, Reader and Dyer, 1869.  Kimechapishwa tena kutokana na toleo la 3 London:  Longman, Green Longman, Roberts and Green, 1864; toleo la 2 London: Parker, 1859 na toleo la kwanza, London: Parker 1859. Kimebainishwa katika bibiografia ya JSM kama “On Liberty” juzuu ndogo baada ya juzuu ya 8 iliyochapishwa katika mwezi wa Februari, 1859 (MacMinn, 92). Kwa maelezo ya vijenzi vya On Liberty na masuala yanayohusiana, tazama matini ya Utangulizi, Ixxviii – Ixxxiii hapo juu.

 

Matini hapa chini, ambayo ni ya toleo la 4 (la mwisho katika maisha ya JSM) yamelinganishwa na yale ya toleo la 3,2, la 1 na Matoleo ya Umma.  Katika tanbihi, mibadala katika toleo la 3 kinaoneshwa kwa “64” toleo la 2 kwa “592” na toleo la kwanza kwa “591”.  Vibadala halisi kati ya toleo la umma na toleo la 4 vimetolewa katika Kiambatisho cha D.

 

“Kanuni kuu inayoongoza”, ambayo kwayo kila hoja imewekwa wazi katika kurasa hizi, zinakutana moja kwa moja ni umuhimu thabiti na ulio bora wa maendeleo ya binadamu katika uanuwai wake wa hali ya juu.”

 

Wilhelm von Humboldt, Sphere and Duties of Government.

 

[Mfasiri: Joseph Coulthard (London: Chapman, 1854) uk. wa 65]

 

Kwa kumbukumbu muhimu na zinazosikitisha za yeye aliyekuwa mvuto, na kwa sehemu mwandishi wa yote yaliyo bora katika maandishi yangu – rafiki na mke ambaye hisia zake za ukweli uliotukuka na haki alikuwa mshawishi wangu imara ambaye kukubali kwake kulikuwa tunu kuu kwangu.  Namtunukia juzuu hii.  Kama ilivyo kwa kazi zangu zote nilizoandika kwa miaka mingi, kazi hii ni yake kama ilivyo yangu, lakini kazi yenyewe kama ilivyo, ilikuwa na kiwango kidogo kisichotosheleza,  manufaa yasiyokadirika ya masahihisho, baadhi ya sehemu zake muhimu kabisa zikiwa zimebakizwa kwa ajili ya upimaji  tena wa uangalifu zaidi ambao katu hawatarajii kuupata.  Kama ningeliweza kuifasilia dunia nusu ya mawazo na hisia zake kuu, zilizozikwa naye kaburini, ningekuwa ni njia ya mafanikio makubwa kuliko inavyoweza kutokea katika kitu chochote ninachoweza kukiandika bila ya kuongozwa na bila ya kusaidiwa na busara zake zisizo na kifani.

 

SURA YA 1

 

Utangulizi

 

Mada ya insha hii sio kile kinachoitwa Uhuru wa Utashi ambao kwa bahati mbaya unapingana na Kanuni isiyoitwa kwa jina lake la umuhimu wa kifilosofia bali uhuru wa kujiamulia mambo ya Kiraia na kijamii: hali na ukomo wa nguvu ambayo inaweza kutumiwa kisheria na jamii juu ya mtu binafsi.  Hoja inayotamkwa mara chache na ambayo ni nadra kujadiliwa kwa ujumla lakini ambayo huathiri sana mabishano ya kiutendaji ya kizazi hiki kwa uwepo wake wa ufiche, na hivi karibuni kuna uwezekano wa kujitambulisha kama hoja muhimu sana kwa siku zijazo uko mbali sana katika kwenye upya, kiasi kwamba kwa namna fulani imemgawa binadamu kutoka vizazi vya kale huko nyuma; lakini katika hatua ya maendeleo ambamo kwamo sehemu zilizostaarabika za spishi zilizoendelea zaidi hivi sasa zimeingia, zinajitokeza zikiwa kwenye mazingira mapya, na huhitaji ushughulikiaji tofauti na ulio muhimu sana.

 

Mapambano kati ya Uhuru wa Kujiamulia na Mamlaka ni hali isiyoonekana waziwazi kabisa katika sehemu za historia ambazo tunazifahamu mapema zaidi, hususani katika Ugiriki, Roma na Uingereza.  Lakini siku za zamani, mjadala huu ulikuwa kati ya masomo au baadhi ya matawi ya masomo na aSerikalia.  Kwa neno Uhuru wa Kujiamulia ilimaanishwa ulinzi dhidi ya udhalimu wa watawala wa kisiasa. Watawala walidhaniwa (isipokuwa kwenye baadhi ya serikali pendwa za Ugiriki) kama nafasi yenye umuhimu wa uhasama kwa watu waliowatawala,  walitokana na tabaka tawala au kabisa linalotawala waliopata Mamlaka yao kutokana na urithi au ushindi ambao katika matukio yote hawakushikilia mamlaka ya ridhaa ya waliowatawala na wenye watu wenye mamlaka ya juu kabisa hawakuthubutu, labda hawakutamani, kushindana na hadhari zozote zile ambazo zingechukuliwa dhidi ya matendo yao ya kiugandamizaji.  Madaraka yao yalionekana kuwa ni ya lazima, lakini pia ya hatari ya hali ya juu, kama silaha ambayo wangeweza kujaribu kuitumia dhidi ya adui zao wa nje.  Kuwazuia wanajamii walio dhaifu zaidi dhidi ya kufanywa mawindo na viumbe wakali wasio na idadi, palihitajika kuwapo na mnyama aliye mkali au mwenye nguvu zaidi kuliko wengine wote walioagizwa kuwagandamiza.  Lakini kama mfalme wa tai asiyekuwa na tofauti katika kuwinda kundi la wanyama kuliko kulalamalalama, ilikuwa lazima awe katika mkabala wa lazima wa ulinzi dhidi ya mdomo na kucha zake.  Hivyo, lengo la wazalendo lilikuwa kuweka ukomo kwa mamlaka ambayo utawala ungelazimika kuyatumia  kwa jamii; na ukomo huu ndicho walichomaanisha kwa jina uhuru wa kujiamulia mambo.  Jambo hili lilijaribiwa kwa namna mbili: Kwanza kwa kupata kutambuliwa kwa kinga fulanifulani, zinazoitwa uhuru wa kisiasa au uhuru wa kujiamuliwa mambo, ambao ulikuwa uchukuliwe kama ukiukaji wa kazi mtawala kunako halifu na ambako, kama atahalifu, ukinzani mahsusi au maasi ya jumla yangekuwa halali.  Njia ya pili, na aula ya kwa jumla ilifaa baadaye, ilikuwa uanzishwaji wa uhakiki wa kikatiba, ambao ridhaa ya jamii au chombo cha aina fulani kinachotazamiwa kuwakilisha maslahi yake kilifanywa kuwa ni shuruti la lazima kwa baadhi ya vitendo muhimu zaidi ya mamlaka ya utawala.  Kwa hoja ya kwanza ya aina hizi za ukomo mamlaka za utawala katika nchi nyingi za ulaya zililazimishwa sana au kiasi kukubali.  Haikuwa hivyo kwa njia ya pili, na ili kufanikisha hivi au iwapo kwa kiwango fulani imekwishapatikana, kupata kikamilifu yanakuwa madhumuni makuu ya wapenda utumwa kujiamini kila mahali.  Na kwa kuwa binadamu waliridhika na kupambana na adui mmoja kwa mwingine na kutawaliwa na Bwana kwa masharti ya kuhakikishiwa matokeo yanayotakiwa dhidi ya mdhalimu wake, hawakuyachukua matarajio yao mbali zaidi ya hoja hii.

 

Hata hivyo, katika maendeleo ya binadamu, ukaja wakati, ambapo binadamu aliacha kufikiri  umuhimu wa asili kwamba watawala wao wawe na mamlaka huru, yanayokinzana na maslahi yao wenyewe.  Kwao ilielekea kuwa vizuri zaidi kwamba mahakimu mbalimbali wa Dola wawe wapangaji au wajumbe wao wakiwabadilisha jinsi wanavyopenda.  Katika njia hiyo peke yake, ndiyo wangekuwa na usalama kamili ambapo mamlaka za serikali zisingetumiwa vibaya kwa hesabu yao.  Kwa kiwango fulani, mahitaji haya mapya ya watawala wa kuchaguliwa na wa muda, lilikuwa lengo dhahiri la ugandamizaji la chama kinachopendwa kila wakati ambapo chama cha aina hiyo kilikuwepo na kwa kiasi kikubwa kilizidi juhudi za awali za kudhibiti mamlaka ya watawala.  Kadri mapambano yalivyoendelea kufanya  mamlaka yanayotawala yanatokana na  uteuzi wa vipindi wa watawaliwa, ndiyo baadhi ya watu walivyoanza kufikiri kwamba umuhimu uliokithiri uliwekwa kwenye ukomo wa mamlaka yenyewe.  Hiyo (inaweza kuwa) ili kuwa raslimali dhidi ya watawala ambao kitabia maslahi yao yalitofautiana na yale ya watu.  Hivi sasa kilichotakiwa kilikuwa kwamba watawala wafanane na watu wao.  Kwamba maslahi na utashi wao viwe ni utashi na maslahi – dhamira ya Taifa kwa jumla. Taifa halikuhitaji kulindwa dhidi ya utashi wake wenyewe. Halikuwa na woga na kujidhalimu lenyewe.  Waache viongozi wawajibike kwa Taifa, waliweza kuondolewa mara moja na lingeweza kuwaamini kwa mamlaka ambayo lenyewe lingeweza kutamka matumizi yake yaliyopaswa kufanywa.  Mamlaka yalikuwa ni mamlaka ya taifa lenyewe, yaliyowekwa mahali  pamoja na aina inayofaa kwa utendaji.  Aina hii ya fikra, au labda hisia ilikuwa ya kawaida miongoni mwa vizazi vilivyopita vya wapenda mabadiliko wa Ulaya, katika sehemu ya Bara ambayo kwayo dhahiri inatawala.  Wale wanaokubali ukomo wowote ule wa kile ambacho serikali inaweza kukifanya isipokuwa katika serikali zile ambazo wanafikiri hazipaswi kuwepo licha ya kuachilia mbali watu wenye fikra nyingi za kisiasa wa Bara hili.  Sauti za aina hiyo hiyo za maono, kwa wakati huu zingekuwa zimeenea nchini mwetu iwapo mazingira ambayo yalitia moyo kwa wakati fulani yangeendelea bila ya kubadilika.

 

Lakini, katika nadharia za kisiasa na kifalsafa, pamoja na katika watu, ufanisi huweka bayana makosa na udhaifu ambao kutofanikiwa kungeweza kuficha kutokana na kugunduliwa.  Dhana kwamba watu hawana haja ya kuweka ukomo wa mamlaka yao yajuu yao, inaweza kuonekana kuwa dhahiri bila ya uthibitisho, ambapo serikali inayopendwa ilikuwa jambo la kuotwa tu, au la kusomwa kwamba liliwahi kuwepo nyakati za zamani.  Pia, si lazima kwamba dhana hiyo ilighasiwa na mihengeuko ya muda mfupi kama vile Mapinduzi ya Ufaransa, Ulaya zaidi ikiwa kazi ya wanyang’anyi wachache na ambayo kwa vyovyote vile haikuwa ya utendaji kazi wa kudumu wa asasi zinazopendwa, bali kwa kuzuka kwa machafuko ya ghafla dhidi ya udikteta wa mfano wa kifalme na utawala wa makabaila.  Hata hivyo, baada ya muda mpenda jamhuri mwanademokrasia alikuja kumiliki sehemu kubwa ya kuhodhi.  Sehemu kubwa ya uso wa dunia na kuifanya ijihisi kama mojawapo wa wanachama wenye nguvu sana wa jamii ya mataifa, na serikali ya kuchaguliwa ni inayowajibika likawa somo la uchunguzi na uhaikiki ambao kusubiri ukweli uelewa uliopo.  Hivi sasa ilitambuliwa kwamba misemo kama vile “kujitawala” na “nguvu za watu juu yao wenyewe “hazielezi hali halisi ya kadhia hiyo.  “Watu” ambao wanatekeleza mamlaka si siku zote ni wakwale pamoja na wale ambao juu yao inatekelezwa; na “kujitawala” kunakoongelewa si serikali ya kila mtu kwa ajili yake mwenyewe, bali ya kila mtu kwa wengine wote.  Juu ya hayo kiiutendaji utashi wa watu unamaansiha utashi wa walio wengi kabisa au sehemu ya watu iliyo sehemu tendaji zaidi, au walio wengi au wale wanaofanikiwa katika kujifanya wakubaliwe kama wengi, umma; hivyo, wanaweza kutaka kugandamiza sehemu ya idadi yao na hadhari zinazohitajika sana dhidi ya hili kama dhidi ya matumizi yoyote mabaya ya mamlaka.  Hivyo, ukomo, mamlaka ya serikali juu ya watu binafsi havipotezi sehemu yoyote ya umuhimu wake wakati washika madaraka wanapowajibika mara kwa mara kwa jamii, yaani sehemu yenye nguvu zaidi ndani yake.  Mtazamo huu wa mambo ambao unajipendekeza sawia kwa akili za wanaofikiri na kwa matakwa ya matabaka muhimu katika jamii ya Ulaya kwa wale ambao maslahi halisi au yanayodhaniwa kuwa demokrasia ni mbaya, hayakuwa na matatizo katika kujianzisha; na mabahatisho ya kisiasa “udhalimu wa walio wengi” [*] hivi sasa yanajumuishwa kwa ujumla katika kati ya uovu ambao dhidi yake jamii inahitaji kuwa makini.

 

Kama dhuluma nyingine zozote, mwanzo udhalimu wa walio wengi ulikuwa, na kipungufu bado unaogopwa, zaidi kama kufanya kazi kupitia vitendo vya mamlaka ya umma.  Lakini watu wanaofikiri wanatambua kwamba jamii yenyewe inapokuwa dhalimu – jamii kwa pamoja, juu ya watu binafsi tofauti walioiunda – njia zake za kidhalimu hazibanwi kwenye vitendo ambavyo vinaweza kuvifanya kwa mikono ya watendaji wake wa kisiasa.  Jamii inaweza na inatekeleza mamlaka yake yenyewe: na iwapo inatoa mamlaka yasiyo sahihi, badala ya sahihi, au mamlaka yoyote yale katika mambo ambayo inatakiwa kutokuingilia, inaufanya udhalimu wa kijamii uweze kukua zaidi kuliko aina nyingine za ugandamizaji wa kisiasa kwa vile, ingawa haitetewi na adhabu zilizokiuka, huacha njia chache za kukwepa, ikiingia ndani zaidi katika utondoti wa maisha, na kuitia roho yenyewe utumwani.  Hivyo, ulinzi dhidi ya udhalimu wa hakimu hautoshi: kunahitajika pia ulinzi dhidi udhalimu wa maoni na hisia zilzopo, dhidi ya mwelekeo wa jamii kulazimisha, kwa njia nyingine zaidi ya adhabu za kiraia, maoni na vitendo kama taratibu za mwenendo kwa wale wasiokubaliana nao; kutia pingu maendeleo na kama inawezekana, kuzuia kuundwa kwa ubinafsi wowote usio katika upatanifu na njia zake, na kulazimisha wahusika wote kujiweka katika mtindo kwa mfano wake wenyewe.  Kuna ukomo kwenye uingiliaji wa kihaki wa mawazo ya pamoja na uhuru binafsi wa kujiamulia: na kupata ukomo huu na kuudumisha dhidi ya kuingiliwa, haviachani kwa mazingira mazuri ya mambo ya binadamu, kama vile ulinzi dhidi ya udikteta wa kisiasa.

 

Lakini ingawa wazo hili halina uwezekano wa kushindaniwa katika hali ya jumla, lakini swali halisi, wapi pa kuweka ukomo – jinsi ya kuweka rekebisho linalofaa kati ya uhuru binafsi na udhibiti wa kijamii – ni somo ambamo kabla kile kitu kitafanywa.  Kinachofanya kuwepo kuwe na maana kwa yeyote yule, kunategemea utekelezaji wa vikwazo juu ya vitendo vya watu wengine.  Hivyo, baadhi ya kanuni za mwenendo lazima ziamuriwe, kwanza kwa sehria na kwa maoni kuhusu mambo mengi ambayo si mada zinazostahili kwa uendeshaji wa sheria.  Hizi sheria ziwe nini ni swali kuu katika mambo ya binadamu; lakini kama tukiacha chache ya hali ya kadhia zilizo dhahiri kabisa, ni mojawapo ya zile ambazo zimepata maendeleo kidogo sana katika kuyatatua.  Si miongo miwili na si hata nchi mbili, zimeamua katika maana moja; na uamuzi wa mwongo mmoja au nchi moja ni maajabu kwa nchi nyingine.  Hata hivyo, watu wa mwongo wowote ule na nchi yoyote hawatilii shaka tena tatizo lolote ndani yake, kuliko kama ingekuwa mada ambayo wakati wote binadamu walikuwa wamekubaliana.  Kanuni ambazo zinakubalika miongoni mwao kwa zinaelekea kujishuhudia na kujihalalisha.  Hili ambalo ni ndoto ya mifano ya athai za desturi za kichawa, ambayo si asili ya pili tu, kama methali inavyosema, bali inaendelea kuchanganywa na ya mwanzo.  Athari za desturi katika uzuiaji wa mashaka yoyote kuheshimu kanuni za mwenendo ambazo binadamu hulazimishana, zimekamilika kabisa kwa sababu mada ni ile ambayo haifikiriwi kwa ujumla kuwa muhimu kwamba sababu lazima zitolewe au na mtu mmoja kwa wengine, au kwa kilea moja kwake mwenyewe.  Watu wamezoea kuamini na wamekuwa wakitiwa moyo katika imani na baadhi ambao wanatamani tabia ya wanafalsafa, kwamba hisia zao kwenye mada za hali hii ni bora zaidi kuliko mantiki na kufanya mantiki yasiwe muhimu.  Kanuni inayotendeka ambayo inawaongoza kwenye maoni yao kuhusu kanuni za mwenendo wa binadamu ni hisia katika akili ya kila mtu kwamba kila mtu atakuwa kufanya kama yeye, pamoja na wale ambao wanahurumiana, wangepena watende.  Hakika, hakuna hata mmoja anayedai katika nafsi yake kwamba kiwango chake cha hukumu ni kupenda kwake, lakini maoni kwenye suala la mwenendo, yasiyoungwa mkono na mantiki yanaweza kuhesabiwa kama upendeleo wa mtu binafsi; na pale ambapo mantiki yanatolewa, ni ombi tu la upendeleo unaofanana wa watu wengine, bado ni upendeleo wa watu wengi tu badala ya mtu mmoja.  Hata hivyo, kwa mtu wa kawaida, upendeleo wake mwenyewe ulioungwa mkono hivyo si sababu sahihi inayoridhisha tu, bali sababu peke ambayo kwa ujumla kwa sababu yoyote ile ya dhani zake za kimaadili, kionjo, umiliki ambavyo havikuandikwa katika imani zake za kidini, na mwongozo mkuu hata katika fasili ya hiyo.

Maoni ya binadamu, kwa kupatana, kuhusu chenye kusifika au kulaumika yanaathiriwa na sababu zote za namna nyingi na mbalimbali ambazo huathiri matakwa yao kuhusu mwenendo wa wengine na ambazo ni nyingi kama zile ambazo zinaamua matakwa yao kuhusu mada yoyote ile.  Wakati mwingine mantiki yao – katika nyakati nyingine upendeleo wao au ushirikina: mara nyingi athari za kijamii, si mara chache athari zao dhidi ya kijamii, husuda au kijicho au ufidhuli na dharau: lakini kawaida zaidi matamanio yao au hofu kwa ajili yao wenyewe – maslahi yao binafsi ya kihalali au yasiyo ya kihalali.  Kila  palipo na tabaka la juu, sehemu kubwa ya maadili ya nchi hutokana na maslahi yake ya kitabaka na hisia zake kuhusu ubora wa tabaka.  Maadili kati ya Waspatani na Waheloti, kati ya walowezi na wanegro, kati ya watoto wa kifalme na watawaliwa, kati ya malodi na watwana, kati ya wanawake na wanaume kwa sehemu kubwa yamekuwa uundaji wa maslahi haya ya kitabaka na hisia: na mawazo yaliyozalishwa namna hiyo badala yake kujibiza kwenye hisia za kimaadili za wanajamii wa tabaka la juu, katika uhusiano miongoni mwao.  Kwa upande mwingine, pale ambapo tabaka lililokuwa la juu limepoteza nafasi yake au pale ambapo nafasi yake ya juu imekuwa haipendwi, hisia za kimaadili zilizopo, mara nyingi huvumilia chapa ya kuchukia kukoza uvumilivu wa ubora.  Kanuni nyingine kuu ya uamuzi wa kanuni za mwenendo, katika kutenda na uvumilivu, ambavyo vinatishiwa na sheria au maoni, umekuwa unyonge wa  binadamu kuelekea kwenye kile kinachodhaniwa kuwa upendeleo wa chuki kubwa za mabwana wa muda, au miungu yao. Ingawa huu unyonge ni wa kiuchoyo, lakini si unafiki; huibua hisia halisi za kuchukua; uliwafanya watu wawachome wachawi na waasi:  Miongoni mwa athari nyingi duni, maslahi ya jamii ya jumla na yaliyo bayana yamekuwa na nafasi yake, na kubwa, katika uelekezaji wa hisia za kimaadili: pungufu ya hivyo, kama suala la kimantiki; na kwa fikra zao wenyewe, kutoka matokeo ya huruma na uhasama uliotokana navyo na huruma na uhasama ambao ulihusiana kidogo sana na maslahi ya jamii au haukuhusiana hata kidogo, vinajifanya vihisiwe katika uanzishaji wa maadili kwa nguvu kubwa.

 

Yanayopendwa na yasiyopendwa na jamii au baadhi ya sehemu zake zenye nguvu ndio jambo kuu ambalo kiutendaji liliamua kanuni zilizowekwa kuyanatwa kwa ujumla, chini ya adhabu za sheria au maoni.  Na kwa ujumla, wale walio mbele ya jamii katika fikra na hisia wameiacha hali hii ya mambo ambayo kimsingi haichokozwi:  Hata hivyo, wanaweza kuwa wamekinzana nayo katika baadhi ya utondoti wake.  Wamejishughulisha katika kuulizia mambo ambayo jamii inapaswa kuyapenda au kuyachukia kuliko katika kuuliza iwapo mambo yake yanayopendwa au kuchukiwa yawe sheria kwa watu binafsi.  Walipendelea kujitahidi kubadilika hisia za binadamu kuhusu hoja mahususi ambazo wao wenyewe walikuwa waasi juu yake, kuliko kufanya jambo la pamoja katika ulinzi wa uhuru, pamoja na uasi kwa ujumla.  Kadhia pekee ambayo sababu kuu imechukuliwa kimsingi na kudumishwa kwa uthabiti, na yeyote yule ila mtu binafsi hapa ni kule, ni ile ya imani ya kidini: kadhia elekezi katika namna nyingi elekezi na kuunda mfano unaovutia wa kuweza kuwa na kosa wa kile kinachoitwa hisia za kiadilifu; kwa odium theologicum, katika Wokole mwaminifu ni mojawapo ya kadhia zisizo tata za hisia za kiuadilifu. Wale ambao walivunja kiini cha kile kilichojiita Kanisa la Ulimwengu, kwa ujumla walikuwa na utashi mdogo kuruhusu tofauti ya mawazo ya kidini kama lile kuanza lenyewe.  Lakini joto la mgogoro lilipomalizika, bila ya kutoa ushindi kamili kwa upande wowote, na kule kanisa au dhehebu lilipunguzwa kupunguza matumaini yake kwenye kubakiza umiliki wa ardhi ambayo lilikuwa likimiliki; wachache kwa kuona hawakuwa na fursa ya kuwa wengi, walikuwa chini ya ulazima wa kuwasihi wale ambao hawakuweza kuwabadili, kwa ruhusa ya kutofautiana.  Ni kwa mujibu wa uga huu wa mapambano, karibu pekee, kwamba haki za mtu binafsi dhidi ya jamii zinadaiwa kuhusu uwanja mpana wa kanuni, na dai la jamii kutekeleza mamlaka juu ya wanaopinga wakaribisha wezi.  Waandishi wakubwa ambao dunia inawiwa nao uhuru wa kidini ulio nao, wanadai uhuru wa kufikiri kama haki inavyowezeakana na walikataa kabisa kwamba binadamu anawajibika kwa wengine kwa imani yake ya kidini.  Hata hivyo, kilicho asili kabisa kwa ubinadamu ni kutovumilia katika chochote kile wanachokijali, hasa kwamba uhuru wa dini hauekelezwi popote pale ila pale ambapo kuna kutojali dini, ambako hakupendwi amani yake ibughudhiwe na magomvi ya kiteolojia, kumeongeza uzito wake kwenye kipimo.  Katika akili za karibu watu wote waumini wa dini, hata katika zile nchi zenye uvumilivu wa hali ya juu kabisa, daraka la uvumilivu linakubaliwa kwa sazo la ukimya.  Mtu mmoja atavumilia maoni asiyokubaliana nayo katika masuala ya serikali ya kanisa lakini si imani ya kusikiliza bila ya kuuliza, mwingine anaweza kumvumilia kila mtu, pamoja na Mfanasi wa Kanisa la Kihateliki au Mkristo asiyeamini utatu Mtakatifu, mwingine kila mtu anayeamini katika dini iliyopata mfumo; wache humnyeusha huruma yao mbali zaidi lakini kukoma kwenye imani ya Mungu katika hali ya siku za baadaye.  Popote pale ambapo hisia za wengi bado ni za kweli na kali, huonekana kupunguza sehemu ndogo ya dai lake la kuheshimiwa.

 

Nchini Uingereza, kutokana na mazingira ya kipekee ya historia yetu ya kisiasa, ingawa kiini cha maoni pengine ni kizito, kile cha sheria ni chepesi zaidi, kuliko katika nchi nyingi nyingine za Ulaya; na kuna wivu mwingi wa kuingiliwa moja kwa moja, kwa mamlaka ya kutunga sheria ya kiutendaji yenye mwenendo binafsi, sio hasa kutoka kwenye fikra zozote za haki kwa uhuru wa mtu binafsi; kama kutoka kwenye tabia inayoendelea ya kujikimu ya kuiangalia serikali kwenye serikali kama kuwakilisha maslahi kinzani kwa umma.  Walio wengi bado hawajajifunza kuhisi mamlaka ya serikali, nguvu zao au maoni yake, maoni yao.  Wanapofanya hivyo, pengine uhuru binafsi utajiweka wazi kuvamiwa kutoka serikalini;  kama ambavyo iko tayari kuteka maoni ya umma.  Lakini hadi sasa, kuna kiasi kikubwa cha kuhisi tayari kuitwa dhidi ya jaribio lolote la sheria la kuwadhibiti watu binafsi katika vitu ambavyo hadi sasa hawajazoea kudhibitiwa navyo; na hili ni kwa ubaguzi mdogo iwapo suala hili liko au haliko ndani ya eneo la kihalali la udhibiti wa kisheria; kiasi kwamba hisia, kwa ujumla salamu za hali ya juu, ni pengine mara nyingi kuwekwa mahali pasipo pake pamoja na kukwamishwa katika mazingira mahususi ya matumizi yake.  Kwa kweli, hakuna kanuni inayotambuliwa na adabu au utovu wa adabu wa kuifikia kati serikali inapimwa kidesturi.  Watu huamua  kwa mujibu wa upendeleo wao binafsi.  Baadhi, popote pale wanapoona zuri lolote kufanywa, au baya la kurekebishwa wangechochea kwa hiari yao serikali kufanya shughuli hiyo; ambapo wengine wangependelea kubeba karibu kiasi chochote cha uovu wa jamii kuliko kuongeza mojawapo ya idara za maslahi ya kibinadamu yenye kuongozwa na udhibiti wa serikali.  Na watu hujipanga kwenye upande mmoja au mwingine katika kadhia yoyote ile mahususi, kufuatana na huu mwelekeo wa jumla wa hisia zao; au kwa mujibu wa kiwango cha maslahi ambacho wanahisi katika kitu mahususi ambacho kinapendekezwa kwamba serikali ifanye nini au kwa mujibu wa imani wanafahamu kwamba serikali ingefanya au isingefanya katika jinsi wanayopendelea, lakini mara chache sana kuhusiana na maoni yeyote ambayo wanayafuata kwa uthabiti; kuhusu mambo gani yanafaa kufanywa na serikali.  Na kwangu inaonekana kwamba kufuatilia huku kutokuwepo kwa sheria au kanuni hivi sasa upande mmoja unakosea mara nyingi kama upande mwingine, uingiliaji kati wa serikali bila ya mfuatano uliokuwa umeombwa katika namna isiyo nzuri na kulaaniwa katika namna isiyo nzuri.

 

Lengo la Insha hii ni kuteka kanuni moja nyepesi sana, kama ilivyo na haki ya kutawala kikamilifu shughuli za jamii pamoja na mtu binafsi katika namna ya shurutisho na udhibiti, iwapo njia zilizotumiwa na nguvu za kimwili katika umbo la adhabu za kisheria au kulazimishwa kimaadili na maoni ya umma.  Kanuni ni kwamba mwisho pekee ambao binadamu wamethibitishiwa, mtu mmojammoja au kwa pamoja katika kuingilia uhuru wa vitendo wa mmojawao yeyote, ni kujilinda.  Kwamba nia pekee ambayo kwayo nguvu zinaweza kutumika kwa haki kwa mwanajamii yoyote iliyostaarabika, dhidi ya utashi wake ni kuzima madhara dhidi ya wengine.  Faida yake mwenyewe ama ya kimwili au kiakili si uthibitisho wa kutosha.  Hawezi kulazimishwa kisheria kufanya au kuvumilia kwa sababu itakuwa bora kwake kufanya hivyo, kwa sababu itamfurahisha zaidi, kwa sababu, katika mawazo ya wengine kufanya hivyo kungekuwa busara, au hata haki.  Hizi ni sababu nzuri za kumlalamikia au kuongea naye kwa mantiki, au kumshawishi au kumsihi, lakini si kwa kumlazimisha, au kumtembelea kwa jicho la uovu, pale anapofanya vinginevyo kuhalalisha hilo, mwenendo ambao unakusudiwa kumzuia lazima upangwe ili kuzalisha uovu kwa mtu mwingine.  Sehemu pekee ya mwenendo wa mtu yoyote, ambaye yeye ni msikivu kwa jamii, ni ile inayowahusu wengine.  Katika sehemu ambayo inahusu yeye tu, kwa haki uhuru wake ni kamili.  Uhuru yeye mwenyewe, mwili na akili yake, mtu binafsi yuko huru.

 

Pengine hakuna umuhimu wa kusema kwamba kanuni hii imekusudiwa kutumika tu kwa binadamu katika ukomavu wa welekevu wao.  Hatuzungumzii  kuhusu watoto, au vijana chini ya kumi ambao sheria inaweza kupanga kama wa mwanamume au mwanamke.  Wale  ambao bado wako katika hali ambayo inahitaji kupatiwa matunzo na wengine, lazima walindwe dhidi ya vitendo vyao wenyewe pamoja na dhidi ya madhara ya nje.  Kwa mantiki hiyohiyo, tunaweza kutozingatia zile hali za kuwa nyuma za jamii ambamo mbari yenyewe inaweza kufikiriwa katika utoto.  Matatizo ya awali katika njia ya maendeleo ya kujianzia ni makubwa sana, kiasi kwamba mara chache kunakuwepo na uchaguzi wowote wa njia za kuyashinda; na mtawala aliyejawa na ari ya maboresho anathibitishiwa katika matumizi ya manufaa yoyote ambayo yatapata mwisho, pengine vinginevyo mwisho usiopatikana.  Udiktekta ni aina halali ya serikali halali katika kushughulikia ukatili, ili mradi mwisho yawe maboresho yao na njia zilikuwa halali kwa kuhakikisha matokeo hayo.  Kama kanuni, uhuru haitumiki katika hali ya mambo kutangulia wakati ambapo binadamu wanakuwa wanaweza kuboreshwa na majadiliano huru na ya usawa.  Hadi hapo, hakuna chochote kwa ajili yao bali utiifu unaojitokeza kwa Akbar au Charlemagne, iwapo wana bahati kupata walau moja.  Lakini mara tu binadamu wakipata uwezo wa kuongozwa kwenye uboreshaji wao wenyewe kwa imani au ushawishi (kipindi ambacho kimeafikiwa zamani katika mataifa yote ambayo tunahitaji kujishughulisha) shurutisho, katika aina ya moja kwa moja au katika maumivu na adhabu kwa kutoyafuata, haihitajiki tena kama njia kuelekea kwenye mafanikio yao wenyewe na kuhalalika tu kwa usalama wa wengine.

 

Inafaa kutamka kwamba ninaacha faida ambayo ingeweza kupatikana kwenye hoja yangu kutoka kwenye wazo la haki dhahania, kama kitu kilicho huru kutokana na matumizi.  Nachukulia matumizi kama maombi ya mwishowe kwenye maswali yote ya kimaadili: lakini lazima iwe matumizi katika maana yake pana kabisa yenye msingi wa maslahi ya kudumu ya mtu kama kiumbe cha maendeleo.  Nadai kwamba maslahi haya yanatoa mamlaka ya  kugandamiza kwa hiari ya mtu binafsi kwa udhibiti wa nje; kuhusu tu vile vitendo vya kila kimoja ambavyo vinahusu maslahi ya watu wengine.  Iwapo mtu yeyote yule akifanya kitendo cha kuwaumiza wengine, kuna hadhi kama ilivyoonekana mwanzoni ya kumwadhibu kwa sheria au pale ambapo adhabu za kisheria hazitumiki kiusalama, kwa kutoridhika kwa jumla.  Pia, kuna vitendo vingi chanya kwa manufaa ya wengine ambavyo anaweza kulazimika kihaki kuvifanya kama vile kutoa ushahidi kwenye mahakama ya sheria, kuchukua hisa yake stahiki katika ulinzi wa wote, au katika kazi yoyote ya pamoja iliyo muhimu kwa maslahi ya jamii ambayo anafaidi ulinzi; na kutekeleza vitendo fulani vya manufaa, kama vile kuokoa maisha au kuingilia kati kuwalinda wasio na ulinzi dhidi ya matumizi mabaya, mambo ambayo kila yanapokuwa jukumu la mtu kufanya anaweza kuwajibishwa na jamii kwa haki kabisa kwa kutotenda.  Mtu anaweza kusababisha uovu kwa wengine sio tu kwa vitendo vyake bali kwa kuiga chake, na kwa vyovyote vile anawajibika kihaki kwa madhara.  Ni kweli, kadhia ya pili inahitaji jaribio la hadhari zaidi la ulazimishaji kuliko kadhia ya mwanzo.  Kumfanya mtu yeyote kuwajibika kwa kuwafanyia wengine maovu, ni sheria, kumfanya awajibike kwa kutokuzuia uovu, kwa kuongea kiulinganishi, ni upekee.  Hata hivyo, kuna kadhia nyingi bayana na hatari vya kutosha kuhalalisha upekee huo.  Katika mambo yote yanayochukulia uhusiano wa nje wa mtu binafsi, yeye kisheria ni mtiifu kwa wale ambao maslahi yao yanahusika, na iwapo kuna haja ya jamii kama mlinzi.  Mara nyingi, kuna sababu nzuri kwa kutomwona kuwa anawajibika; lakini sababu hizi lazima zitokane na manufaa ya kadhia: kwa sababu ni aina ya kadhia ambamo yeye kwa ujumla ana uwezekano wa kufanya vizuri zaidi, anapoachwa kwa busara yake, kuliko anapodhibitiwa kwa namna yoyote ile ambayo jamii ina mamlaka ya kumdhibiti; au kwa vile jaribio la kutekeleza udhibiti lingezalisha uovu mwingine, ukubwa uleule ambao ingeuzima.  Pale ambapo sababu kama hizi zinazuia ulazimishaji wa utiishaji wa wajibu dhamini ya wakala mwenyewe iingie katika kiti kitupu cha utoaji hukumu na kulinda lengo maslahi ya wengine ambayo hayana ulinzi wa nje: akijihukumu imara zaidi, kwa sababu kadhia haikubali kuwajibishwa kwa hukumu ya viumbe wenzake.

 

Lakini kuna uwanja wa vitendo ambamo jamii, kama inavyotofautishwa na mtu binafsi inaweza kuwa tu na maslahi yasiyo ya moja kwa moja; kuelewa sehemu yote ile ya maisha na mwenendo wa binadamu unaomwathiri yeye mwenyewe tu, au kama pia unawaathiri wengine kwa kukubali bila kudongwa na ushiriki huru, wa kujitolea.  Ninaposema yeye tu, ninamaanisha moja kwa moja na kwa mara ya kwanza: kwa chochote kile kinachomwathiri kinaweza kuwaathiri wengine bkupitiab yeye mwenyewe; na mkatao unaoweza kutolewa katika tukio hili la bahati nasibu utafikiriwa katika matokeo.  Hii basi ndio miliki ya halisi ya ukanda wa uhuru wa kujiamulia wa binadamu.  Kwa dhamiri, ikidai uhuru wa wawili wa dhamira, katika namna pana kabisa, uhuru wa mawazo na hisia; uhuru wawili wa maoni na mawazo kuhusu mada zote, kiutendaji au kuwazia, kisayansi, kiuadilifu, au kiteolojia.  Uhuru wa kutoa au kuchapisha maoni unaweza kuelekea kuangukia chini ya kanuni tofauti, kwa sababu ni sehemu ya ile sehemu ya mwenendo wa mtu binafsi ambayo inahusu watu wengine; lakini kwa kuwa na umuhimu sawa na uhuru wa maoni wenyewe, na ukitegemea kwa kiasi kubwa kwenye sababu zilezile, haitenganishiki nao.  Pili, hiyo kanuni inahitaji uhuru wa vionjo na kufuatilia; wa kuunda mpango wa maisha yetu kuendana na tabia zetu wenyewe; wa kufanya tunachopenda, kwa shuruti ya matokeo kama yafuatayo: bila ya kizuizi kutoka kwa binadamu wengine, ili mradi tunachokifanya hakiwadhuru, ingawa hata kama wanaweza kuuona mwenendo wetu kuwa wa kipuuzi, wa kikaidi au usio sawa.  Tatu, kutoka kwenye huu uhuru wa kujiamulia wa kila mtu binafsi unafuata uhuru ndani ya ukomo huohuo, wa mchanganyiko miongoni mwa watu binafsi; uhuru wa kuunganika, kwa nia isiyohusisha madhara kwa wengine: watu wanaounganika wakidhaniwa kuwa watu wazima na wasiolazimishwa wala kudanganywa.

 

Hakuna jamii ambayo uhuru huu haiuheshimu kwa ujumla, ambayo iko huru, hata serikali yake iwe ya aina gani, na hakuna jamii iliyo huru kabisa ambamo uhuru huu hauko kabisa na hauna sifa kamili.  Uhuru pekee unaostahili jina hilo ni ule wa kufuatilia mambo yetu wenyewe kwa namna yetu wenyewe ili mradi hatujaribu kuwanyima wengine kile kilicho chao au kuzima juhudi zao za kukipata.  Kila mtu ni mlezi anayestahili wa afya yake mwenyewe, iwe ya kimwili, au kiakili na kiroho.  Binadamu ni wanufaikaji wakubwa zaidi.  Kwa kusumbuana kuishi jinsi inavyoonekana inafaa kwao, kuliko kulazimishana kuishi kama inavyoonekana inafaa kwa wengine wote.

 

Ingawa kanuni hii si mpya na kwa baadhi ya watu inaweza kuwa na kauli ya ukweli, hakuna kanuni inayokinzana moja kwa moja na tabia ya jumla ya kuwepo kwa maoni na utendaji.  Jamii imetumia kikamilifu juhudi nyingi katika jaribio (kwa mujibu wa mwanga wake) kuwalazimisha watu kukubali dhana zake za ubora wa binafsi na wa kijamii.  Jumuiya za madola ya zamani walidhani walistahili kutenda, na wanafalsafa wa zamani waliunga mkono, kanuni ya kila sehemu ya mwenendo.  Mwenendo binafsi kwa mamlaka ya umma, kwa msingi mwamba Dola ilikuwa na maslahi ya ndani kabisa katika nidhamu ya kiwiliwili na kiakili ya kila mmoja wa raia zake; aina ya kufikiri ambayo ingeweza kukubalika katika jamhuri ndogondogo zilizozungukwa na maadui wenye nguvu katika hatari kubwa za mara kwa mara za kuangamizwa na mashambulizi ya kigeni au viungu za ndani, ambazo kwazo hata kipindi kifupi cha nguvu zilizopumzishwa na kujiamulia, kungekuwa hatari kwa urahisi kabisa kiasi kwamba wasingeweza kumudu kusubiria athari za kudumu za kufaa za uhuru.  Katika dunia ya kisasa, ukubwa zaidi wa jamii za kisiasa, na juu ya yote, utenganisho kati ya mamlaka ya kiroho na ya maisha (ambayo yaliweka mwelekeo wa dhamiri ya binadamu katika mikono mingine kuliko ile abayo ilidhibiti mambo yao ya kidunia), zilizuia  uingiliaji kati mkubwa wa sheria katika utanashati wa maisha binafsi; lakini mashine za ugandamizaji wa maadili zimetumika kwa nguvu nyingi zaidi dhidi ya maono tofauti kutokana na mawazo yanayotawala katika kujifikiria binafsi, kuliko hata katika masuala ya kijamii, dini, sifa zenye nguvu kabisa ambazo zinaingia katika uundaji wa hisia za kiuadilifu, zikiwa karibu zimetawaliwa tu na aina na lengo la msonge wa madaraka, wakitafuta udhibiti juu ya kila idara ya mwenendo wa binadamu, au kwa roho ya utakatifu.  Na baadhi ya hao wafanye mageuzi wa kisasa ambao wamejiwekea katika upinzani wenye nguvu kabisa kwa dini za zamani; kwa namna yoyote ile hawakuwa nyuma ya aina makanisa au madhehebu katika utetezi wa haki ya utawala wa kiroho: hususan M. Comte ambaye mfumo wake wa kijamii, kama ulivyojionyesha katika cSystem de Politique Positivec [*] unalenga kuanzisha (ingawa zaidi kwa uadilifu kuliko vifaa vya kisheria) udikteta wa jamii juu ya mtu binafsi; kuzidi kitu chochote kilichofikiriwa katiak siasa bora ya wananidhamu imara kabisa miongoni mwa wanafalsafa wa kale.

 

Ukiacha itikadi za kipekee za mtu mmojammoja mwenye fikra nyingi, pia duniani kwa ujumla kuna mwelekeo unaoongezeka wa kuongeza visivyostahili madaraka ya jamii juu ya mtu binafsi; kwa nguvu za maoni na hata kwa njia ya kutunga sheria: na kama mwelekeo wa mabadiliko yote yanayotokea duniani, ni kuimarisha jamii, na kupunguza nguvu za mtu binafsi,, kuingilia huku si mojawapo ya maovu yanayoelekea kutokomea yenyewe lakini kinyume chake kukua zaidi na hali zaidi.  Tabia za binadamu, iwapo ni kama viongozi au raia, kulazimisha maoni na mielekeo yao kama sheria ya mwenendo kwa wengine, inaungwa mkono kwa nguvu na baadhi ya hisia bora na maya kabisa kwa asili ya binadamu, ambazo mara nyingi hazizuiwi na chochote kile isipokuwa utakaji wa madaraka; na kwa vile mamlaka hayapungui bali huongezeka, isipokuwa kama kizuizi kizito cha kusadiki kwa kiadili kinaweza kuinuliwa dhidi ya madhara katika mazingira ya sasa ya dunia lazima itegemee kuongezeka.

 

Kwa ajili ya hoja itafaa iwapo badala ya kuingia mara moja kwenye tasnifu ya jumla, tujibane kwanza kwenye tawi lake moja, ambako kanuni inayosemwa hapa ni kama si kamilifu, lakini kwa kiasi fulani, inatambuliwa na maoni ya sasa.  Hili tawi moja ni Uhuru wa Maoni: ambayo kutoka kwake haiwezekani kutenganisha uhuru  unaohusiana na uhuru wa kuongea na wa kuandika.  Ingawa, kwa kiasi kikubwa, uhuru huu wa kiujiamulia unaunda sehemu ya uadilifu wa kisiasa wa nchi zote zinazotabiri kuvumiliana  kidini na asasi huru, misingi, kwa pande zote mbili za kifalsafa na kiutendaji, ambamo zimo, pengine hazijulikani sana kwa akili ya jumla pia haitambuliwi kikamilifu na hata wengi wa viongozi wa maoni, kama ambavyo ingetegemewa.  Misingi hiyo inapoeleweka kwa usahihi, ina matumizi mapana zaidi kuliko kwasehemu moja tu ya somo, na mafikirio makini ya sehemu hii ya swali itaonekana kuwa utangulizi bora kabisa kwa yaliyosalia.  Wale ambayo nitakayosema si mapya natumaini wanaweza kunisamehe iwapo naingia zaidi katika mjadala wa somo ambalo limekuwa likijadiliwa kwa karne nyingi.

 

SURA YA II

 

Kuhusu Uhuru wa Maoni na Majadiliano

 

Inatumainiwa kwamba wakati umepita ambapo utetezi wowote ungekuwa lazima kwa “uhuru wa vyombo vya habari” kama mojawapo ya usalama dhidi ya serikali fisadi na ya kidikteta.  Hivi sasa tunaweza kufikiria kwamba hakuna hoja inayohitajika dhidi ya kuruhusu kutunga sheria au utendaji, ambao hakubainishwa katika maslahi na watu, kuwaagiza maoni na kuamua dhana au hoja zipi watakazoruhusiwa kuzisikia.  Kipengele hiki cha swali kinalazimishwa mara nyingi na kwa ushindi na waandishi waliotangulia, kiasi kwamba hakuna haja ya kusisitizwa mahali hapa.  Ingawa kuhusu somo la vyombo vya habari, sheria ya Uingereza hivi leo ni dhalili kama ilivyokuwa nyakati za Matida, kuna hatari ndogo sana ya kutekelezwa dhidi ya majadiliano ya kisiasa, isipokuwa tu wakati wa hofu ya muda mfupi, ambapo woga wa upinzani huwasukuma mawaziri na majaji kutoka kwenye taratibu zao; – na, kuongea kwa ujumla, katika nchi za kikatiba si jambo la kukamatwa, kwamba iwapo serikali inawajibika kikamilifu kwa watu au la, mara nyingi atajaribu udhibtii wa kutoa maoni, isipokuwa iwapo pale katika kuifanya hivyo, inajifanya kuwa chombo kutovumilia kwa jumla cha umma.  Kwa hiyo, tufikirie kwamba serikali iko pamoja na watu kikamilifu na kamwe haifikirii kutumia madaraka yoyote ya nguvu isipokuwa pale tu inapokubaliana na kile inachokidhani kuwa sauti yao.  Lakini nakana haki ya watu kutumia ushurutishaji huo ama wao wenyewe au na serikali yao.  Mamlaka yenyewe ni haramu.  Serikali bora kabisa haina jina zaidi ya lile lililo baya zaidi.  Inadhuru au inadhuru zaidi, inapotumia nguvu kwa mujibu wa maoni ya umma kuliko inapopigana nayo.  Iwapo binadamu wote, ila mmoja, wangekuwa na maoni yanayofanana, na mtu mmoja tu angekuwa na maoni tofauti, binadamu wasingekuwa na haki katika kumnyamazisha huyo mtu mmoja, kuliko yeye iwapo huyo mtu mmoja angekuwa na mamlaka, angekuwa na haki ya kuunyamazisha ubinadamu.  Kama maoni yangekuwa umiliki binafsi usiokuwa na thamani ila kwa umiliki tu; iwapo kuzuiwa katika kipindi kingekuwa madhara binafsi tu, ingefanya tofauti kama madhara hayo yalilazimishwa kwa watu wachache tu au kwa wengi.  Lakini uovu huu wa kipekee wa kuunganisha utoaji wa mawazo ni kuibia mbari ya binadamu, vizazi vya baadaye pamoja na kizazi kilichopo, wale wanaoasi kutoka kwenye maoni, wengi zaidi kuliko wale wanayoyashikilia.  Iwapo maoni hayo ni sahihi, yananyimwa fursa ya kubadilishana kosa kwa ukweli: iwapo ni kosa, wanapoteza, kile ambacho karibu ni manufaa – makubwa, utambuzi dhahiri zaidi na wenye picha ya uhai zaidi ya ukweli, uliozalishwa na mgongano wake na kosa.

 

Ni muhimu kuzifikiria hizi nadharia tete kitofauti, kila moja ikiwa na tawi bayana la hoja linalofanana nalo.  Hatuwezi kuwa na uhakika kwamba maoni tunayojitahidi kukomesha ni wazo la uongo.

 

Kwanza: Maoni ambayo yanajaribiwa kugandamizwa na mamlaka yanawezekana kuwa kweli.  Wale wanaotamani kuyagandamiza wanaukana ukweli wake, lakini hawana uhakika.  Hawana mamlaka kuamua swala la binadamu wote, na kutokumjumuisha mtu mwingine yeyote kutoka jinsi ya kutoa uamuzi.  Kukataa kusikiliza maoni kwa sababu wana uhakika ni kosa, ni kudhania kwamba uhakika wao ni jambo lilelile wana uhakika kamili.  Majadiliano yote ya ugandamizaji ni dhana ya kuwa  na uhakika.  Kulaaniwa kwake kunaweza kukubaliwa kutoka katika hoja hii ya wote, si mbaya zaidi kwa kuwa ya wote.

 

Kwa bahati mbaya, kwa dhana nzuri ya binadamu, ukweli wa uhakika wao uko mbali sana na kubeba uzito wa uamuzi wao wa kiutendaji, ambao kila wakati unakubaliwa kinadharia kwani ambapo kila mmoja anajifahamu kuwa na uhakika, wachache wanafikiri ni muhimu kuchukua hadhari dhidi ya uhakika wao wenyewe, au kukubali dhana kwamba wazo lolote ambalo wanahisa kuwa la uhakika sana, kunaweza kuwa mojawapo ya mifano ya kosa ambalo wenyewe wanakiri kuwajibika.  Watoto wa wafalme safi au wale ambao wanazoea staha isiyo na kikomo, kwa kawaida, hulihisi hili kujiamini kikamilifu katika mawazo yao karibu kwenye mada zote.  Watu walio katika hali ya furaha zaidi, ambao wakati mwingine husikia mawazo yao yakipingwa na siyo kwamba hawakuzoea kusahihishwa pale ambapo hawako sahihi, huweka utegemezi huohuo usio na mipaka kwenye maoni yao tu kama yanavyoungwa mkono na wale wote wanaowazunguka, au ambao wana tabia ya kutofautiana: kwani katika uwiano wa mtu kutaka kujiamini katika uamuzi wake pweke, mara nyingi hatulii, kwa imani inayojitokeza kuhusu kutokuwa na uaminifu wa “dunia” kwa ujumla.  Na kwa hilo mtu binafsi, dunia ina maana ya sehemu yake ambayo anakutana nayo; upande wake, dhehebu lake kanisa lake, tabaka la jamii yake: kwa ulinganisho mtu anaweza kuitwa mkarimu na kiburi ambaye kwake inaweza kumaanisha  lolote pana kama nchi yake au umri wake mwenyewe.  Hata imani yake katika haya mamlaka ya pamoja hayatingishiki kwa kutambua kwamba vizazi vingine, nchi nyingine, madhehebu mengine, makanisa, matabaka na vyama vimefikiri na hata hivi sasa vinafikiri kinyume chake.  Hukabidhi madaraka kwenye dunia yake mwenyewe jukumu la kuwa katika usahihi dhidi ya dunia za uasi za watu wengine na katu haimsumbui kwamba ajali tu imeamua ipi katika hizi dunia nyingi ni lengo la utegemezi wake, na kwamba sababu hizohizo zinazomfanya mtu wa Kanisa katika London, zingeweza kumfanya Budda au ufuasi wa Konyayusashi katika Peking.  Hata hivyo, kuna ushuhuda ndani yake, kama kiasi chochote cha hoja kinavyoweza kudhihirisha kwamba vizazi havina tena uhaikika kuliko watu binafsi; kila kizazi kikiwa kimepata kuwa na mawazo mengi ambayo vizazi vilivyofuatia havikuona uongo tu bali upuuzi; na ni uhakika kwamba mawazo mengi, hivi sasa ya jumla yatakataliwa na vizazi vijavyo, kama ilivyo kwamba mengi mwanzo yakiwa ya jumla hukataliwa na kizazi cha sasa.

 

Katazo lenye uwezekano wa kutolewa kwenye hoja hii, pengine lingechukua umbo kama ifuatavyo.  Hakuna dhana kubwa ya kutokuwa na uhakika katika kukataza kueneza kwa kosa, kuliko katika kitu kingine chochote kinachofanywa na mamlaka ya umma kuhusu uamuzi wake wenyewe na wajibu.  Uamuzi hutolewa kwa watu ili waweze kutumia.  Kwa vile unaweza kutumiwa kimakosa, je, watu waambiwe hawapaswi kuutumia kabisa?  Kukataza kile wanachofikiri kina madhara, hakudai kupata msamaha kutokana na kosa, lakini kutimiza daraka linalowapasa ingawa linaweza kuwa na kosa, la kutekeleza ushawishi wa kufanya kwa makini.  Iwapo tusingekuwa tunatekeleza kwa mujibu wa mawazo yetu, kwa vile unaweza hayo pengine si sahihi, tungeacha maslahi yetu yote bila ya kutunzwa, na majukumu yetu yote kutokutekelezwa.  Katazo ambalo linahusika na mwenendo wote, haliwezi kuwa katazo halali kwenye mwenendo wowote mahususi.  Ni wajibu wa serikali na watu binafsi kuunda mawazo ya kweli kabisa wanayoweza kuyaunda kwa uangalifu na kutayalazimisha kwa wengine ila tu iwapo wana uhakika kabisa wa kuwa sahihi.  Lakini kama wana uhakika (wanaofikiri hivyo wanaweza kusema), si dhamiri bali uwoga kunywea kutekeleza kutokana na mawazo yao, na kuruhusu dhana ambazo kwa uhakika kabisa wanadhani ni hatari kwa ustawi wa binadamu, ama katika maisha haya au maisha mengine, kusambazwa nje bila ya kikwazo kwa sababu watu wengine, katika nyakati ambazo hazikuwa na mwanga wa kutosha, wana mawazo ya kuteswa ambayo hivi sasa yanaamuliwa kuwa kweli.  Tuwe waangalifu, inaweza kusemwa, kutofanya kosa lilelile: lakini serikali na mataifa yamefanya makosa katika mambo mengine, ambayo hayakataliwi kuwa masomo yanayofaa kwa utekelezaji wa mamlaka: wanapanga kodi mbaya, wanapigana vita visivyo vya haki.  Hivyo, tusitoze kodi na chini ya uchokozi wowote ule tusipigane vita?  Watu na serikali lazima watende kwa mujibu wa uwezo wao wa hali ya juu.  Hakuna kitu kama uhakika halisi, lakini kuna uhakika wa kutosha kwa madhumuni ya maisha ya binadamu.  Tunaweza na lazima kufikiri wazo letu kuwa kweli kwa mwongozo wa mwenendo wetu wenyewe: na si kubadili tena wakati tunapowakataza watu wabaya wanapoipotosha jamii kwa kueneza mawazo tunayoyadhania kuwa potofu na yanayodhuru.

 

Najibu kwamba ni kusadiki mengi mno.  Kuna tofauti kubwa kati ya kudhania wazo kuwa kweli kwa sababu kwa kila fursa ya kushindana, haijakanushwa na kusadiki ukweli wake kwa nia ya kutoruhusu kukanushwa kwake.  Uhuru kamili wa kukuza na kukanusha wazo letu ndio hali inavyotuhalalisha katika kusadiki ukweli wake kwa madhumuni ya vitendo; na katika hali yoyote ile nyingine, binadamu mwenye akili zake hawezi kuwa na uhakika wowote wa urasimu wa kuwa sahihi.

 

Tunapozingatia ama historia ya maoni, au mwenendo wa kawaida wa maisha ya binadamu, kwa kitu gani kinachopaswa kudhaniwa kwamba kimoja na zaidi kuliko mengine?  Hakika, si kwa nguvu za asili za welewa wa binadamu; kwani kwa suala lolote lisilojidhihirisha kuna watu tisini na tisa wasio na uwezo kabisa wa kutolea maamuzi, kwani mtu mwenye uwezo, na uwezo wa mtu wa mia ni wa kulinganisha tu: wengi wa watu mashuhuri wa kila kizazi kilichopita walishikilia mawazo ambayo hivi sasa yanajulikana kuwa makosa, na walifanya au kuthibitisha vitu vingi ambavyo hivi sasa hakuna mtu atakayevitetea.  Kwa nini basi kwa ujumla kuna kuzidi miongoni mwa mawazo ya kirazimi na mwenendo wa kirazini?  Iwapo kweli kuna huku kuzidi – ambako lazima kuwepo isipokuwa tu iwapo, na siku zote imekuwa hivyo katika hali ambayo ni sawa na yenye kukata tamaa – ni kutokana na ubora wa akili ya binadamu, chanzo cha kila kitu kinachoheshimika katika binadamu ama kama kiumbe chenye akili au maadili, yaani, kwamba makosa yake yanarekebishika.  Ana uwezo wa kurekebisha makosa yake, kwa majadiliano na uzoefu.  Si kwa uzoefu peke yake.  Lazima pawepo na majadilinao, kuonyesha jinsi ambavyo uzoefu unapaswa kufasiliwa.  Mawazo na vitendo potofu, taratibu hutoa nafasi kwa ukweli na hoja: lakini ukweli na hoja ili kuweza kuzalisha athari yoyote akilini lazima viletwe mbele yake.  Ukweli mchache sana unaweza kueleza hadithi yao wenyewe, bila ya kutoa maana yake.  Hivyo, nguvu na thamani yote ya maamuzi ya binadamu, kutegemeana na sifa moja, kwamba inaweza kufanywa kuwa sahihi wakati ambapo ni kosa, utegemezi inaweza kuwekwa kwake pale tu ambapo wakati wote njia za kusawazisha ziko karibu.  Katika suala la mtu yeyote ambaye maamuzi yake unahitaji hasa kujiamini, imekuwaje hivyo?  Kwa sababu ameweka akili yake wazi kwa ukosoaji wa maoni na mwenendo wake.  Kwa sababu imekuwa kawaida yake kusikiliza yote yale ambayo yangeweza kusemwa dhidi yake; kunufaika nacho kwa kadiri ilivyokuwahaki, na kujielezea kinagaubaga na wakati mwingine kuwaeleza watu wengine, dhana yenye kosa ya kile kilichokuwa cha kiuongo.  Kwa sababu amehisi kwamba njia pekee ambamo binadamu anaweza kufanya mkabala kufahamu somo lote, ni kwa kusikia kinachoweza kusemwa kukihusu na watu wa kila aina za mawazo na kutafiti aina zote ambamo inaweza kutazamwa na kila mhusika wa kumbukumbu.  Hakuna mtu wa busara aliyepata hekima katika njia yoyote ile ila hii; wale haiko katika asili ya akili ya binadamu kuwa mwenye hekima katika namna nyingine yoyote.

 

Tabia imara ya kusahihisha na kukamilisha wazo lake mwenyewe kwa kulilinganisha na lile ya wengine, umbali kutaka kusababisha wasiwasi na kusita katika kuitekeleza, ni msingi pekee thabiti kwa utegemezi wa haki: kwani, kuwa mtambuzi wa hayo yote kunaweza, walau ni dhahiri, kusemwa dhidi yake, na baada ya kuchukua msimamo wake dhidi ya wapinzani kwa kujua kwamba ametafuta mikamo na matatizo, baada ya kuvikwepa, na haikuzuia mwanga ambao unaweza kumwagwa kwenye somo kutoka sehemu yoyote – ana haki ya kufikiri uamuzi vizuri zaidi kuliko ule wa mtu yeyote, au wingi wowote, ambao hawakupitia mchakato wa aina hiyohiyo.

 

Si mzigo mkubwa kutaka kwamba wenye busara zaidi miongoni mwa binadamu, wale wenye haki ya kuamini uamuzi wao wenyewe, kuona lazima kuthibitisha kutegemea kwao upelekwe na mkusanyo anuwai wa watu binafsi wengi wenye hekima na wapumbavu wachache, wanaoitwa umma. Mojawapo ya makanisa yasiyo na uvumilivu kabisa, Kanisa la Kiroma hata kwenye uingizaji wa katika utakatifu wa kikristo, anakubali na kumsikiliza kwa utulivu “wakili wa uovu.”  Inaelekea mtu aliye mtakatifu kuliko wote hawezi kukubaliwa kuingizwa katika heshima za baada ya kufa, hadi hapo ambapo yote yale ambayo shetani angeweza kusema dhidi yake inajulikana kama yaliyopimwa.  Iwapo hata falsafa ya Newton haikuruhusiwa kusaiiliwa, binadamu wasingeweza kuhisi kama uthibitisho uamili ya ukweli wake kama wanavyoujua.  Imani ambazo tuna haki nazo hazina ulinzi wa kutegemea, ila karibisho lililopo la dunia nzima kuzithibitisha kutokuwa na msingi.  Iwapo changamoto hii haikubaliwi, au inakubaliwa na jaribio hilo linashindwa, bado tuko mbali vya kutosha kutoka uhakika; lakini tumefanya kadiri tunavyoweza kiasi kwamba hali iliyopo ya mantiki ya binadamu inakubali; hatukutekeleza chochote ambacho kingeweza kumpa ukweli nafasi ya kutufikia: iwapo orodha hizo ziliwekwa wazi, tunaweza kutegemea kwamba iwapo kuna ukweli bora zaidi, utaonekana wakati akili ya binadamu inaweza kuipokea, na kwa hivi sasa tunaweza kutegemea kuhusu kupata mkabala wa aina hiyo kwa ukweli, kama inavyowezekana katika siku yetu wenyewe.  Hiki ndicho kiasi cha uhakika tunachoweza kutegemea kuwa tumekipata kwa kuweza kuwa na kosa, na hii njia pekee ya kufikia.

 

Ni ajabu kwamba watu wanaweza kukubali uhalali wa hoja kwa ajili ya mjadala huru, lakini wakakataa “kusukumwa kwao pembezoni”, wasione kwamba isipokuwa kama sababu ni nzuri kwa kadhia isiyo na kadri, si nzuri kwa kadhia yoyote.  Ajabu kwamba mimi nadhani kwamba hawadhani kutoweza kukosa, wanapokiri kwamba kuwepo na mjadala huru kwenye mada zote ambazo zinaweza kuwa za mashaka lakini wanadhani kwamba kanuni au dhana mahususi zikatazwe kusailiwa kwa sababu ni hakika mno, yaani kwasababu wana uhakika kwamba ni hakika.  Kuliita pendekezo lolote kuwa hakika, iwapo kuna mtu ambaye angeukana uhakika wake kama akiruhusiwa, lakini nami haruhusiwi, ni kudhani kwamba sisi wenyewe na hao wanaokubaliana nasi ni majaji wa uhakika, na majaji bila ya kumsikiliza upande mwingine.

 

Katika ulimwengu wa sasa – ambao umeelezwa kama “maskini wa imani, lakini unaogopa shuku” [*] – ambamo watu wanahisi hakika, si kwa vile inawazo yao ni kweli, kwa vile hawapaswi kujua wafanye nini bila ya hayo – madai ya wazo kulindwa dhidi ya shambulio la umma hayategemei sana kuhusu ukweli, kama umuhimu wake kwa jamii.  Inadaiwa kwamba imani fulanifulani, muhimu sana licha ya kusema ya lazima kwa maisha, kwamba ni wajibu wa serikali kutetea hizo imani, kama kulinda maslahi mengine yoyote ya jamii.  Katika kadhia ya umuhimu wa aina hiyo, na moja kwa moja katika mpangilio wa jukumu lao inadaiwa kitu pungufu ya kutokuwa na kosa kunaweza kusababisha na hata kubana serikali kufanya kazi kwa maoni yao, ikithibitisha na maoni ya jumla ya ubinadamu.  Pia, mara nyingi hoja inatolewa kwamba, na pia inafikiriwa mara nyingi watu wabaya tu ndio wangependa kudhoofisha hizi imani za kutia afya njema; na inafikiriwa hakuwezi kuwa na tatizo katika kuzuia watu wabaya na kukataza kile ambacho watu wa aina hiyo wangependa kufanya.  Aina hii ya kufikiri hufanya uhalali wa ukwazo kuhusu majadiliano si ukweli wa dhana bali umuhimu wake; hujisifu mno yenyewe kwa njia hivyo kukwepa majukumu ya kudai kuwa jaji asiyeweza kuwa na kosa la maoni: Lakini wale wanaojiridhisha wenyewe hawatambui kwamba dhana ya kutoweza kufanya kosa ni kuhamisha tu kutolea hoja moja hadi nyingine.  Umuhimu wa wazo ni swala lake la wazo, hana linalopingika lililo wazi kwa mjadala na linalohitaji mjadala kama wazo lenyewe.  Kuna haja ilele ya jaji asiyeweza kufanya kosa la maoni kuamua wazo kuwa la kudhuru, kuamua kuwa kosa, ila tu kama wazo likilaumiwa lina fursa kamili ya kujitetea.  Na haitasaidia kusema kwamba mwasi anaweza kuruhusiwa kudumisha manufaa ya kutokudhuru kwa wazo lake, ingawaje anakatazwa kudumisha ukweli wake.  Ukweli wa wazo ni sehemu ya umanufaa wake.  Kama tungejua iwapo inafaa na kwamba pendekezo linaaminiwa, inawezekana kutojumuisha fikirio la iwapo ni kweli au la?  Katika wazo hili, si la watu wabaya, bali la watu bora hakuna imani inayopingana na ukweli inayoweza kuwa ya manufaa hasa: na unaweza kuzuia aina hiyo ya watu kutokana na kutoa hoja ya ombi hilo wanapopewa adhabu kwa kukana baadhi ya dhana ambazo wanaambiwa zinafaa lakini wanazoamini ni uwongo?  Wala walio katika upande wa maoni ya kupokea, hawashindwi kuchukua faida ya ombi hili; huwaoni wakishughulikia swali la maana kama kwamba linaweza kuchomolewa kutoka kwenye ukweli huo: kinyume chake iko juu ya yote kwa sababu ni dhana ya b”ukweli”b kwamba maarifa au imani yake inaaminiwa kuwa lazima.  Hakuwezi kuwa na mjadala wa haki wa swali la umuhimu, wakati hoja iliyo muhimu sana inaweza kutumiwa upande mmoja, lakini sio upande mwingine.  Na ukweli ni kwamba wakati sheria au hisia za umma haziruhusu  ukweli wa wazo kubishaniwa, ni wavumilivu kidogo tu na kukana umuhimu wake.  Sanasana wanachomruhusu ni kupunguza uhamilifu wa muhimu wetu, au hatia chanya ya kuikataa.

 

Ili kubainsiha kikamilifu madhara ya kukataa kusikilizwa kwa maoni kwa sababu sisi, katika hukumu yetu wenyewe, tunawahukumu, itakuwa inafaa kuupanga mjadala kwenye hadhia; nachagua kwa upendeleo kadhia ambazo sizipendi kabisa – ambamo hoja dhidi ya uhuru wa maoni katika hoja ya ukweli na katika ile ya manufaa, inahesabiwa kuwa yenye nguvu kabisa.  Acha maoni yanayotiliwa shaka yawe imani katika Mungu na katika hali ya siku za baadaye, au maadili yoyote yale ya dhana izlizopokewa pamoja na uadilifu.  Kupigana vita katika aina hiyo ya uwanja, hutoa faida kubwa kwa uhasama usio wa haki kwa kuwa takuwa na uhakika kusema (na wengi wasio na matamanio watasema kindanindani).  Hizi ndio dhana msizoziona kuwa na uhakika wa kutosha kuchukuliwa chini ya ukuzi wa sheria?  Je, imani katika Mungu mojawapo ya maoni ya kuhusi uhakika ambao unachukulia kutokiweza kukosa?  Na shughuli ya kuamua swali hilo kwa wengine bila ya kuwaruhusu kusikia kinachoweza kusemwa katika upande wa pingamizi.  Na ninalaani na kuchukia kwa nguvu kujidai huku kama kukifanywa kwa upande wangu wa kutiwa hatiani kwa taadhima.  Ushawishi wa mtu hata uwe chanya kiasi gani, sio tu matokeo ya ongo bali yenye kudhuru, – sio tu matokeo yenye kudhuru, bali kutumia miemo ambayo yote yanailaani), uovu na kufuru ya wazo; hata hivyo kama ni kufuatia hukumu ya binafsi; ingawa inaungwa mkono na hukumu ya umma wa nchi yake au hivi hirimu lake, anazima wazo lisisikilizwe katika utetezi anaodhani hauwezi kuwa na makosa.  Na kutokana na fikra ya kukataa kiasi au hatari kidogo kwa sababu wazo linaitwa uovu au kufuru hii ni kadhia ya nyingine zote ambamo ni hatari sana.  Haya ni matukio ambamo watu wa kizazi kimoja hufanya hayo makosa mabaya ambayo yanasisimua inastaajabu na chukizo la vizazi vya baadaye.  Ni miongoni mwa hao ambamo tunaona mfano za kukumbuka katika historia, wakati mkono wa sheria umetumika kutokomeza watu bora na dhana za kiadilifu.  Pamoja na ufanisi unaosikitisha kwa watu, ingawa baadhi ya dhana zimeishi (kama katika dhihaka) kumwomba Mungu katika utelezi wa mwenendo wa aina hiyohiyo kuelekea kwa hao wenye maoni tofauti kutoka kwao, au kutoka fasili yao waliyopata.

 

Binadamu hawezi kukumbushwa mara nyingi, kwanza hapo zamani alikuwepo mtu aliyeitwa Socrates, ambaye kati yake na mamlaka ya kisheria na wazo la umma wakati wake, kulifanyika mgongano wa kukumbukwa.  Akiwa amezaliwa katika kizazi na nchi iliyojawa na utukufu binafsi, mtu huyu ameletwa kwetu na wale ambao wakimfahamu vizuri yeye na kizazi, kama mtu mwadilifu kabisa ndani yake; ambapo sisi tunamfahamu kama mkuu wa watu sampuli ya awali na watu waliofuatilia wa maadili, chanzo cha usawa wa msukumo bora wa Plato, na busara ya mawazo ya kuleta faida ya Aristotle, “i maestri di color che sanno” [*], kichwa cha spring mbili za uadilifu kama za falsafa nyingine. Huyu bwana anayetambulika na watu wote mashuhuri wanaofikiri sana ambao wamepata kuishi – ambao umaarufu wao bado unakua baada ya zaidi ya mwaka elfu mbili anayezidi majina yote mengine yanayolifanya jiji lake maarufu alilozaliwa – aliuawa na watu wa nchini mwake, baada ya hukumu ya mahakama kwa kufuru uovu.  Kufuru katika kukana miungu inayotambuliwa na Dola; mshtaka wake alidai (tazama Apologia) kwamba hakuamini katika miungu yoyote kabisa.  Uovu kwa kusimamia dhana zake, vyanzo yake, “mpotoshaji wa vijana” [+]. katika hivi sasa binadamu wanazichukulia hizi shughuli za kujutia, hususan hao wawili wa pili wanawageuza kuwa si wa haki hata kidogo katika hukumu yao ya watendaji wasio na furaha.  Kwa mwonekano wote, hawa hawakuwa watu wabaya – si wabaya kuliko watu walivyo kwa kawaida, lakini kinyume chake; watu waliokuwa nayo kiukamilifu au zaidi ya kipimo uamili; kidini, kiadilifu, na hisia za kiza baada ya wakati na watu wao: aina ya watu, nasi tukiwemo, wakati wote, wana kila nafasi ya kupita katika maisha bila ya lawama na wakiheshimiwa.  Kuhani mkuu aliyekodisha mavazi yake wakati maneno yalipotamkwa, ambavyo, kwa mujibu wa mawazo yote ya nchi yake, yalifanyiza hatia mbaya kabisa kwa mawazo yote yalikuwa kweli katika hofu kuu na uchungu, kama ujumla wa watu wanaoheshimika na wa dini hivi sasa walivyo katika hisia za kidini na kiuadilifu wanazotabiri na wengi wao hivi sasa wanatetemeka kwa mwenendo wake, iwapo, kama waliishi katika wakati wake na kujaliwa wayahudi ambao wangefanya kama alivyofanya. Wakristo wenye imani sahihi ambao wanajaribu kufikiri kwamba wale waliowapiga mawe mashuhuda wa mwanzo wa dini lazima walikuwa watu wabaya zaidi kuliko wao wenyewe, wanapaswa kukumbuka kwamba mmojawapo wa wadhalimu alikwua Mtakatifu Paulo. [+]

 

Tuongeze mfano mmoja zaidi, unaovutia kuliko mifano yote, iwapo mvuto wa kosa unapimwa kwa hekima na maadili ya huyo anayeangukia humo.  Iwapo mtu yeyote yule aliyepagawa na madaraka alikuwa na sababu za kujifikiria kuwa bora kabisa na mwongofu miongoni mwa hirimu wake, alikuwa Mfalme Marcus Aurelius.  Mfalme peke wa dunia yote iliyostaarabika maishani kote alidumisha haki safi, lakini jambo ambalo halikutegemewa katika malezi yake ya uvumilivu kabisa, moyo mwororo kabisa.  Kushindwa kuchache ambako kunasemekana kutokana naye, kote kulikuwa katika upande wa huruma: wakati ambapo maandiko yake, matokeo ya uadilifu wa hali ya juu ya akili ya kizamani, yanatofautiana kidogo sana kimtazamo, iwapo kuna utofauti, kutoka maisha mafundisho ya kipekee ya Kristo.  Mtu huyu, Mkristo katika yote na maana halisi ya  imani kuliko karibu mamlaka yoyote halisi ya Kikristo ambayo tangu wakati  huo yametawala, yakiwatesa Wakristo.  Akiwa amelelewa juu kabisa ya mafanikio yoyote yaliyopita ya binadamu, kwa akili wazi isiyo na kipingamizi, na tabia iliyomwongoza kujiunganisha katika maandiko yake ya kiuadilifu ya ukamilifu wa Kikristo, hata hivyo alishindwa kuona kwamba Ukristo ulikuwa uwe mzuri na wala si uovu kwa dunia, pamoja na kazi zake ambazo zilimwingia sana.  Jamii iliyokuwepo aliufahamu kuwa katika hali ya kusikitisha.  Lakini pamoja na kuwa hivyo, alidhani aliona kwamba ilikuwa imefungwa pamoja na kuzuiliwa kuwa mbaya zaidi. Kwa kuamini na unyenyekevu wa utukufu wa Mungu uliopokelewa, kama mtawala wa binadamu, aliona ni wajibu wake kutoidhuru jamii katika vipandevipande; hakuona vipi hana viungo vyake vilivyopo vingeondolewa, vingine vyovyote vile vingeweza kuundwa ambavyo vingefungwa tena pamoja.  Kwa uwazi, dini mpya ililenga kuvivunja viungo hivi ila tu kama ulikuwa wajibu kuitumia dini hiyo, ulielekea kuwa wajibu wake kuinyamazisha.  Kwa kiasi ambacho wakati huo teolojia ya Mkristo kwake haikuelekea kuwa kweli au ya asili ya Utakatifu: kwa kadiri ambavyo hii historia ya ajabu ya Mungu aliyesulubiwa haikuw aya kuaminika kwake, na mfumo ambao ulidai kutegemea kikamilifu msingi kwake ambao hauaminiki hata kidogo, isingeweza kutabiriwa naye kuwa ule wakala wa ukarabati ambao, baada ya kuzuiwa kote, hakika umethibitika kuwa mwanafalsafa wa kiungwana na mpole kuliko wote, chini ya hali ya jukumu zito aliamuru mateso ya Ukristo.  Kwa mawazo yangu huu ni miongoni mwa ukweli wa kusikitisha sana katika historia yote.  Ni wazo chungu, Ukristo wa dunia kwa jinsi gani ungekuwa, iwapo imani ya Kikristo ingetumika kama dini ya ufalme chini ya uangalizi wa Marcus Aurelins badala ya ule wa Konstantino.  Lakini, kwa kiasi hichohicho, isingekuwa haki kwake na ingekuwa uongo kwa ukweli kukana kwamba hakuna hata ombi linaloweza kusikiwa kwa kuadhibu mafundisho dhidi ya Ukristo kulikuwa kutaka kwa Marcus Aurelius kuadhibu, kama alivyofanya, uenezaji wa Ukristo.  Hakuna Mkristo aliyeamini kwa uthabiti hasa kwamba Ukana Mungu ni uongo na unaelekea kuiangamiza jamii, kuliko Marcus Aurelins alivyoamini mambo hayohayo ya Ukristo: Yeye, ambaye kati ya watu wote waliokuwa wakiishi wakati huo, angeweza kufikiriwa kwenye uwezo kuliko wote wa kutambua.  Isipokuwa tu kama yeyote yule anayeikubali adhabu kwa ajili ya kutangaza rasmi maoni, anajidanganya mwenyewe kwamba yeye ana busara zaidi na mtu bora zaidi kuliko Marcus Aurelins – anayefahamu kwa undani zaidi katika busara za wakati wake, mwenye uwezo zaidi  katika akili juu yake – aliye mkweli zaidi katika utafutaji wake wa ukweli, au kwa lengo moja katika upendo mkubwa kwake baada ya kupatikana; – acha aache dhanio la kuwa na uhakika wa pamoja yeye na umati, jambo ambalo Antoninus alilifanya kwa matokeo ya kusikitisha.

 

Akiwa na welewa wa kutowezekana kwa kutetea matumizi ya adhabu kwa kudhibiti maoni yasiyokuwa ya kidini, kwa hoja yoyote ambayo haitamridhisha Marcus Antoninus, maadui wa uhuru wa dini wanapobanwa sana, mara chache hulikubali tokeo hili na kusema, pamoja na Dkt. Johnson, kwamba watesaji wa Ukristo walikuwa sahihi; kwamba mateso ni msukosuko ambao kwao ukweli unapaswa kupitia na siku zote hupita kwa mafanikio, adhabu za kisheria mwishoni yakiwa hayana nguvu dhidi ya ukweli, ingawaje wakati mwingine zikiwa za manufa dhidi ya makosa ya utundu.  Hii ni aina ya hoja kwa ajili ya uvumilivu wa kidini, ambao haupaswi kupitwa bila ya kuonekana.

 

Nadharia inayodai kwamba ukweli unaweza kuteswa kihaki kwa sababu mateso hayana uwezekano wa kuudhuru ukweli, haiwezi kushtakiwa kwa kuwa mgomvi kwa makusudi kwa upokeaji wa ukweli mpya; lakini hatuwezi kutukuza ukarimu wa utendaji wake shughuli na watu ambao watu wanadai kwa ajili yao.  Kuigundulia dunia kitu ambacho kinauhusu sana, ambacho hapo awali ulikuwa haukitambui; kuthibitishia kwamba ulikuwa umekosea kuhusu maslahi ya kidunia au kiroho, ni huduma muhimu kama binadamu anavyoweza kuwapatia binadamu wenzake, na katika kadhia fulanifulani, kama katika zile za Wakristo wa mwanzoni na katika enzi za wanamageuzi, wale wanaofikiri na Dkt. Johnson wanaiamini kuwa zawadi iliyo tunu kubwa kabisa ambayo wanaweza kupatiwa binadamu.  Kwamba watunzi wa manufaa mazuri kama hayo wazimishwe na ushujaa; kwamba malipo yao yashughulikiwe kama kosa la jinai bayana sana, si juu ya nadharia hii, kosa la kusikitisha na mkosi, ambao ubinadamu lazima uomboleze katika nguo za magunia na majivu, lakini hali ya kawaida na iliyo halali.  Kwa mujibu wa mafundisho haya ya dini, mpendekezaji ukweli mpya anapaswa asimame, kama ilivyokuwa katika sheria za Locrians, mpendekezaji wa sheria mpya, na mnyororo shingoni mwake, kukazwa  mara moja iwapo baada ya kusikiliza sababu zake, makutano ya umma yatumie pendekezo hili hapohapo.  *  Watu wanaoitetea hali hii ya kuwatendea watenda mema, haiwezi kufikiriwa kuweka thamani kubwa kwenye faida hiyo; na uamini mtazamo huu wa somo umejifunga zaidi kwenye aina ya watu wanaodhani kwamba ukweli mpya, unawezekana ulitamaniwa wakati fulani, lakini hivi sasa umetushosha.  Lakini, hakika, siku zote ukweli huyashinda mateso, ni mojawapo ya uongo unaopendeza ambao binadamu hurejea mmoja baada ya mwingine hadi unafika katika sehemu za kawaida mno, lakini ambazo historia inazikataa.  Historia hujiunga na matukio ya ukweli ulioandikwa na mwendesha mashtaka.  Iwapo haugandamizwi milele, unaweza kurudishwa nyuma kwa karne na karne.  Kuongea kuhusu mawazo ya kidini tu: Mageuzi yalitokea ghafla walau mara ishirini kabla ya Luther na yalivunjwa.  Arnold wa Brescia alivunjwa.  Fra Dolcino alivunjwa.  Savonarola alivunjwa.  Akina Albegois walivunjwa. Akina Vondois walivunjwa.  Akina Lollards walivunjwa.  Wahisanti walivunjwa.  Hata baada ya kizazi cha Luther popote pale mateso yaling’ang’aniwa, yalifanikiwa.  Nchini Spain, Italy, Flanders, Ufalme wa Austria, upinzani ulitokomezwa na Uingereza pia kungekuwa na uwezekano wa kuwa hivyohivyo, iwapo Malkia Mary angekuwa anaishi au kama Malkia Elizabeth angekufa. Siku zote mateso yamefanikiwa, isipokuwa pale ambapo waasi walikuwa sehemu yenye nguvu kiasi kwamba wasingeweza kuteswa kiasi cha kuleta athari.  Hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kutia shaka kwamba ukristo ungeweza kuangamizwa katika ufalme wa Roma.  Ulienea na kuwa wenye athari juu ya wengine, kwa sababu mateso yalikuwa ya mara chache, yakidumu muda mfupi na yaliyotenganishwa na vipindi virefu vya karibu propaganda isiyobughudhiwa.  Ni sehemu ya hisi za moyoni zisizo na kazi kwamba ukweli, kama ukweli tu, una nguvu ya asili iliyokatazwa kwa kosa la kuwepo dhidi ya shina na hatari.  Watu hawana tena dhana ya ukweli kuliko jinsi walivyo na raghba ya kosa, na matumizi ya kutosha ya kisheria au hata ya adhabu za kijamii kwa ujumla yatafanikiwa katika kusimamisha uenezaji wa mojawapo.  Faida halisi ambayo ukweli unao, ambayo ni huu, kwamba wazo linapokuwa kweli linaweza kutokomezwa mara ya kwanza, ya pili, au mara nyingi lakini katika vizazi kwa ujumla watapatikana watu wa kuligundua tena hadi uibukaji wake mmoja unaangukia kwenye wakati ambapo kutokana na mazingira  mazuri unatoroka mateso hadi hapo utakapopata nguvu ya kukabiliana na majaribio yafuatayo ya kuligandamiza.

 

Itasemwa kwamba hivi sasa hatuwaoni waanzilishi wa mawazo mapya.  Sisi si kama baba zetu waliowachinja mitume, sisi hata tunawajengea makaburi ya mawe.  Ni kweli, hivi sasa hatuwaui waasi; na kiwango cha adhabu inayotolewa ambacho pengine hisia za kisasa zingevumisha, hata dhidi ya mawazo ya makuruhu kabisa, hazitoshi kuwavunjavunja.  Lakini tusijidanganye kwamba tayari tuko huru hutokana na hata doa la mateso ya kisheria adhabu kwa ajili ya maoni au walau kwa ajili ya kutoa maoni, bado zipo kisheria; na katika siku hizi utiishaji wake si wa mfano mbaya kiasi cha kuzifanya zote kuwa za kushangaza kiasi kwamba siku fulani zinaweza kuhuishwa katika hali kamili. Katika mwaka 1857, wakati wa majira ya joto, katika mahakama zinazosikilizwa na jaji na wazee wa baraza mkoa wa Cornwall mtu mwenye bahati mbaya * anayesemekana kuwa wa mwenendo usiokuwa tofauti katika uhusiano wote wa maisha alihukumiwa kifungo cha jela cha miezi ishirini na mmoja, kwa kutamka na kuandika kwenye lango maneno ya dhambi kuhusu Ukristo.  Ndani ya mwezi huohuo, huko Old Bailey, kwenye matukio mawili tofauti, watu wawili, walikataliwa kama wazee wa Baraza na mmojawao alitukanwa viabaya na jaji na mmojawapo wa mawakili kwa sababu walitamka kwa uaminifu kwamba hawakuwa na imani ya kiteolojia, na wa tatu, mtu wa nchi ya kigeni, kwa sababu hiyohiyo alinyimwa haki dhidi ya mwizi.  Ukataaji huu wa fidia ulitokea kutokana na dhana ya kisheria, kwamba hakuna mtu anayeweza kuruhusiwa kutoa ushahidi katika mahakama ya sheria, ambaye hatangazi imani katika Mungu (mungu yeyote yule anatosha) na katika siku za baadaye za dola, ambayo ni sawa na kuwatangaza watu wa aina hiyo kuwa mhalifu, wasiojumlishwa kwenye ulinzi wa mabaraza; ambao sio tu wanaweza kuibiwa au kushambuliwa bila hofu ya kuadhibiwa wala kuumia, iwapo hakuna mtu mwingine ila wao tu, au watu wa mawazo yanayofanana, lakini mwingine yeyote yule anaweza kuibiwa  au kushambuliwa na kuadhibiwa au kuumia, iwapo uthibitisho wa ukweli unategemea ushahidi wao.  Dhana ya msingi wa jambo hili, ni kwamba hapo hakuna faida kwa mtu asiyeamua katika hali ya baadaye; pendekezo linabashiri  ujinga mwingi wa historia katika hao wanaoridhia (kwa vile ni kweli kihistoria kwamba kiasi kikubwa cha makafiri katika vizazi vyote wamekuwa watu wa heshima iliyojipambanua na utukufu); na isingedumishwa na yeyote yule aliyekuwa na welewa wa chini kabisa wa wangapi wa watu katika sifa kubwa kabisa, kwa maadili na kwa mafanikio wanajulikana vizuri, walau kwa marafiki wao wa karibu sana, kuwa waumini.  Pamoja na hayo, kanuni yenyewe ni kifo na huharibu msingi wake yenyewe.  Kwa kisingizio kwamba wakana mungu lazima wawe waoga, inakubali ushuhuda wa wakawa mungu wote walio tayari kudanganya, na anakataa wale tu walio na wanaojasiri fedheha ya kukiri imani inayochukiwa kuliko kukubali uwongo, kanuni ya kujihukumu ya upuuzi kadiri inavyohusu nia yake iliyotabiriwa, inaweza kutekelezwa tu kama ishara ya chuki, kumbukumbu za mateso; mateso, pia kuwa na upekee, kwamba sifa ya kufanya ni kuthibitishwa dhahiri kutoistahili.  Kanuni hiyo pamoja na nadharia inayoelekeza ni matusi kwa waumini kama ilivyo kwa makafiri.  Kwani yule asiyeamini katika hali ya baadaye, lazima anadanganya, inafuatia kwamba hao wanaoamini wamefanya kuzuiliwa tu kudanganya, iwapo wanazuiwa kwa woga wa jahanamu.  Hatutawatendea waandishi na watenda maovu wa kanuni maumivu ya kudhani kwamba dhana waliyoiunda ya maadili ya Ukristo imechukuliwa kutoka kwenye utambuzi wao wenyewe.

 

Hakika, haya, ni dhihaka na masalio ya mateso na yanaweza kufikiriwa kutokuwa ishara ya kutaka kutesa, kama mfano wa upungufu wa mawazo wa mara kwa mara wa mawazo ya Kiingereza, ambayo huwafanya wachukue furaha isiyo na maana katika kuteka kwa dhati kanuni mbaya, pale ambapo si mbaya za kutosha kuhitaji kuitekeleza hasa.  Lakini kwa huzuni, hakuna usalama katika hali  ya mawao, kwamba kusimamishwa kwa aina mbaya mateso ya kisheria, ambazo zimekuwepo kwa karibu kipindi cha kizazi, zitaendelea.  Katika kipindi hiki, hali ya ukimya wa utaratibu mara nyingi hutibuliwa na majaribio ya kuchochea uovu wa  zamani, ili kuanzisha mafao mapya.  Kinachojivunia hivi sasa kama uhuishaji wa dini, siku zote katika mawazo yasiyo mapana na yasiyotolewa, walau kama  wa uhakika; na pale palipo na chachu ya kutokuwa na uvumilivu katika hisia za watu, ambazo wakatiwote huvumisha katika matabaka ya kati ya nchi hii, inahitaji kidogo tu  kuwachokoza katika kuwatesa wale ambao hawakuacha kufikiria vyombo sahihi vya matenso * kwani ni hayo – ni maoni ambayo watu hukirimum, na hisia wanazotunza, zikiheshimu wale wanaokana imani wanazoziona muhimu, ambazo huifanya nchi hii isiwe mahali pa uhuru wa makili.  Kwa muda mrefu zamani, madhara makubwa ya adhabu ni kwamba zinainamisha unyanyapaa wa jamii.  Ni unyanyapaa huo ambao unatoa matokeo hasa, na inafaa sana, kwamba utaalamu wa maoni ambao uko chini ya zuri ya kupiga marufuku ya jamii si wa kawaida sana katika Uingereza, kuliko ilivyo katika nchi nyingi nyingine ambazo kukiri kwamba Hoja za Uongobisha hatimisho la adhabu wa sheria.  Kuhusiana na watu wote, isipokuwa wale ambao  mazingira yao yanahusika na fedha huwafanya kuwa huru kutokana na madhumuni mema ya watu wengine, maoni kuhusu mada hii ni yenye kuleta maendeleo yanayotakiwa kama sheria; watu wangeweza hata kufungwa, kama kutajumlishwa katika njia za kupata riziki.  Wale ambao riziki yao imekwishapatikana na hawataki upendeleo kutoka kwa watu walio madarakani; au kutoka kwa vyombo vya watu, au kutoka umma hawana cha kuogopa kukiri waziwazi maoni yoyote, ila kufikiriwa na kuzungumzwa vibaya, na hivi havihitaji tabia yoyote ya ujasiri kuvumilia.  Hakuna nafasi ya rufaa ya ad misericordian kwa niaba ya watu wa aina hiyo.  Lakini ingawa watu hatusababishi uovu sana kwa wale wanaofikiri tofauti nasi, kama ilivyokuwa tabia yetu kufanya hapo zamani, inawezekana kwamba tunajifanyia uovu sana kwa jinsi tunavyowatendea. 

RELATED ARTICLES