Ludwig Lachmann’s, “The Market Economy and the Distribution of Wealth”

Uchumi wa Soko na Mgawanyo wa Utajiri

– Ludwig M. Lachmann, Mtaji, Matarajio, na Mchakato wa Masoko

 

Kila mahali hivi leo katika Dunia huru tunakuta wapinzani wa uchumi wa soko wakikosa hoja za kukubalika.  Hivi karibuni “swala la mipango mikuu” linapoteza sehemu ya heshima ya kale.  Tuna uzoefu mkubwa mno nalo.  Maelezo ya miaka arobaini iliyopita ni ya umbuji mno.

 

Hivi sasa ni nani anayeweza kutia shaka, kama Profesa Mises alivyoeleza miaka thelathini iliyopita, miaka thelathini ya kisiasa inajumuisha afua kila uingiliaji kati wa kisiasa unahitaji uingiliaji kati zaidi kuzuia matokeo ya kiuchumi yasiyoepukika ya hatua ya kwanza yasifanyike?  Nani atakataa kwamba udhibiti wa uchumi unahitaji mazingira ya mfumko wa bei ili ufanye kazi, na leo hii nani hajui athari mbaya za mfumko wa bei unaodhibitiwa?” Hata kama wachumi wengine sasa wamebuni neno la kusifu “mfumko wa bei wa dunia”  ili kuelezea mfumko wa bei wa kudumu tunaoufahamu vizuri wote, haielekei kwamba mtu yeyote amedanganywa.  Haukuhitaji kabisa mfano wa hivi karibuni wa Mjerumani kutuonyesha kwamba uchumi wa soko utajenga utaratibu kutokana vurugu “zinazodhibitiwa kiuendeshaji” hata katika mazingira yasiyofaa.  Aina ya shirikia la kiuchumi linalotokana na ushirikiano wa kujitolea na ubadilishanaji wa maarifa kidunia liko juu ya muundo wowote wa ngazi za madaraka, hata kama katika hilo jaribio la uwiano kwa ajili ya sifa za wale wanaotoa neno la udhibiti lingekuwepo.  Wale ambao hawawezi kujifunza kutokana na sababu na uzoefu walilijua hilo kabla, na wale ambao hawakujua hawaelekei kujifunza hata sasa.

 

Kimechapwa upya kutika Mary Sennholz, ed., On Freedom and Free Enterprise: Essays in Honor of Ludwing Von Misers (New York: D Van Nostrand, 1956.)

 

Wakikabiliwa na hali hii, wapinzani wa uchumi wa soko wamebadili msimamo wao; sasa hivi wanaupinga kuhusu “jamii” badala ya msimamo ya kiuchumi. Wanautuhumu kuwa sio wa haki na kwa hakika hauna ufanisi.  Sasa hivi wanazungumzia sana kuhusu “athari za upotoshaji” za kumiliki mali na wanadai kuwa “kura ya maoni ya soko inayumbishwa na kura ya wengi”.  Wanaonyesha kuwa mgawanyo wa mali unaathiri uzalishaji na mgawanyo wa mapato, kwa kuwa wamiliki wa mali sio tu wanapata “Hisia siziso sawa” za mapato ya jamii, bali utaathiri muundo wa zao la jamii:  vitu vya anasa ni vingi mno na mahitaji muhimu ya lazima ni machache.  Zaidi ya hayo, kwa kuwa wamiliki ndio wawekaji wakubwa wa akiba wanaamua vilevile kiwango cha malimbikizo ya mtaji na hivyo kukuza uchumi.

 

Baadhi ya wapinzani hawa wasingekataa kwa pamoja kwamba kuna namna ambamo mgawanyo wa mali ni matokeo ya ulimbikizaji wa utendaji wa nguvu za kiuchumi, lakini wangeshikilia kuwa ulimbikiza hufanya kazi kwa mtindo wa kuufanya wakati uliopo mtumwa wa wakati uliopita, kipengele kisicho na msingi cha zamani katika wakati uliopo.  Hivi leo mgawanyo wa mapato unapewa sura na mgawanyo wa hivi leo wa mali, na hata kama mali za leo kwa sehemu zililimbikizwa jana, ililimbikizwa kwa mchakato ulioakisi athari ya mgawanyo wa mali wa juzi.  Kimsingi hoja ya wapinzani wa uchumi wa soko inazingatia taasisi ya urithi ambayo, hata katika jamii inayoendelea, tunaambiwa, wamiliki walio wengi wanawiwa mali zao.

 

Hoja hii inaelekea kukubaliwa sana siku hizi, hata na wengi ambao kwa ukweli kabisa wanaunga mkono uhuru wa uchumi.  Watu hao wamekuja kuamini kuwa “ugawanyaji upya wa mali “kwa mfano kupitia majukumu ya kifo yangetamanisha kijamii, lakini bila matokeo ya kiuchumi yanayofaa.  Kinyume chake, kwa kuwa hatua hizo zingesaidia kuuokoa muda uliopo kutoka kwenye “mkoino uliokufa” wa muda uliopita zingesaidia vilevile kurekebisha mapato ya sasa kwa mahitaji ya sasa.  Mgawanyo wa mali ni data za koso, na kwa kubadilisha data tunaweza kubadilisha matokeo bila ya kuingilia utaratibu wa soko!  Unafuatilia kwamba ni wakati tu utakapoambatana na sera iliyobuniwa kuendelea kugawanya mali iliyopo, ndipo mchakato wa soko ungeweza kuwa na matokeo “yanayovumilika kijamii.”

 

Kama tulivyosema, mtazamo huu, unashikiliwa na wengi, hata na baadhi ya wachumi wanaoelewa ukubwa wa uchumi wa soko zaidi ya uchumi wa idhibiti na upingaji wa uingiliaji kati, bali kuchukia kile wanachokiona kama matokeo ya kijamii ya uchumi wa soko.  Wamejiandaa kuukubali uchumi wa soko tu pale ambapo utendaji wake unaambatana na sera hiyo ya ugawanyaji upya.

 

Makala haya yametolewa kwa uhakiki wa msingi wa mtazamo huu.

 

Kwanza kabisa, hoja nzima inasimama kimantiki katika mkanganyiko wa maneno unaotokana na maana yenye utata ya neno “datum”.  Katika matumizi ya kawaida na vilevile katika sayansi nyingi, kwa mfano kwenye takwimu, neno “data” linalomaanisha kitu ambacho kuna wakati, “lilitolewa” kwetu kama watazamaji wa tukio.  Kwa maana hii, bila shaka, ni ukweli ulio wazi kuwa namna ya ugawanyaji wa mali ni datum katika wakati wowote, katika maana ndogo tu ambayo inaonyesha kuwepo na hakuna namna nyingine inayofanya hivyo.  Lakini katika nadharia za mlingano ambazo, kwa uzuri au ubaya, zimekuja kumaanisha sana hivi sasa wazo la kiuchumi na kwa kiasi kikubwa zimetengeneza maudhui yake, neno “datum” limepata maana ya pili na tofauti sana:  Hapa datum maana yake ni hali muhimu ya mlingano, na iliyobadilikabadilika, na “data” kwa pamoja maana yake ni jumla ya masharti ya lazima na yanayotosha ambayo mara tutakavyoyafahamu yote bila zaidi tunaweza kufasiri bei na idadi inayolingana.  Kwa maana ya pili mgawanyo wa mali, pamoja na data nyingine, ungeweza kuwa KIUKILIO, ingawa sio kiukilio pekee, cha bei na idadi ya huduma na bidhaa mbalimbali zilizonunuliwa na kuuzwa.

 

Hata hivyo, litakuwa ni jukumu letu kuu katika makala hii kuonyesha kuwa mgawanyo wa mali sio “data” katika namna hii ya pili.  Mbali na kuwa “kitu kigeugeu huru” cha mchakato wa soko, kinyume chake kinategemea mabadiliko ya nguvu za soko.  Sio lazima kusema, hii sio kukataa kwamba kwa wakati wowote ni miongoni mwa nguvu zinazotengeneza njia ya mchakato wa soko hivi karibuni, lakini ni kukataa kuwa maana ya ugawanyaji kama hivyo unavyoweza kuwa na athari yoyote ya kudumu.  Ingawaje wakati wote mali inagawanywa kwa njia dhahiri, namna ya ugawanyaji hii inabadilika wakati wote.

 

Ni pale tu ambapo namna ya ugawanyaji ingebakia ilivyo muda hadi muda, wakati mali za mtu binafsi zinahamishwa kwa njia ya urithi, ndipo namna hii ingeweza kuitwa nguvu ya uchumi ya kudumu.  Ukweli ni kwamba sio hivyo, mgawanyo wa mali unatengenezwa na nguvu za soko kama lengo na sio nguvu, na kwa vyovyote namna zake zitakavyokuwa hivi leo hivi karibuni zitakuwa kitu cha zamani kisichokuwa na umuhimu.

 

Hata hivyo, mgawanyo wa mali, hauna nafasi katika data za mlingano.  Hata hivyo, kinacholeta maslahi makubwa ya kiuchumi na kijamii sio namna ya mgawanyo wa mali katika wakati fulani, bali namna yake ya kubadilika kwa wakati.  Badiliko hilo, tutaona, hutafuta nafasi yake halisi kati ya matukio yanayotokea katika “njia” yenye matatizo hivyo, kupelekea kwenye mlingano.  Ni jambo lenye “hamasa” hasa.  Ni jambo la kushangaza kwamba kuna wakati umuhimu ulisikika sana wa utafutaji na uendelezaji wa utafiti wa elimu mwendo unapaswa kuamsha shauku ndogo.

 

Umiliki ni dhana ya kisheria inayohusu vitu dhahiri.  Mali ni dhana ya kiuchumi inayohusu raslimali adimu.  Raslimali zote za thamani ni, au zinaonyesha, au kujumuisha vitu, bali sio vitu vyote ni raslimali.  Nyumba zilizohamwa na malundo ya takataka ni mifano dhahiri, kama ilivyo kwa vitu vyovyote ambavyo wamiliki wangevitoa kwa furaha kama wangempata mtu aliyekuwa tayari kuviondoa. Hata hivyo, raslimali za leo zinaweza zisiwe zile za kesho, wakati kitu ambacho hakina thamani leo kinaweza kuwa na thamani zaidi kesho.  Hali ya raslimali vitu kwa hiyo wakati wote ina matatizo na kutegemea kwa kiwango fulani cha kuiona mbele yajayo.  Kitu kinageuka kuwa mali pale tu kinapokuwa chanzo cha mkondo wa mapato.  Thamani yakitu kwa mmiliki, halisi au raslimali, inaonyesha wakati wowote uwezo wake wa kuvuna mapato yaliyokusudiwa.  Badala yake, hili litategemea matumizi ya kitu yanayoweza kugeuziwa.  Umiliki tu wa vitu, kwa hiyo, sio lazima ulete mali; ni matumizi yake yenye mafanikio ndiyo huleta mali.  Sio umiliki bali utumiaji wa raslimali ndio chanzo cha mapato na mali.  Kiwanda cha aiskrimu mjini New York kinaweza kutoa mali kwa mmiliki wake; kiwanda kama hichohicho Greenland ni vigumu sana kuwa raslimali.

 

Katika dunia yenye mabadiliko yasiyotegemewa utunzaji mali wakati wote ni tatizo; na hatimaye inaweza kusemwa kuwa haiwezekani.  Ili kuweza kutunza kiasi kilichotolewa cha mali ambacho kingeweza kuhamishwa kwa urithi kutoka kizazi kimoja kwenda kingine, familia ingepaswa kumiliki raslimali hizo kwa kuwa itavuna mtiririko wa mapato halisi ya kudumu k.v. mkondo wa ziada ya thamani ya mapato juu ya gharama ya huduma za kipengele cha kukamilishana kwa raslimali zinazomilikiwa.  Inaelekea kwamba hili lingewezekana tu ama katika dunia iliyosimama, dunia ambao leo, na ambamo basi, siku hadi siku, na hivyo ambamo siku hadi siku na mwaka hadi mwaka, mapato hayohayo yatapatikana kwa wamiliki haohao au warithi wao; au wamiliki wote wa raslimali wangekuwa na maono halisi.  Kwa kuwa masuala yote mawili yako mbali na uweli tunaweza kuyapuuza.  Ni nini, basi kinachotokea hasa kwa mali katika dunia yenye mabadiliko yasiyotegemewa?

 

Utajiri wote unajumuisha raslimali za mtaji, ambazo, kwa namna moja au nyingine, zinajumuisha au angalau mwishowe zinaonyesha raslimali vitu za uzalishaji, ambavyo ni vyanzo vya mapato ya thamani.  Mapato yote huzalishwa kutokana na kazi ya binadamu kwa msaada wa mchanganyiko wa raslimali hizo.  Kwa ajili hiyo raslimali zinapaswa kutumiwa katika michanganyiko fulani; ukamilishanaji ni muhimu katika utumiaji wa raslimali.  Njia za ukamilishanaji hii hazitolewi kwa namna yoyote kwa wajasiriamali ambao hufanya, kuanzisha na kutekeleza mipango ya uzalishaji.  Kuna ukweli kwamba hakuna kitu kama uzalishaji A ambamo kinafanya kazi.  Kinyume chake, jukumu la ujasiriamali linajumuisha hasa katika kutafuta, katika dunia ya mabadiliko ya kudumu, ambayo mchanganyiko wa raslimali utavuna, katika masharti ya hivi leo, ziada kubwa zaidi ya kinachopatikana zaidi ya thamani ya kinachowekwa, na katika kubahatisha nini kitafanya hivyo katika hali ya kumakinika ya kesho, wakati thamani ya kinachopatikana/mapato, gharama ya kiingizwa, na teknolojia vyote vitakuwa vimebadilika.

 

Kama raslimali zote za mtaji zingekuwa zenye matumizi mbalimbali tatizo la ujasiriamali lisingejumuisha chochote zaidi ya kufuata mabadiliko ya masharti ya nje kwa kugeuza michanganyiko ya raslimali kuwa mfululizo wa matumizi uliofanywa na mabadiliko haya kuwa na faida.  Kama ilivyo, raslimali zina, kama sheria, mlolongo mdogo wa matumizi mbalimbali, kila moja ni maalumu kwa matumizi kadhaa.  I Kwa kuwa, umuhimu wa marekebisho yakubadilika wakati utajumuisha umuhimu wa mabadiliko katika muundo wa kundi la raslimali, kwa ajili ya “upangaji upya wa mtaji”.  Lakini kila badiliko kwa namna ya ukamilishanaji litaathiri thamani ya raslimali kwa kuanzishwa kwa faida na hasara za mtaji.  Wajasiriamali wataweka zabuni za juu sana kwa ajili ya huduma ya zile raslimali ambazo wameziona zina matumizi yenye faida zaidi, na zabuni za chini sana kwa zile ambazo matumizi yake hayaleti faida kubwa.  Katika hali inayozuia ambayo hakuna (wakati uliopo au ujao) matumizi yanayoweza kupatikana kwa ajili ya raslimali ambayo mapaka sasa imekuwa sehemu ya mchanganyiko wenye faida, ambao raslimali hii itapoteza sifa yake ya raslimali pamoja.  Lakini hata katika suala lenye athari ndogo faida na hasara ya mtaji iliotokana na raslimali za kudumu ni kiambata kisichoepukika cha dunia yenye mabadiliko yasiyotegemewa.

 

Kwa hiyo, mchakato wa soko unaonekana kuwa ni mchakato unaolingana.  Katika uchumi wa soko mchakato wa ugawanyaji mali upya unafanyika wakati wote kabla ya michakato kama hiyo ya nje ambayo wanasiasa wa siku hizi wana mazoea ya kuanzisha, kuonekana kutokufaa kiulinganifu, kama bila sababu nyingine kuliko hiyo ambayo soko huleta mali kwa wale ambao wanaweza kushikilia, wakati wanasiasa hutoa kwenye majimbo yao ya uchaguzi, ambao, kama sheria, hawawezi.

 

Mchakato huu wa ugawanyaji mali upya hauchochewi na hatari za kufuatana.  Wale wanaoshiriki katika mchakato huo hawafanya mchezowa kubahatisha, bali mchezo wa ujuzi.  Mchakato huu, kama ilivyo michakato yote halisi yenye nguvu, unaonyesha upitishaji wa maarifa kichwa hiki kwenda kingine.  Inawezekana tu kwa sababu watu wengine wana maarifa ambayo watu wengine bado hawajayapata, kwa sababu maarifa ya mabadiliko na maana wake huenea polepole na bila ulinganifu katika jamii.

 

Katika mchakato huu anafanikiwa yule anayeelewa mapema kuliko mtu mwingine yeyote kwamba raslimali fulani, ambayo hivi leo inaweza kuzalishwa ikiwa mpya, kwa bei A, kesho itakuwa sehemu ya mchanganyiko wa tija kama matokeo ya ile itakayokuwa na thamani A’.  Faida na hasara vitokanavyo na mauzo ya raslimali iliyochochewa na bahati ya, au umuhimu kwa ajili ya kugeuza raslimali kutoka aina moja ya matumizi kwenda nyingine, kubwa au ndogo kwa ya kwanza hufanya nguvu ya uchumi unaomaanisha mali katika dunia inayobadilika na ndiyo chombo kikubwa cha mchakato wa ugawanyaji upya.

 

Katika mchakato huu haielekei kabisa kwamba mtu huyohuyo ataendelea kuwa sahihi katika kubahatisha kwake kuhusu utumiaji mpya unaowezekana kwa ajili ya raslimali zilizopo au zilizodirika muda baada ya muda, mradi awe kweli mkuu.  Na katika jambo hili la karibuni warithi wake hawaelekei kuonyesha mafanikio ya kufanana – labda wa kweli wakuu, pia.  Katika dunia yenye mabadiliko yasiyotegemewa, hasara itokanayo na mauzo ya raslimali haiepukiki kama ilivyo kwa faida itokanayo na mauzo ya raslimali.  Ushindani baina ya wamiliki mtaji na hali mahsusi ya raslimali za kudumu, hata kama zina “upekee mwingine”.  Zinataka kwamba faida hufuatiwa na hasara kama ambavyo hasara hufuatiwa na faida.

 

Maelezo haya ya kiuchumi yana matokeo fulani katika jamii.  Kama ambavyo wahakiki wa uchumi wa soko siku hizi wanavyopendelea kuchukua msimamo wao kuhusu misingi ya “kijamii”, inaweza ikawa haifai haha kueleza matokeo halisi ya kijamii ya mchakato wa soko.  Tumekwisha tayari kuusema kama mchakato mlingano.  Kwa urahisi zaidi, tunaweza sasa tukayaelezea matokeo haya kama mfano ambao Pareto aliuita “mzunguko wa wasomi”.  Mali haielekei kukaa kwa muda mrefu mikononi mwa watu haohao.  Hupita kutoka mkono kwenda mkono kwa kuwa badiliko lisilotarajiwa huleta thamani, sasa katika raslimali hii maalumu likisababisha faida na hasara. Tunaweza kusema pamoja na Schumpeter, wamiliki wa mali ni sawa na wageni katika hoteli au abiria kwenye treni:  Wakati wote wapo lakini kamwe sio watu haohao kwa muda mrefu.

 

Inaweza kupingwa kwamba hoja yetu inatumika kwa vyovyote kwa sehemu ndogo tu ya jamii na kwamba mzunguko wa wasomi hauondoi kutokuwa na haki katika jamii.  Mzunguko huo unaweza kuwepo miongoni mwa wamiliki wa mali, lakini inakuwaje kwa waliobakia katika jamii?  Ni nafasi gani waliyonayo wale wasio na mali ya hata kushiriki, licha ya kushinda, katika mchezo?  Pingamizi hili, hata hivyo, lingeweza kupuuza sehemu iliyofanywa na mameneja na wajasiriamali katika mchakato wa soko, sehemu ambayo hivi karibuni tutapaswa kurejea.

 

Katika uchumi wa soko, tumeona, utajiri wote wa kiasili una matatizo.  Jinsi raslimali zilivyo za kudumu na jinsi zilivyo na upekee, jinsi mfuatano wa utumiaji unavyowekewa mipaka ambao unaweza kugeuzwa, ndivyo tatizo linapoonekana kuwa dhahiri zaidi.  Lakini katika jamii yenye mtaji mdogo wa kudumu ambamo mali nyingi imelimbikiwa unachukua namna ya akiba ya bidhaa, hasa za kilimo na zinazoweza kuharibika kwa urahisi, vinavyofanywa kwa vipindi vya muda mbalimbali, jamii ambamo bidhaa zitumiwa za kudumu, isipokuwa labda nyumba na samani, hazikuwepo kabisa, tatizo halikuonekana kwa uwazi.  Hiyo ilikuwa, jamii ambamo wachumi maarufu wa zamani walikuwa wakiishi na ambamo walikopa sifa nyingi bainishi.  Katika masharti ya nyakati zao, kwa hiyo, wachumi hawa wa zamani walihalalishwa, kufikia kiwango, kuhusiana na mtaji wote wa namna moja na unaobadilika, kuutofautisha na ardhi, raslimali pekee mahususi na isiyozalisha.  Lakini katika wakati wetu kuna uthibitisho mdogo au hakuna kabisa kwa ajili ya mwainisho huo.  Kwa jinsi bidhaa zilivyo za kudumu zaidi, na jinsi zilivyo aushi, ndivyo ulivyo uwezekanao mkubwa wa raslimali hizo za mtaji kabla ya kuchakaa, zinapaswa kutumiwa kwa madhumuni zaidi ya yale yaliyobuniwa mwanzoni.  Hii ina maana kwamba katika uchumi wa soko la kisasa hakuwezi kuwa ni kitu kama hicho kama chanzo cha mapato ya kudumu.  Muda wa kudumu na ukomo wa matumizi mbalimbali uHoja za Uongobisha kutokuwezekana.

 

Inaweza kuulizwa kama katika kuwasilisha hoja yetu hatukuchanganya mmiliki wa mtaji na mjasiriamali, kwa kudhani kuwa kazi za wa mwanzo ambazo hasa ni za huyu anayefuatia.  Sio uamuzi kuhusu utumiaji wa raslimali zilizopo pamoja na uamuzi ambao unataja bayana namna thabiti raslimali za maji mpya, yaani uamuzi wa uwekezaji, jukumu hasa la kijasiriamali?  Sio kwa ajili ya mjasiriamali kuipanga upya na kuieneza upya michanganyiko ya bidhaa za mtaji?  Je, hatudai kwa wamiliki wa mtaji shughuli za kiuchumi za mjasiriamali?

 

Kwanza hatuhusiki na kudai shughuli kwa mtu yeyote.  Tunahusika na athari za badiliko lisilotegemewa kuhusu thamani ya raslimali na kuhusu ugawanyaji wa mali.  Athari za badiliko hilo litawaangukia wamiliki wa mali bila kujali chanzo kinakotokea.  Kama tofauti baina ya bepari na mjasiriamali ingeweza wakati wote kufanywa kwa urahisi, ingeweza kudaiwa kuwa ugawanyaji upya unaoendelea wa mali ni matokeo kitendo cha kijasiriamali, mchakato ambao wamiliki wa mtaji wana sehemu ndogo tu.  Lakini kwamba mchakato hutokea hasa, kwamba mali inayogawanywa upya na soko, haiwezi kutiliwa shaka, wala kwamba mchakato unachochewa na upitishaji wa maarifa kutoka kituo kimoja cha ujasiriamali kwenda kingine.  Pale ambapo wamiliki wa mtaji na wajasiriamali wanaweza kutofautishwa kwa uwazi, ni kweli kwamba wamiliki wa mali hawashiriki kikamilifu katika mchakato wenyewe, bali wanapaswa kukubali matokeo kimyakimya.

 

Hata hivyo,bado kuna mambo mengi ambamo tofauti iliyo dhahiri kabisa haiwezi kufanyika.  Katika dunia ya sasa mali hasa huchukua namna ya dhamana.  Mmiliki wa mali nii mdau hasa.  Je, mdau ni mjasiriamali?  Profesa Knight anatetea kwamba, yeye anafuatia waandishi kuanzia Walter Rathenau 2 hadi Bw. Burnham wamemnyima hadhi hiyo.  Bila shaka, jibu linategemea, tafsiri yetu ya mjasiriamali.  Kama tunamwelezea kama mwenye kubadilika badilika, ni wazi kuwa mdau ni mjasiriamali. Lakini katika miaka ya hivi karibuni kuna tabia inayoongezeka ya kumwelezea mjasiriamali kama mpangaji na mtoa maamuzi.  Kama ni hivyo, wakurugenzi na mameneja ni wajasiriamali, lakini wadau, inaelekea, sio.

 

Bado tunapaswa kuwa makini katika kutoa uamuzi.  Mojawapo ya majukumu yaliyo muhimu sana ya mjasiriamali ni kutaja bayana namna madhubuti ya raslimali za mtaji, kusema ni majengo gani yasimamishwe, bidhaa gani zihifadhiwe, n.k. kama tuko wazi kutofautisha baina ya bepari na mjasiriamali lazima tuchukulie kuwa mjasiriamali “halisi” asiye na mali yake mwenyewe, hukoa mtaji wa fedha, k.v. katika namna isiyo mahsusi, kutoka kwa wamiliki “halisi” wa mtaji. 3

 

Lakini, je, wakurugenzi na mameneja wa ngazi za juu katika shirika wanatoa maamuzi yote?  Maamuizi mengine mengi hayakaliwi na mameneja, wasimamizi wa ujnzi, n.k.? Je inawezekana kweli kumwonyesha “mjasiriamali” katika dunia ambamo shughuli za kimeneja zimeenea?

 

Kwa upande mwingine, uamuzi wa mmiliki wa mtaji kununua hisa mpya katika kampuni A badala ya kampuni B ni uamuzi pia unaoelezea.  Ukweli ni kwamba huu ni uamuzi wa awali ambao maamuzi yote ya kimeneja ndani ya kampuni hatimaye hutegemea, kwani bila ya mtaji kusingekuwa na kitu cha wao kukelezea.  Inaelekea tunapaswa kutambua, , kwamba maamuzi yanayoelezea ya wadau, wakurugenzi, mameneja, n.k., mwishoni mwa yote ni kutegemeana, ni viungo katika mnyororo.  Yote ni maamuzi yanayoelezea yanayotofautishwa tuna kiwango cha uthabiti unaoongezeka kwa jinsi tunavyoelekea chini ya ngazi ya shirika.  Kununua hisa kwenye kampuni A ni uamuzi unaoupa mtaji namna iliyo thabiti kidogo kuliko unavyofanya uamuzi wa meneja wa karakana kuhusu vifaa gani vitengenezwe, bali ni uamuzi wa kuelezea hata hivyo, na mwingine ambao unatoa vifaa kwa ajili ya meneja wa karakana kuchukua hatua.  Kwa ajili hiyo tunaweza kusema kuwa wamiliki wa mtaji wanatoa uamuzi wa kuelezea wa hali ya juu sana.

 

Hivyo basi, tofauti baina ya mmiliki mtaji na mjasiriamali wakati wote sio rahisi kufanywa.  Kwa kiasi hiki, basi tofauti kati ya wajasiriamali halisi, ya kuunda na kusambaza upya michanganyiko ya raslimali za mtaji, na wamiliki wa kimyakimya wa raslimali, ambao wanapaswa kukubali ukweli wa nguvu za soko kuhusu kufanikiwa kwa wajasiriamali “wao”, imetiwa chumvi.  Hata hivyo, wadau hawabaki bila utetezi katika haya.  Kama hawawezi kuwashawishi wakurugenzi wao kuondokana na hatua fulani, kuna jambo moja wanaweza kufanya:  Wanaweza kuuza!

 

Lakini inakuwaje kwa wenye dhamana?  Wadau wanaweza kutengeneza faida na hasara itokanayo na mauzo ya raslimali; mali zao zinaathiriwa na nguvu za soko.  Lakini wenye dhamana wanaelekea wote kuwa na msimamo tofauti.  Je, sio wamiliki wa mali ambao wanaweza kudai kuwa na kinga dhidi ya nguvu za soko tulizoelezea, na hivyo dhidi ya mchakato wa ugawanyaji upya?

 

Kwanza kabisa, bila shaka, tofauti ni kiasi tu cha kiwango, bado hakuna kinachofahamika, kutokana na kushindwa kwa mipango, menejimenti kukosa ufanisi, au kwa mazingira ya nje ambayo hayajatabiriwa, wenye dhamana wanapaswa kuchukua kampuni na hivyo kuwa wadau wasio wa hiari.  Hata hivyo ni kweli kwamba wenye dhamana wengi ni wamiliki wa mali wanaosimama, kama ilivyokuwa kama tulivyokwishaelezea, kutoka kwenye chanzo cha mabadiliko yanaathiri thamani ya raslimali zilizo nyingi, ingawa sio kweli kwa zote.  Athari nyingi zinazotokana na chanzo hiki kingekuwa, kama kilivyokuwa, kuingiliwa na nyingine kabla ya kuwafikia wenye dhamana.  Wakati “gia” ya mtaji wa kampuni, tabaka la kinga ya hisa lilivyo jembamba zaidi, ndivyo athari zaidi zitakavyowafikia wenye dhamana, na ndivyo watakavyokuwa wameathiriwa zaidi.  Hivyo ni makosa kabisa kutaja suala la wenye dhamana ili kuonyesha kuwa wapo wamiliki wa mali waliosamehewa katika shughuli ya nguvu za soko tulizoelezea.  Wamiliki wa mali kama tabaka hawawezi kusamehewa hivi, ingawaje baadhi wanaweza kuathirika zaidi kuliko wengine.

 

Zaidi ya hayo, kuna mambo mawili ya nguvu za kiuchumi yanayosababisha faida na hasara zitokanazona mauzo ya raslimali, ambazo kutokana na hizo, kwa hali ya mambo haya, mwenye dhamana hawezi kujilinda mwenyewe, hata hivyo kwa vyovyote ulinzi mzito wa hisa utakavyokuwa: kiwango cha riba na mfumko wa bei.  Kupanda kwa viwango vya riba vya muda mrefu kutashusha thamani za dhamana ambapo wenye hisa wanaweza bado kutumaini kujifidia wenyewe kwa faida kubwa sana.  Wakati kushuka kutakuwa na athari iliyo kinyume.  Mfumko wa bei unahamisha mali kutoka kwa wawia kwenda wawiwa, pale ambapo kupungua kwa jumla ya fedha zitumiwazo ili kudhibiti bei kuna athari iliyo kinyume.  Katika mambo yote, bila shaka ipo mifano ya ugawanyaji upya wa mali ambayo tumefanya vizuri.  Tunaweza kusema kwamba kwa kiwango cha riba cha muda mrefu na bila badiliko katika thamani ya fedha, kuathirika kwa haraka kwa mali ya wenye dhamana kwa badiliko lisilotegemewa kutatugemea msimamo wao unaohusiana dhidi ya wenye hisa, “umbali wao kiuchumi” kutoka kwenye usumbufu; wakati mabadiliko ya riba na mabadiliko katika thamani ya fedha yatarekebisha msimamo huo unaohusiana.

 

Wamiliki wa dhamana za serikali, bila shaka, wanaondolewa kutoka kwenye athari nyingi za badiliko lisilotegemewa, lakini hasa kutoka kwenye zote.  Ili kuwa na uhakika, hawahitaji ulinzi mkubwa wa hisa, kuwakinga dhidi ya nguvu za soko ambao zinarekebisha bei na gharama.  Bali mabadiliko ya riba na mfumko wa bei ni tishio kwao kama ilivyo kwa wamiliki wa dhamana wengine.  Katika dunia ya mfumko wa bei wa kudumu tuliomo sasa hivi, kuziona mali katika namna ya dhamana za serikali kutokustahili katika mmomonyoko unaofanywa na nguvu za badiliko kungekuwa ni upumbavu.  Bali kwa vyovyote kuwepo kwa deni la serikali sio matokeo ya uendeshaji wa nguvu za soko.  Ni matokeo ya shughuli za wanasiasa wenye shauku ya kuhudumia majimbo yao kutokana na jukumu la kupaswa kulipa kodi ambazo vinginevyo walipaswa kulipa.

 

Jambo kubwa ambalo tumesisitiza katika makala haya, ni ugawanyaji upya wa mali unaosababishwa na nguvu za soko katika dunia yenye badiliko lisilotegemewa, ni uweli wa maoniya pamoja.  Kwa nini, basi, je linapuuzwa mara kwa mara?  Tunaweza kuelewa kwa nini wanasiasa wanachagua kulipuuza:  hata hivyo, majimbo yao ya uchaguzi yaluiyo mengi hayaelekei kuathiriwa nayo moja kwa moja, na kama ilivyoonyeshwa kwa upana katika suala la mfumko wa bei hawataweza kulielewa.  Lakini kwa nini wachumi waamue kulipuuza?  Kwamba namna ya ugawanyaji wa mali ni matokeo ya utendaji wanguvu za kiuchumi, ni aina ya pendekezo ambalo, mtu angefikiri, angeweza kuziomba. Kwa nini, basi wachumi wengi wanaendelea kuuona ugawanyaji wa mali kama “datum” kwa maana ya pili iliyotajwa hapo juu?  Tunaridhia kwamba sababu haina budi kutafutwa katika kushughulikia kunakoongezeka  matatizo ya ulinganifu.

 

Tuliona kabla kwamba namna za mfuatano wa ugawanyaji wa mali ni wa dunia isiyo na ulinganifu.  Faida na hasara zitokanazo  na mauzo ya raslimali zinazojitokeza kwa sababu raslimali za kudumu zinapaswa kutumika kwa njia zisizopangiwa, na kwa sababu baadhi ya watu wanaelewa vizuri sana na mapema kuliko watu wengine maana ya mahitaji na raslimali za dunia inayozunguka.  Ulinganifu maana yake ni uthabiti wa mipango, bali ugawanyaji upya wa mali unaofanywa na soko ni matokeo ya tendo lisilo thabiti.  Kwa wale waliofundishwa kufikiri kuhusiana na ulinganifu labla ni kawaida tu kwamba michakato hiyo kama tulivyoielezea inapaswa kuonekana “kutokuheshimika”.  Kwao wao nguvu halisi za kiuchumi ni zile zinazoelekea kuanzisha na kudumisha ulinganifu.  Nguvu zinazofanya kazi tu pasipo na ulinganifu zinachukuliwa kuwa hazivutii na kwa hiyo mara kwa mara zinapuuzwa zote.  Yawezekana kukawa na sababu mbili za uuzwaji huo.  Bila shaka ipo imani inaosema kuwa mwelekeo kuelekea ulinganifu haipo kwa ukweli na kwamba, katikahali yoyote inayofikiriwa, nguvu zinazoelekea kwenye ulinganifu siku zote zitakuwa na nguvu sana kuliko nguvu za upinzani.

 

Lakini sababu nyingine yenye nguvu kama hiyo, tunayoweza kuishuku ni kushindwa kwa wachumi wanaoshughulika na ulinganifu wa kustahimili nguvu zisizo na ulinganifu.  Nadharia yote haina budi kutumia mifano iliyo wazi na yenye kueleweka.  Kama mtu ana mfano mmoja tu kama huo mambo mengi ambayo hayaelekei kufaa kwenye mpango yanaweza kubakia kutokutolewa maelezo.  Upuuzaji wa mchakato wa ugawanyaji upya sio tu wa umuhimu unaofika mbali katika uchumi wa kisiasa kwa kuwa unatuzuia kuelewa baadhi ya sifa za dunia tunamoishi.  Aidha ni muhimu kimetholojia katika eneo la kati la fikra ya kiuchumi.

 

Hakika, hatusemi kwamba mchumi wa sasa, aliyesoma sana katika sarufi linganifu, asiyefahamu ukweli wa soko, hawezi au hayuko tayari kustahimili badiliko la kiuchumi; ambalo lingekuwa halina maana.  Tunasema kwamba amejiandaa vizuri kushughulikia tu aina za mabadiliko ambayo hutokea kulingana na mwelekeo imara.  Katika fasihi nyingi zilizoko wakati huu badiliko linafikiriwa kuwa ni namna ya mpito kutoka ulinganifu mmoja kwenda mwingine, k.v. kulingana na mituamo linganishi.  Kuna hata wachumi wengine ambao, wakiwa wameelewa vibaya wazo la Cassel la “uchumi sawa unaoendelea”, hawawezi kuyafikiria maendeleo ya kiuchumi kwa namna nyingine yoyote! 4 Upitaji huo wa taratibu kutoka ulinganifu mmoja (muda mrefu au muda mfupi) kwenye vikwazo vingine sio tu majadiliano ya mchakato ambao tunauhitaji hapa, bali kwa michakato yote ya kweli ya kiuchumi.  Kwa kuwa mpito huo wa taratibu utafanyika tu pale ambapo msimamo mpya wa ulinganifu tayari unafahamika kwa ujumla na kutarajiwa kabla ya kufikiwa.  Pale ambapo hili haliko hivyo, mchakato wa kubahatisha (Walras’ “tatonnements”) utaanza ambao mwishoni unaweza au unaweza usielekee kwenye msimamo mpya wa uliganifu.  Lakini hata pale ambapo lipo, ulinganifu mpya uliofikiwa hatimaye hautakuwa ule ambao ungefikiwa mara moja kama kila mtui angeutarajia mwanzoni, kwani tatakuwa ni matokeo yaliyolimbikizwa ya matukio yaliyotokea “njiani” akielekea huko.  Miongoni mwa mabadiliko ya matukio haya katika ugawanyaji wa mali unachukua nafasi muhimu.

 

Hivi karibuni Profesa Lindahl 5 ameonyesha ni kwa kiwango gani mfano wa kiuchambuzi wa Keynes unadhoofishwa na uamuzi wake wa wazi wa kubana nguvu mbalimbali za kiuchumi katika msingi wa Procrustean wa uchambuzi wa ulinganifu wa muda mfupi.  Wakati akipenda kuelezea mbinu ya utendaji nguvu mbalimbali, Keynes, alitoa mfano wake katika kieleza cha mfano wa mlinganyo sawia, ingawa nguvu mbalimbali alizochunguza zimekuwa za vipindi vya muda tofauti.  Somo la kujifunza hapa ni kwamba mara tutakapojiruhusu kupuuza vidokezo muhimu kuhusu soko, maarifa haya tofauti, baadhi ya watu kuelewa maana ya tukio kabla ya wengine, na kwa ujumla, ruwaza ya matukio ya muda, tutashawishika kueleza “mapema” athari katika muda mfupi wa ulinganifu.  Na hivi karibuni tutajiruhusu pia kusahau kwamba yaliyo na maslahi hasa ya kiuchumi sio mlingano, hata kama yapo, ambayo kwa namna yoyote yanatiliwa shaka, bali yanayotokea baina yao.  Wafanyakazi wasaidizi wa muda wanaoajiriwa na wachumi wenye mantiki kama dhana ya ukomo” 6 wanaweza kusababisha matokeo yenye maafa makubwa wakitumika vibaya.  Kushughulikia mlingano hatimaye kunaanzia kwenye utatanishi baina ya mhusika na lengo, baina ya akili ya mtazamaji na akili za wa waigizaji wanaotazamwa.  Bila shaka hakuwezi kuwa na sayansi yenye mfumo maalumu bila yakuwa kiunzi cha marekeleo kinachofuatana, lakini hatutegemei kupata mfungamano kwa kuwa kiunzi chetu cha marejeleo kinahitaji vitu vilivyoko tayari vimetayarishwa kwa ajili yetu katika matukio tunayoona.  Ni kinyume, cha jukumu letu la kuzalisha kwa juhudi za kiuchambuzi.  Katika sayansi jamii, kuna matukio tunayoyapendelea hasa kwa sababu shughuli za binadamu ndani yake haziwiani zenyewe, na ambamo mfungamano, kama hatimaye unatolewa kwa muingiliano wa akili juu ya akili.  Makala haya yanashughulikia uchunguzi wa tukio kama hilo.  Tumejitahidi kuonyesha kuwa jambo la kijamii lenye umuhimu linaweza kueleweka kama litawasilishwa kwa namna ya mchakato unaoonyesha mwingiliano wa akili kwa akili, na sio vinginevyo.  Watengeneza mitindo, ekonometriki na vinginevyo, kwa kawaida hupaswa kuepuka mada kama hizo.

 

Inatumainiwa sana kwamba hapo baadaye wachumi wataelekea kupunguza uegemeaji kuliko walivyokuwa hapo mwanzo kutafuta vilivyotengenezwa tayari, bali hali ya kujifanyia mfungamano na kwamba watakuwa na raghaba kubwa katika njia mbalimbali za akili ya binadamu inayofanya kazi kuzalisha mfungamano kutokana na hali ambayo hapo awali haikuwa na mfungamano.

 

MAELEZO

   [1]     Hoja iliyowasilishwa katika kinachofuatia inatokana na wazo zuri ambalo kwanza lilianzishwa na Profesa Mises katika “Das festangelegte Kapital”, kwenye Grundprobleme der Nationalökinomie uk. 201 – 14. [Tafsiri ya Kiingereza kwenye Epistemological Problems of Economics (Ney York: D Van Nostrand, 1960), u. 217 – 31].

 

 [2]      Vom Aktienwese, 1917

 

 [3]   Maelezo haya, bila shaka yana athari za kijamii.  Wale wanaoyakubali hawataweza kuwaona wajasiriamali kama tabaka linalowapa kisichowezekana wale wasio na mali zao wenyewe.  Kwa vyovyote kitakavyokuwa kiwango cha “kukosa ubora cha soko la mtaji” tunachagua kufikiria hakitatupa maokeo haya.

 

[4]     Kwa ajili ya uhakiki unaofaa wa aina hii ya kutengeneza vielelezo, tazama Joan Robinson, “The Model of an Expanding Economy, “Economical Journal 62 (Machi 1952): 42-53.

 

  [5]     Eriki Lindahl “On Keynes’ Economic System, Economic Record 30 (Mei 1954):  19-23; 30 (Novemba 1954): 159-71.

 

 [6]    Ludwig Von Mises, Human Action (New Haven:  Yale University Press, 1949), uk. 352.

RELATED ARTICLES